REINCARNATION IS REAL
Reincarnation wazo kwamba consciousness au utambulisho wa mtu unaweza kuendelea baada ya kifo na kuonekana katika maisha mengine imejadiliwa kwa maelfu ya miaka. Lakini kinachovutia zaidi ni kwamba kuna
kesi zilizochunguzwa na watafiti, si hadithi za kawaida tu. Division of Perceptual Studies ya University of Virginia imekusanya zaidi ya
kesi 2,500 za watoto wanaodai kukumbuka maisha yaliyopita. Watoto wengi huanza kutoa maelezo wakiwa na miaka 2–5, mara nyingi bila kuambiwa kwamba wanapaswa kuamini reincarnation. Baadhi hutaja majina, maeneo, familia na mazingira ya kifo ambayo baadaye watafiti hujaribu kuyathibitisha.
Case ya James Leininger ni mojawapo ya zinazovutia zaidi. Akiwa mtoto mdogo, James alianza kuwa na nightmares kuhusu ndege ya kivita ikianguka na kutoa taarifa zilizohusishwa na rubani wa Marekani aliyekufa katika Vita vya Pili vya Dunia. Utafiti wa psychiatrist Jim Tucker wa University of Virginia ulipitia documentation ya statements na behaviors za James, ikiwemo taarifa zilizorekodiwa kabla ya rubani aliyedaiwa kuwa “previous personality” kutambuliwa. Tucker alihitimisha kwamba kulikuwa na
similarity kubwa kati ya taarifa za mtoto na maisha/kifo cha James M. Huston Jr., ingawa case ina limitations hasa kwa sababu baba wa James ndiye aliyesaidia kumtafuta mtu aliyelingana na taarifa hizo.
Ushahidi mwingine wa kushangaza ni
birthmarks na birth defects. Katika utafiti wa Ian Stevenson, baadhi ya watoto waliodai kukumbuka maisha yaliyopita walikuwa na alama au kasoro za kuzaliwa zilizodaiwa kuendana na majeraha ya mtu aliyekufa. Database ya UVA inasema takribani
30% ya cases zao zina birthmark au birth defect. Stevenson pia alichapisha cases ambazo alijaribu kulinganisha alama hizo na medical records, autopsy reports, police reports au ushahidi wa mashahidi. Kuna hata case iliyochapishwa kuhusu birthmarks zenye pattern kama nyuzi za kamba zilizolinganishwa na majeraha ya kamba kwa mtu aliyekufa.
Sasa swali kubwa linabaki:
kama reincarnation si kweli, tunazielezaje cases hizi? Inawezekana baadhi zinaelezwa na coincidence, taarifa zilizopatikana bila kujua, influence ya wazazi, memory distortion au confirmation bias. Hiyo ndiyo sababu sayansi bado haijasema
“reincarnation imethibitishwa.” Lakini pia si rahisi kuzipuuza zote kama fantasies, kwa sababu baadhi zina documentation na taarifa zinazoweza kuchunguzwa. Kwa hiyo, msimamo wangu si kwamba hizi cases ni
proof ya mwisho, bali ni ushahidi unaofanya swali la reincarnation liwe zito zaidi kuliko watu wengi wanavyodhani:
Je, consciousness inaweza kuendelea baada ya kifo, na kama ndiyo inawezaje kubeba taarifa kutoka maisha moja kwenda nyingine?
Poker