kidaganda
JF-Expert Member
- Aug 26, 2013
- 2,999
- 2,582
Nimebahatika kuwa kwenye kamati mbalimbali za harusi,sendoff na sherehe nyingine tofauti ambazo huitisha kamati..
Yanayofanyika kwenye hizi kamati kwa kweli ni biashara na kuonana wengine ni mazuzu.
Wengi wa wanakamati huja kwa lengo la kufanya biashara na si kusaidia sherehe kufanyika,utasikia chakula mpeni fulani,picha mpeni huyu mara mtu wa mapambo mimi namfahamu bei yake ni ndogo kumbe kuna percent wanapiga.
Kilichonikera hadi kuanzisha uzi huu ni juzi nilikuwa send off ya binti mmoja tumefahamiana na mchango ulikuwa ni laki moja huwezi amini aliyepewa tender ya vinywaji katunywesha vibia vidogo(nyonga ndogo) vi4... kwa akili ya kawaida tu bia ndogo 4*1500!=6000
Kweli hii ni halali??kuja kuuliza alipewa tender anaundugu na bi harusi mtarajiwa nikachoka kabisa.
Ukiachana na hilo mc wa sherehe mnaharibu sherehe za watu sio kila mtu anakuwa na hela za kutoa hapo mbele,mnakamua sana watu na kuaibishana kipuuzi ohh braza wenye tai toa elfu 10..ulinipa???
Mwisho namaliza hivi mnaopanga kunishirikisha kwenye sherehe zenu rekebisheni hizo kero mie ntachangia sababu mie pia ni mwana jamii mwenzenu.
Asanteni.