robert sendabishaka
JF-Expert Member
- Dec 11, 2015
- 3,142
- 3,338
Bwana Kisandu amani kwako! baada ya salamu, nakiri wewe ni kaka yangu, umenitangulia miaka 4. jambo la muhimu jifunze kucheza kwa furaha yako upendavyo lakini usitoke nje ya mapigo ya ngoma yenyewe 'mkito/lele' naamini kuwa panapopigiwa kelele pana kasoro. raha ya jf hatufahamiani kwa sura lakini tunafajamiana kwa hoja zilizoshiba, itikadi na milengo tofauti tofauti. ukiona wadau humu wanakosoa juu ya unachotumegea, fanya maamzi sahihi ya 'mabadiliko' mada zako kiukweli huwa zinahitaji akili pana na tulivu kuzielewa na hata msomaji akijitahidi kuziongezea ujuzi wa ziada kupata chochote aghalabu hakina tija iliyotarajiwa.
*upande wangu nakupongeza kwa kuwa muwazi juu ya kiwango chako cha elimu na jinsi ulivyoisotea hadi ikakufikisha hapo ulipo 'mwalimu wa kiswahili'
*kwa uzi wako wa leo 'cv' umenilisha kitu kingine kipya ambacho hakitanipa shida sana kuelewa kwanini unapenda sana 'kujaribu' na kujiamiani 'umefanya'
*pengine kuna hatua kadhaa uliruka katika maisha ya makuzi na sasa inakugharimu.
*kuna pahala ulipata kusema ulipishana kauli na viongozi wako wa dini hata ukachukua hatua ya kujiondoa ktk huduma kisa tu haupandishwi daraja, isije kuwa madhira yake yanakuandama mkuu.
*jiulize kwanini kukosolewa na kuonekana una upungufu isivyo kawaida kunatokana na nini?