Uchaguzi 2020 Remix ya Wimbo wa Taifa; CHADEMA mmezingua sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,858
CHADEMA WAMEONYESHA UBINAFSI: NI KUHUSU WIMBO WA TAIFA.

Na, Robert Heriel

Nimesikitishwa sana na kile nilichokiona leo kwenye mitandao ya kijamii. Ni video moja ikiwaonyesha wanachama wa CHADEMA wakiimba Remix ya wimbo wa Taifa.

Kuimba Remix ya wimbo wa taifa sio kosa na wala sina neno nao. Lakini mahali waliponichefua ni ujumbe wa maneno waliyoyabadili mule kwenye ule wimbo. Ni maneno ya kipumbavu, kibinafsi, kiuchoyo na kibaguzi mno.

Sikutegemea CHADEMA kama wangefanya kosa la mapema namna hii. Sijajua ni nani alipendekeza maneno hayo, sikufikiri kama kuna mtu angeweza kushauri yawepo maneno hayo achilia mbali ujasiri wa kiwehu uliotumika kuimba mbele ya halaiki,huku kamera zikirekodi. Unajua kuna mambo ni yaaibu sana kuyasikia na kuyaona.

CHADEMA wameonyesha ubinafsi wa hali ya juu mno. Kitendo cha kuimba kuwa "Mungu aibariki Chadema na watu wake" kinaweza kuelezea mambo kadhaa yaliyojifisha ndani ya Chama hiko,

CHADEMA wakati mnataka Mungu awabariki ninyi na watu wenu, hamkufikiri habari za wenzenu wa ACT- WAZALENDO, hamkuwafikiri CUF, haya; je NCCR, vipi TLP, Je hao CCM nao hawataki hizo baraka mnazomuomba Mungui?

Je na sisi tusio na Vyama ambao bila shaka ndio wengi zaidi, je nasi hamjataki tupate baraka za Mungu.

Jambo moja ni muhimu, sisi sio watu wa CHADEMA wala sio Wanachadema, sisi sio watu wa CCM wala sio wanaccm, Sisi sio watu wa ACT wala sio wanaACT halikadhalika na vyama vingine. Sisi ni Watanzania na ni watu waTanzania.

Wimbo wa Taifa ulitungwa zamani kidogo, kinachonishangaza ni CHADEMA kuzidiwa akili na Mtunzi wa nyimbo hiyo ambaye amaitaja Tanzania kisha akawataja na watanzania.

Lakini nyie kwa ufinyu wa fikara mkaona muweke CHADEMA na watu wake bila kufikiri vyema.

Wimbo wenu umedhihirisha mambo yafuatayo
1. Ubinafsi
Kujiombea baraka wenyewe ni dalili ya ubinafsi mkubwa ambao kwa sasa hamuuonyeshi kwa sababu hamkupewa nafasi ya kuuonyesha
2. Ninyi sio wazalendo kwani mpo na maslahi ya Chama zaidi kuliko nchi. Ndio maana mmeomba baraka kwa Mungu kuwa awabariki Wanachadema badala ya kuomba baraka kwa Watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kivyama.
3. Kuzidiwa akili na Mtunzi wa nyimbo
Badala muboreshe kazi ya mtunzi wa nyimbo hiyo ambayo ni nyimbo ya taifa, ninyi mmezidi kuboronga. Kuzidiwa akili na mtunzi wa zamani si dalili njema.

Sijafurahishwa na jambo hilo mimi kama Taikon, sikulitegemea.

Ninyi kila siku mnamlalamikia Magufuli kwa kuwazuia msifanye siasa, kuzuia vyombo vya habari kuwarusha, lakini kile mnachokikataa ndio hicho hicho mnakionyesha mbele za Umma.

Ikiwa mnataka baraka kwenu pekee yenu mkiwa hamjachukua dola, je mkichukua dola mtataka nini zaidi ya dua yenu kwa Mungu. Je hamkusoma kwenye magombo ya kale yasemayo; waombeeni adui zenu tena wale wanaowaudhi waombeeni baraka.

Mmezingua hiyo Remix

Mmezingua sana, sisi tusio na vyama nasi twataka baraka, sisi sio CHADEMA wala sio CCM sisi ni Watanzania.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Naona umeweka namba ya simu kwenye bandiko lako. Bila shaka hii ni safari ya kusaka teuzi kwa watawala.
 
Mawazo ya Ki Lissu Lissu haya. Wimbo wa Taifa ni suala ambalo halijawahi kuwa issue at any time katika kuongeza umoja wa kitaifa
Mawazo haya ambayo hayamwongezei mwananchi afya wala shibe ni ya kijinga sana!

Ina sikitisha kuwa hata watu waliosoma wanakuwa kama wana bangi kichwani, cronic self propagation.
 
Jamani wekeni basi huo wimbo hapa, ili nasi tuusikie na kuona jinsi walivyochemka! Chadema jamano!🤣
 
Huoni tumeusikia?
Mimi sikuwa ndani ya mkutano, nilikuwa nje lakini nimeusikia. Unataka kuniambia nini sasa? Bado ulikuwa wa ndani ya mkutano?
Kwahiyo sala zinazofanyika ndani ya misikiti na na makanisa mitaani wakazi wote majumbani mwao wanashiriki! Shikamoo.
 
Back
Top Bottom