Religion Leadership CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

Religion Leadership CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

Mkuu wafate wataalamu wakushauri mimi naona kuna tatizo kwa haya unayooyandika sio bure...
 
JF burudani tosha!
Hiyo CV unaombea kazi humu au? Halafu ulivyoungaunga sasa....
 
Jifunzeni Kutotoa Majina Ya Ajabu Kwa Watoto Eti "MASHAKA"
 
ACADEMICS&PROFESSIONALS.

Hii ndio Biograph ya Deogratius Kisandu.

Kuzaliwa: 28 Juni 1980. Siku ya Jumamosi.

1990-1994: Shule ya msingi Sunge, kata ya Busoka, Kahama, Shinyanga. Darasa la i-v.

1995-1996: Shule la msingi kahama, kahama, Shinyanga. Darasa la vi-vii.

1997: Kidato cha kwanza, Magu sekondari, Magu, Mwanza.(Evening Class-ODL).Niliishia Form one tu.

July 1998-April 1999: Mtawa shirika la Ndugu wadogo wa Afrika, Morogoro. Niliishia hatua ya Uaspiranti tu(Utakaji) hivyo sikutunukiwa cheti zaidi ya Kitambulisho.

April 1999-2002: Form i-iv, Kishimba sekondari, Kahama, Shinyanga.(Evening classes-ODL).

Desemba 2002-2003: ASTASHAHADA ya Uandishi wa habari, Chuo cha Royal College of Journalism, Dar es Salaàm.

2004: Mwandishi wa habari wa kujitegemea.

2007: Ku attend mtihani wa Kidato cha sita katika kituo cha kufanyia mtihani cha sekondari ya wasichana Tabora.(Cheti cha kidato cha sita)

April 2007-Juni 2007: Induction course for secondary school Teachers, Chuo cha ualimu Tabora(Leseni ya kufundishia 2007-2012).

2007-2012: Mwalimu, Shule ya sekondari Mwamala, Nzega, Tabora.

2008: Kurudia mtihani wa kidato cha sita (resitter), Kahama sekondari.

2008: Msimamizi Mkuu, mtihani kidato cha Pili, Mogwa sekondari, Nzenga.

April 2009: Msahihishaji wa Mitihani ya Mock kidato cha NNE, kanda ya Magharibi, Tabora.(Somo la kiswahili).

2009-2012: Shahada ya Elimu Maalum(Ndani yake nimesoma Political Science and Public Administration), Chuo Kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira cha Sebastian Kolowa(SEKUCo), kwasasa SEKOMU.

2013 up to date: Mwalimu, Shule ya sekondari Mkolani, Mwanza.

2013: Mafunzo maalum ya Gesi asilia na madini, Mwanza, TEITI.

2014: Muwezeshaji Kongamano la KATIBA Mpya, Mwanza.

April 2014: Mafunzo maalum ya mahusiano ya Ndoa na Uchumba, JRC, Mwanza.

2016: Semina ya kusimamia mtihani na kusahisha kidato cha sita, Mwanza.

2016: Msimamizi wa mitihani kidato cha sita, Ngaza sekondari, Mwanza.

2016: Mafunzo maalum ya Imani Takatifu ndani ya Kanisa Katoliki(KATEKESI), Mwanza.

2012-2016: Nimeshiriki semina zote za JUKWAA LA KATIBA kupitia taasisi yetu ya JUKWAA la Mwalimu na Wanafunzi Tanzania (Teachers and Students Forum Tanzania).

Niliposahau nitaleta mwendelezo,

Wenu wa karibu:

Deogratius Nalimi Kisandu.
Ifungulie uzi na hii km bado
 
Utata kidogo 1995-2002 ulikua mwenyekiti wa VIRAFRA Kahama sasa iweje tena uwe mwanafunzi wa utawa huko Morogoro.
Pia hongera kwakuwa sasa ni Katekista
 
picha ya awali na hiyo ya sasa "avatar" inasoma haupo na 'amani' Bwn Kisandu!

kwa cv yako anzisha kanisa; siasa huna pumzi kabisa...
 
hahahahaha
2014-up to dàte: Muimbaji wa Nyimbo za Injili.( kipindi cha nyuma miaka ya 2004 niliwahi kufanya mziki wa Bongofleva na kutoa album kwa jina la MASQO na iliitwa "Usiunyanyapae moyo wangu"
 
Utata kidogo 1995-2002 ulikua mwenyekiti wa VIRAFRA Kahama sasa iweje tena uwe mwanafunzi wa utawa huko Morogoro.
Pia hongera kwakuwa sasa ni Katekista


Niliondoka kwa takribani miezi 10 kwenda utawani na nilipo rudi niliendelea na cheo changu (July 1998-april 1999). Naimani umenipata.
 
picha ya awali na hiyo ya sasa "avatar" inasoma haupo na 'amani' Bwn Kisandu!

kwa cv yako anzisha kanisa; siasa huna pumzi kabisa...


Mikono hiyo ndio alama ya chama itakavyo kuwa.
 
Sasa wewe kisandu umezaliwa 1980 afu unasema ulitangaza nia ya kugombea uraisi 2015? Si bure kisandu anahitaji counselling
 
Mkuu Utakuwa una Mental Disorder jaribu kupata ushauri wa kitaalamu, ni tatizo huwa linatokea Maishani...ukiliacha bila kulishuhulikia utajikuta Unaokota Makopo
 
Msaada au mi ndio sielewi lugha ya Malkia.
Mi nadhani inatakiwa kusomeka ....Religious Leadership CV ya .....
 
Biograph fupi ya Deogratius Kisandu.

Kuzaliwa: 28 Juni 1980. Nakuitwa jina "MASHAKA" hospitali ya wilaya ya kahama, shinyanga.

Kubatizwa: 28 Juni 1992.
Nakuitwa jina "DEOGRATIUS"
Parokia ya kahama mjini.

Komunio ya kwanza: 28 Juni 1992.
Parokia ya kahama mjini.

Kipaimara: 06 Novemba 1994 na Mhashamu hayati Askofu Matheo Shija.
Parokia ya kahama mjini.

UTUMIKIZI WA MISA KANISANI: 1995- November 2002: Jimbo katoliki la Kahama.

1995-2002: Mwenyekiti wa Vijana Rafiki WA Yesu WA Mtakatifu Fransisko WA Asizi(VIRAFRA) Jimbo katoliki la kahama.

July 1998-April 1999: Mwanafunzi wa Utawa wa shirika la Ndugu wadogo wa Afrika, Morogoro.

1999-2002: Mwanachama wa TYCS jimbo katoliki la kahama.

1992-2002: Nimeshiriki semina nyingi sana za dini na makongamano mengi sana ya kidini.

2014-up to dàte: Muimbaji wa Nyimbo za Injili.( kipindi cha nyuma miaka ya 2004 niliwahi kufanya mziki wa Bongofleva na kutoa album kwa jina la MASQO na iliitwa "Usiunyanyapae moyo wangu"

2015-2017: Mshiriki wa mafunzo ya Dini na mwanajumuia za KATEKESI jimbo katoliki la Mwanza.

Nawasilisha,

Deogratius Nalimi Kisandu.
Umesahau- kipengele cha kuhama ukatoliki kwa kujiapiza
 
Back
Top Bottom