Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 898
Kwa ufupi tu ni kwamba amepwaya sana katika wadhifa huo wa meya wa manispaa ya ilala. Na hilo limewaumiza sana vijana ambao wamekuwa wakijitahidi kudai nafasi za uongozi ili waongoze kwa mifano.
Mapato ya manispaa ya ilala yameongezeka toka sh. 16 bilioni hadi sh. 26 bilioni, lakini hakuna shughuli yoyote ya kimaendeleo inayoonekana kufanywa kwa maslahi ya wananchi.
Masoko ni machafu, mitaro imeziba, mitaa ni michafu, hospitali,zahanati na vituo vya afya havina madawa, vifaa tiba wala wahudumu wa kutosha hasa vilivyoko nje ya mji kama ukonga, kitunda,chanika na kwingineko. Barabara za manispaa ni mbaya sana na hazifanyiwi matengenezo yanayostahili ili zipitike muda wote wa mwaka.
Anachofanya sasahivi kwa umakini ni kukusanya fedha za kununulia ubunge 2015! Hana muda na shughuli za maendeleo ya wananchi wa manispaa ya ilala.
Asante Hossam
Kwa faida ya wapenda maendeleo.
Bsc Electronics & Communication UDSM 2005
Atec II NBAA 2003
Cert in Law UDSM 2005
Siku mbili za kuona wananchi ,Monday & Friday
Kata ya Gongolamboto ni mpya kwa sasa tunatumia ofisi za kata ya Ukonga.
Website ya Council www.imc.co.tz
Namba ya wapiga kura ipo,lakini utaratibu mzuri ni kutumia forum zilizopo kuwasilisha.
Twitter Jerry Silaa
Upo muda maalum wa kukutana na wapiga kura. Kwa ujumla wananchi wanawakilishwa na waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa mitaa. Hawa they are free to see me anytime.
Mimi sio mtumishi wa umma, ni kiongozi wa umma na ninadeclear mali na madeni chini ya Tamko kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi kila mwaka kabla ya 31st Dec.
Sina mshahara.
Posho 240,000 kwa mwezi na sitting allowance 60,000 kwa vikao ninavyohudhuria with a maximum ya vikao vinne kwa mwezi.
Hayo ya Ilala watajibu wenyewe.
Ilala ni manispaa sio jimbo na upo mango mkakati nitauweka kwenye website.
Sheria ya umaadili ya TZ ni tofauti ya marekani na haitoi fursa ya kudeclear zawadi. Lakini mimi sio mpokeaji mzuri wa zawadi za kiofisi. Integrity yangu kwa wafanyabiashara u can reserch.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya madiwani ya mwaka 1979 inamtaka udiwani kama shughuli ya kujitolea na diwani anapashwa kuwa na shughuli tofauti na nafasi nyingine za umma, udiwani hauna reflection ya lifestyle. Na kwa kuwa kiongozi wa metropolitan hakuna lifestyle utayoishi ikareflect wananchi wote.
Ushiriki wa shughuli za umma ndio majukumu ya msingi ya kiongozi ws kisiasa. Majibu mazuri ungewauliza waigakura wa Gongolamboto na General Public, majukumu nimengi na pale muda unaporuhusu tunashiriki. Sasa kama kuna mwandishi amecover ukaiita publicity sawa, lakini na yenyewe muhimu ili watu kama nyie muone ushiriki.
Uchaguzi wa 2015 kwa style yangu ya siasa utazungumzwa 2015. Na kwa taarifa yako siasa ya nchi hii what u have done itakupa 20-30 %.
Bajet ya umeya : fomu lak 2, mafuta ya kuzungukia kuomba kura, simu ya logistics + 7m ya udiwani.
Facebook Jerry Silaa
Amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Amemaliza Mwaka 2005, Degree ya BSc. Electronics, wakati akiwa chuo amewahi kushika uongozi kama Waziri wa Mambo ya Kijamii.
Nawasilisha
Mh. Silaa asante sana kwa majibu yako mafupi lakini yanayotia moyo na kuonyesha kwamba wewe ni kiongozi msikivu. Maana hata kujibu humu unaonyesha wewe ni mtu wa namna gani. Salute
Mh. Kama kijana mwenzako, naomba nikiri kwamba uongozi wako una maana kubwa kwetu vijana. Utendaji wako utatufanya vijana wengi tuwe na imani katika siasa au tuikimbie tukiamini ni sehemu ya ufisadi kujineemesha. So keep up the hard work. Its never easy lakini yanawezekana.
Nina ushauri hapa kwako na ofisi yako katika kutafuta suluhu ya mambo kadhaa.
1. Wilaya yetu ya Ilala ni chafu ndugu yangu. Uchafu umezidi kila sehemu na rarely anybody cares. Mimi ombi langu, kwa nini usilivalie njuga hili swala mkuu? Kwanza kabisa ningeshauri uanze na wote wanaokabidhiwa tenda ya kuzoa takataka. Ofisi yako ihakikishe kwamba kila anayeomba tenda hiyo ana vifaa vya kutosha na wafanyakazi wa kutosha. Naamini na wewe umeshashuhudia magari chakavu yakiwa yanasomba taka hapa mjini, sasa unashindwa kuelewa tofauti ya uchafu na gari iliyobeba uchafu. Maana gari nyingi ni chakavu kuliko maelelezo. Hili jambo linakera na inaonekana viongozi either wana interests na haya makampuni kama shareholders au they simply dont care!
2. Ofisi yako ihakikishe haya makampuni yanazingatia sheria za kazi kwa watumishi wao. Ni jambo la kusikitisha unakuta akina mama wakiwa wanafagia barabara za mjini hapa bila protection yoyote kwenye jua la Dar. Ni hali inayotishia usalama wa afya zao. Hili nalo livalie njuga. You will make a difference in the lives of your fellow citizens. Kampuni kama inataka tenda ya usafi ihakikishe wafanyakazi wanapewa vitendea kazi stahiki kulinda afya zao.
3. Kuna swala la huduma za msingi kama maji, afya nk. Hebu jitahidi mkuu ujipambanue kwa kuonyesha kwamba inawezekana. Arguably matatizo ya hapa mjini ni mengi na yanahusisha cross-section ya idara. Lakini wewe waweza kufanya mengi na wananchi certainly tutakusupport.
4. Swala la foleni mjini. Ningeshauri uwasiliane na idara nyingine husika muangalie namna ya ku-control haya magari yanayojazana mjini kati (CBD). Seriously najua wengi humu hawatakubaliana na mimi, lakini kutokana na miundo mbinu yetu ilivyochoka na michache..you guys should make it difficult to drive in town especially kwenye rush hours! ILA hili liende sambamba na miundo mbinu kama kuboresha public transport. Ultimately hatuwezi ku-pretend kwamba Dar itaendelea kwa mtindo huu bila kuchukua maamuzi magumu na 'unpopular'. Kama kulipisha kodi kila gari linaloingia mjini katika mida fulani fulani. Ila as I said, ufanye hivi kwa ku-invest in alternative transport mechanism.
5. Mh. Silaa, mimi nakupongeza na naelewa kabisa uongozi wa sehemu kama Dar si lelemama. Lakini I can assure you, ni watanzania wa leo wengi wanaelewa ukifanya kazi inayonekana we can support you kufanya makubwa zaidi.
6. JIPAMBANUE uondokane na hii sense ya 'business as usual' kwenye mambo ya msingi yanayotuhusu wakazi wa mji huu.
Ipe heshima yake kaka ni Bsc. Electronics and Telecomunication.
Mheshimiwa Jery Slaa naomba kukuuliza swali kama mpiga kura wako..
Mkuu
Kuna kipindi mzee Masaburii alitaka kuvunja mkataba na yule contractor uchwara anaeendesha soko la feri kwa kua hafagii wala vyoo japo vya shimo hajaachimba nakumbuka ulikawa mkali sana eti mzee anaingia kwenye 18 zako, nadhani aligusa maslahi flani... vipi mmefikia wapi na huyu dalali wa lile soko, mmesham terminate au bado anapeta tu, Kwa faida yako pale hua napita sana kula pweza na nakuta maji machafu yanachuruzika hadi barabarani kule!!i hadi hamu ya kul octopus wangu kwa ajili bukande inapotea mzee mwezio
Nawasilisha
Kwa sasa hiyo kozi inaitwa hivyo, ingawa sisi tulisoma course za Telecomunication Engineering lakini Degree program iliitwa Bsc Electronics science and communication.