REINCARNATION maybe is real

REINCARNATION maybe is real

VERIFY

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2024
Posts
1,092
Reaction score
2,589

REINCARNATION IS REAL​


Reincarnation wazo kwamba consciousness au utambulisho wa mtu unaweza kuendelea baada ya kifo na kuonekana katika maisha mengine imejadiliwa kwa maelfu ya miaka. Lakini kinachovutia zaidi ni kwamba kuna kesi zilizochunguzwa na watafiti, si hadithi za kawaida tu. Division of Perceptual Studies ya University of Virginia imekusanya zaidi ya kesi 2,500 za watoto wanaodai kukumbuka maisha yaliyopita. Watoto wengi huanza kutoa maelezo wakiwa na miaka 2–5, mara nyingi bila kuambiwa kwamba wanapaswa kuamini reincarnation. Baadhi hutaja majina, maeneo, familia na mazingira ya kifo ambayo baadaye watafiti hujaribu kuyathibitisha.


Case ya James Leininger ni mojawapo ya zinazovutia zaidi. Akiwa mtoto mdogo, James alianza kuwa na nightmares kuhusu ndege ya kivita ikianguka na kutoa taarifa zilizohusishwa na rubani wa Marekani aliyekufa katika Vita vya Pili vya Dunia. Utafiti wa psychiatrist Jim Tucker wa University of Virginia ulipitia documentation ya statements na behaviors za James, ikiwemo taarifa zilizorekodiwa kabla ya rubani aliyedaiwa kuwa “previous personality” kutambuliwa. Tucker alihitimisha kwamba kulikuwa na similarity kubwa kati ya taarifa za mtoto na maisha/kifo cha James M. Huston Jr., ingawa case ina limitations hasa kwa sababu baba wa James ndiye aliyesaidia kumtafuta mtu aliyelingana na taarifa hizo.


Ushahidi mwingine wa kushangaza ni birthmarks na birth defects. Katika utafiti wa Ian Stevenson, baadhi ya watoto waliodai kukumbuka maisha yaliyopita walikuwa na alama au kasoro za kuzaliwa zilizodaiwa kuendana na majeraha ya mtu aliyekufa. Database ya UVA inasema takribani 30% ya cases zao zina birthmark au birth defect. Stevenson pia alichapisha cases ambazo alijaribu kulinganisha alama hizo na medical records, autopsy reports, police reports au ushahidi wa mashahidi. Kuna hata case iliyochapishwa kuhusu birthmarks zenye pattern kama nyuzi za kamba zilizolinganishwa na majeraha ya kamba kwa mtu aliyekufa.


Sasa swali kubwa linabaki: kama reincarnation si kweli, tunazielezaje cases hizi? Inawezekana baadhi zinaelezwa na coincidence, taarifa zilizopatikana bila kujua, influence ya wazazi, memory distortion au confirmation bias. Hiyo ndiyo sababu sayansi bado haijasema “reincarnation imethibitishwa.” Lakini pia si rahisi kuzipuuza zote kama fantasies, kwa sababu baadhi zina documentation na taarifa zinazoweza kuchunguzwa. Kwa hiyo, msimamo wangu si kwamba hizi cases ni proof ya mwisho, bali ni ushahidi unaofanya swali la reincarnation liwe zito zaidi kuliko watu wengi wanavyodhani: Je, consciousness inaweza kuendelea baada ya kifo, na kama ndiyo inawezaje kubeba taarifa kutoka maisha moja kwenda nyingine?

Poker
 
What’s your angle on this?
Nimesoma reincarnation, nimesoma Hinduism, nimesoma Buddhism, nimefanya meditation Buddhist Temple and Meditation Center Dar es salaam chini ya Rev. Pannasekara. Mshana Jr anamjua.

Nimesoma vitabu vikubwa vya Hinduism na Buddhism takriban vyote.

Bado kidogo tu niwe an ordained Buddhist monk.

Hiyo ni zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Reincarnation ni dhana ya kifalsafa na kidini tu kwenye uhalisia ukifa material yako yanakiwa recucled wanaibuka viumbe wengine.

Na hakuna soul, hiyo ni story tu.
 
Ninesoma reincarnation, nimesoma Hinduism, nimesoma Buddhism, nimefanya meditation Buddhist Temple and Meditation Venter Dar es salaam chini ya Rev. Pannasekara. Mshana Jr anamjua.

Hiyo ni zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Nimesoma vitabu vikubwa vya Hinduism na Buddhism takriban vyote.

Reincarnation ni dhana ya kifalsafa na kidini tu kwenye uhalisia ukifa material yako yanakiwa recucled wanaibuka viumbe wengine.

Na hakuna soul, hiyo ni story tu.
Got you, but I go deep material yanakua recycled and rotten, tukienda upande wa souls imekaaje ? Or you just perish forever
 
There is no soul. That is just an idea, a philosophical and religious narrative to propose and advocate for a nonexistent continuity.

Hata kwenye Buddhism hakuna a permanent soul.
Kama unaamini kwamba roho au soul haipo na kila kitu tunachokiita ‘mimi’ kinatokana na ubongo na mwili tu, basi ni nini hasa kinachoendelea ndani yetu kinachotufanya tuwe na consciousness, hisia, kumbukumbu, maamuzi na ile hali ya kujitambua kwamba ‘mimi ni mimi’ na ubongo ukifa, ni nini hasa kinachofanya huyo ‘mimi’ aache kabisa kuwepo ?
 
Nimesoma reincarnation, nimesoma Hinduism, nimesoma Buddhism, nimefanya meditation Buddhist Temple and Meditation Center Dar es salaam chini ya Rev. Pannasekara. Mshana Jr anamjua.

Nimesoma vitabu vikubwa vya Hinduism na Buddhism takriban vyote.

Bado kidogo tu niwe an ordained Buddhist monk.

Hiyo ni zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Reincarnation ni dhana ya kifalsafa na kidini tu kwenye uhalisia ukifa material yako yanakiwa recucled wanaibuka viumbe wengine.

Na hakuna soul, hiyo ni story tu.
Kaka umejibu dhana yangu kwa uhakika mkubwa sana, atakae bisha anaweza thibitisha mwenyewe
 
Back
Top Bottom