Rekebisheni haya ndio nitachangia harusi

Rekebisheni haya ndio nitachangia harusi

Mleta mada wewe sio mchangaji, kwanza michango ni hiari sasa malalamiko ya nn huku JF.!!
Sherehe bajet yake 28M wewe umetoa elf 70 ndio unakuja kufungua uzi..!?.
Hahahaaa hatari sana
 
Niliwahi kuchangia harusi moja hadi nikapatwa hasira ila baadae bibi harusi alikuja kuzilipa pesa zangu kwa kunipa Nyapu yake.
We Sio mtu mzuri kwenye jamii ya watu wastaarabu. [emoji35]
 
Nimebahatika kuwa kwenye kamati mbalimbali za harusi,sendoff na sherehe nyingine tofauti ambazo huitisha kamati..

Yanayofanyika kwenye hizi kamati kwa kweli ni biashara na kuonana wengine ni mazuzu.

Wengi wa wanakamati huja kwa lengo la kufanya biashara na si kusaidia sherehe kufanyika,utasikia chakula mpeni fulani,picha mpeni huyu mara mtu wa mapambo mimi namfahamu bei yake ni ndogo kumbe kuna percent wanapiga.

Kilichonikera hadi kuanzisha uzi huu ni juzi nilikuwa send off ya binti mmoja tumefahamiana na mchango ulikuwa ni laki moja huwezi amini aliyepewa tender ya vinywaji katunywesha vibia vidogo(nyonga ndogo) vi4... kwa akili ya kawaida tu bia ndogo 4*1500!=6000
Kweli hii ni halali??kuja kuuliza alipewa tender anaundugu na bi harusi mtarajiwa nikachoka kabisa.

Ukiachana na hilo mc wa sherehe mnaharibu sherehe za watu sio kila mtu anakuwa na hela za kutoa hapo mbele,mnakamua sana watu na kuaibishana kipuuzi ohh braza wenye tai toa elfu 10..ulinipa???

Mwisho namaliza hivi mnaopanga kunishirikisha kwenye sherehe zenu rekebisheni hizo kero mie ntachangia sababu mie pia ni mwana jamii mwenzenu.

Asanteni.
Good observation, Mimi baada ya uchunguzi wangu niligundua huu uhuni katika harusi nyingi nikaamua kufanya kama ifuatavyo;
Mosi mi ndo nilikuwa namiliki line kwa ajili ya wachangiaji na kukusanya cash yaani mhasibu alikuwa mfuatiliaji tu.
Pili nilifanya negotiations zote katika kila sekta Mimi mwenyewe.
Tatu,kamati ya ufuatiliaji ilitengenezwa wiki mbili kabla ya shughuli kwa ajili ya kuratibu na kufuatilia tu kwani sekta zote kesho nilitoa Mimi mwenyewe.
Siku ya tukio kila kitu kilienda safi na watu walikunywa na kusaza na fedha kidogo ilibaki. Kwa hiyo katika mambo haya inahitaji ujiongeze vinginevyo shughuli yako itageuzwa dili na utavunja mahusiano mazuri na jamii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom