Rekebisheni haya ndio nitachangia harusi

Rekebisheni haya ndio nitachangia harusi

Nimebahatika kuwa kwenye kamati mbalimbali za harusi,sendoff na sherehe nyingine tofauti ambazo huitisha kamati..

Yanayofanyika kwenye hizi kamati kwa kweli ni biashara na kuonana wengine ni mazuzu.

Wengi wa wanakamati huja kwa lengo la kufanya biashara na si kusaidia sherehe kufanyika,utasikia chakula mpeni fulani,picha mpeni huyu mara mtu wa mapambo mimi namfahamu bei yake ni ndogo kumbe kuna percent wanapiga.

Kilichonikera hadi kuanzisha uzi huu ni juzi nilikuwa send off ya binti mmoja tumefahamiana na mchango ulikuwa ni laki moja huwezi amini aliyepewa tender ya vinywaji katunywesha vibia vidogo(nyonga ndogo) vi4... kwa akili ya kawaida tu bia ndogo 4*1500!=6000
Kweli hii ni halali??kuja kuuliza alipewa tender anaundugu na bi harusi mtarajiwa nikachoka kabisa.

Ukiachana na hilo mc wa sherehe mnaharibu sherehe za watu sio kila mtu anakuwa na hela za kutoa hapo mbele,mnakamua sana watu na kuaibishana kipuuzi ohh braza wenye tai toa elfu 10..ulinipa???

Mwisho namaliza hivi mnaopanga kunishirikisha kwenye sherehe zenu rekebisheni hizo kero mie ntachangia sababu mie pia ni mwana jamii mwenzenu.

Asanteni.
Hivi ma MC nao huwa wanapewa percent fulani kwenye zile pesa wanazotukamua?
 
Nchi ya mazuzu inaishi kizuzu zuzu. Ama kweli ujinga ni mama wa mahangaiko yote! The whole thing of ''vikao vya harusi na kamati zake'', ''michango ya harusi na matumizi yake'' ni ujinga wa kiwango cha juu. sijui ni lini utaondolewa hapa nchini. Halafu mnalia eti vyuma vimekaza? Siyo kweli.
 
Mimi nilikuwa naona kama hadithi tu hizi mpaka nilipoalikwa siku moja kwenye kikao tena ya kujitakia
Kwa kweli nilishangaa sana jinsi watu wanavyopangiwa kutoa hela

Tupo tofauti kwa kweli
Nilioa bila mchango wowote na ilifana sana watu walialikwa tu na Kula na kisomo na kuagana
Acheni kulalamika ni mambo mliotengeneza wenyewe
 
Mie nilishaachaga kuchangia michango kama ya harusi, sends off, kipaimara, birthday, mahafali na vitu vingine kama hivyo zamani sana. Ujinga mtupu huko
Kwa sababu ww ulichangiwa
 
Nyie mnawaza kula na kunywa tuu,gharama za ukumbi,MC/Music,Mapambo na zawadi kwa wanaharusi hamzioni?
Hizo zinatakiwa ziwe gharama zao na wanafamilia. Miw yananihusu nini hayo!!!
Mie naenda kula na kunywa na kufurahi baaaasi.
 
Afadhali hata wewe unakunywa bia kidogo unafaidi,sasa sie wanywa soda tunaishia kunywa chupa 1.tu ya 500.maana hatuwezi kunywa soda 2 at once! Na hela tumetoa sawa sawa!
Angalau mie mnywa maji naagiza kama chupa 4 zile ndogo nakaa napiga taratibu.
 
Na sasa hivi kuna hii tabia mbaya sijui imetoka wapi!!! Mtu yupo mikoa ya mbaaali huko eti anawekwa kwenye kamati ilimradi tu apigwe vilaki. Shenzi type tutanuniana sana.
 
Pole Sana mkuu... Mimi nilisha acha kitambo kuchangia hayo mambo yasio namaana wallah......
Mtu akitaka kufunga ndoa, anapaswa ajiandae yeye mwenyewe kwasababu, ndoa sio Jambo la ghafla. Sasa yanapo kuja mambo ya kulazimisha michangi nisawa na muoaji/muolewaji kubebesha mzigo wake kwa watu wengine.
 
Niliwahi kuchangia harusi moja hadi nikapatwa hasira ila baadae bibi harusi alikuja kuzilipa pesa zangu kwa kunipa Nyapu yake.
 
Mtalaumiana bure tu. Ukishaamua kumchangia mtu basi changa, usitegemee kulewa siku ya sherehe au kula unavyotala. Kwanza mstaarabu anaweza kuchaga kiasi kikibwa cha pesa halafu siku ya sherehe wala asihudhurie. Kama unataka kufaidi pesa yako kaitumie mwenyewe binafsi. kama una kinyongo na sherehe basi acha tu kunchangia, ili kuepusha lawama.
 
Ninachukia sana hii michango ya harusi,

Haina maana kabisa hata kidogo,

Wengi wamefanya kama sehemu ya kutafutia mitaji,

Ni upuuzi wa hali ya juu kabisa

Nilishaacha kuchanga haya mambo.
 
Mimi sichangii kabisa hizo sherehe. Misiba, ugonjwa na natural calamities nitachangia. Sherehe yako sichangii na siji. Sitachangisha watu pia.
 
Mchango wangu hauzidi 30,000 hata usiponipa kadi nafurahi zaidi maana utaambiwa ukumbi ni mbezi beach,kutoka chanika mpaka mbezi beach usafiri sio chini ya 30,000 halafu unakula kipapatio na pepsi moja tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom