Report maalum: Madanguro ya kichina chanzo cha mauaji ya wachina

Daahh malizia basi
JamiiForums-1347950702.jpg
 
Inaendelea sehemu ya pili

Wale mabinti kuna mmoja ama wawili hao ni spesheli ya boss ama watu wake maalum..hao huwa hawagusi sana ama kabisa na ukimgusa huyo dau lake si la kitoto
Wabongo tunapenda ligi na kuoneshana ufahari lakini bado hatujawafikia wachina...Kuna mchina alikuja kufika bei kisha akamtorosha yule asali wa boss.. Boss hakuweza kwenda polisi bali akaweka kisasi
Katika kumtafuta mbaya wake akakuta tayari keshapewa bonge la shavu na passport mpya juu( baada ya kuripoti kupotelewa na ya kwanza) hayo yalifanyika ubalozini.. Alipotaka kulianzisha akatolewa mguu wa kuku ikabidi awe mpole atimue

Huyu mchina aliyemtorosha yule binti naye akamtumia kuwaleta wengine kisha wakaenda kupanga ghorofa lile lile la wale wengine, hii ilikuwa ni kuoneshana utemi tuu, kisha akaleta vitu vya ukweli sana na promo kibao..

Ikawa sasa ni mashindano ya kugombea wateja,.. Bifu ikatoka kwa mabosi mpaka kwa machangu wenyewe.. Kuna siku zikapigwa sana hapo ghorofani mpaka kuumizana kabisa.. Ishu ikazimwa kimyakimya na wakutibiwa wakatibiwa..Mpaka kufikia hapo ikawa kuna makundi mawili ya mabosi mahasimu kabisa ..

Kundi la kwanza lile la zamani boss akawa na bastola na mabaunsa wa kibongo, kundi la pili likawa na boss mwenye bastola na wapiga king fu kwa kichina.. Patamu hapo..! Ikawa sasa ni mwendo wa fitina, vitisho, kutambiana na kutunishiana misuli
Hayawi hayawi mwisho yakawa.. Kuna siku wakakutana mahali zikaanza kupigwa.. Huyu wa zamani mwenye mabaunsa wa kibongo (wanatoka Gym ya vijana pale Mwananyamala)... Hawa wakawachakaza wale wapiga kung fu , boss wao alipoona wamezidiwa akawapelekea moto na kujeruhi wawili mchina na mbongo na kumuua mmoja..!

Hii kesi ilimalizwa kimyakimya na marehemu akaenda kuzikwa kwao Bagamoyo.. Haya makundi mawili yalihasimiana mpaka yakawa kero kule Masaki yalikokuwa yamepanga...
Kwa kawaida wale mabinti huwa hawakatiwi vibali bali vya ukazi bali ni business visa za miezi mitatu mpaka sita baada ya hapo huhamishiwa nchi nyingine maana maboss wana mitandao yao..!

Hawa mabosi sasa wakaanza kuchomeana serikalini.. Waswahel wanasema vita ya panzi ni furaha ya kunguru, wakaaza kutoleana siri za biashara zao chafu na watu wanaoshirikiana nao toka mamlaka za serikali.. Hili sakata liliondoka na wengi huko mamlakani lakini na wachina nao wakaishia kutimuliwa nchini...

Hapa pamoja na mengine madogo madogo ndio palikuwa chanzo cha kuwa na makundi hasimu ya hizi biashara chafu hasa kusafirisha binadamu na kuwatumikisha kingono..

Haya niliyoandika leo ilikuwa ni muhtasari wa asili ya tatizo na yalitokea kabla ya 2015.. Ambapo kwa kipindi hicho wachina walinunua silaha kwa wingi sana.. Na biashara za kamari na uchangu zilishamiri.. Kuna mengi sijayaandika hapa kwakuwa nimechagua kipengele cha uchangudoa
Baada ya 2015 hizi biashara zilipotea kwa sehemu kubwa na mabinti wa kibongo wakapanda chati
Kilichonisukuma niandike sasa ni haya mauaji yaliyonza kutikisa tena na kesi kuwa nyingi.. Nitarejea nkmalizie sehemu ya tatu na ya mwisho
Nasubiri mwendelezo
 
Back
Top Bottom