Reginald Mengi on Nape: Muache Mungu afanye Kazi Yake

Reginald Mengi on Nape: Muache Mungu afanye Kazi Yake

Astakafulai Nape Nnauye! Waheshimu wazee ndugu yangu. Kwani sisi vijana hatutakufa? Au na sisi hatutakuwa wazee! Na kama ni kweli ni maoni ya Wazee kwani hawana haki ya kutoa maoni? Au ni mwendelezo wa siasa za kibaguzi kwa misingi ya umri!
 
Aliwambia anajiandaa kuja na hoja za maendeleo, duh! kwelI tunaona umekuja.
 
Huyo Nape anakurupukaga kama katoka kwenye friji....
Yeye aonyeshe mkataba wake wakuishi hapa duniani alioandikiana na aliyemuumba.
 
Mmeanza kuwekea watu maneno mdomoni make hamchelewi kusema fulani kasema hivi kumbe umepika tory,
1+1=2 na siyo vinginevyo serikali tatu ndiyo mnyama gani watuondolee uchuro huo.

kama hujui kaa kimya. Hapa nchi hazikujumlishwa ziliunganishwa. Unadhani tz ya sasa ni ya Nyerere. Kama ni serikali mbili elezeni za wapi na wapi! Naona mnahaha.
 
Huyu jamaa nafikiri ni miongoni mwa watu ambao wamepewa nafasi katika chama bila kumfanyia screening maana siku zote huongea maneno yenye makapi
 
me hata cshangai....nape,mwiguru na pinda wote ni vilaza.....viwatokavyo midomoni mwao ni Up.u.pu mtupu
 
Nafurahi mnavyojitekenya wenyewe na mkicheka wenyewe ha ha ha ha ha mengi bana yani kubambikizwa twins wale tayari anaweza kupambana na vijana we mzee kwishne kabisaa
 
Ndugu Nape ni kweli wazee wetu wmasubiri kufa kama na sisi tunavyyosubiri kufa kwani ajuaye utkufa lini ni mUngu pekee. Baadhi ya wazee waliomo kwenye tume ya katiba ni Joseph Sinde Waryoba, Joseph Butiku, Baregu na Salim. Kama kauli hii inawalenga hawa basi Nape kapotoka anatakiwa arudi kwenye mstari.
 
"Waliopendekeza Serikali tatu ni Wazee wanaosubiri kufa"-Nape.
 
Nape ni kichaa kwa kiwango chake....kwani kufa kunajali umri? Anaweza akafa yeye kwanza kabla ya wazee anodai kuwa wanakaribia kufa. Aache upinda
 
Haswa, akili ndogo ndo imekalia vyeo vikubwa, kazi tunayo TZ, hata Nape naeeee HAMNAZO
 
CCM kisipowatosa Nape na Mwigulu kitaambulia kaburi 2015.
Uwepo wao ni furaha kwa wapenda mabadiliko
Kauli zao ni sumu inayokiua chama taratibu..
Atakufa yeye kabla ya hao wazee wenye hekima.
 
Nafurahi mnavyojitekenya wenyewe na mkicheka wenyewe ha ha ha ha ha mengi bana yani kubambikizwa twins wale tayari anaweza kupambana na vijana we mzee kwishne kabisaa

Ndo matatizo hayo sasa......kwahiyo Mengi hana uhuru wakuongea kisa kabambikiziwa twins kama unavyosema ww.
 
Mzee Reginald Mengi ame tweet mawazo yake juu ya Kauli ya Nape Nnauye ambae inadaiwa kasema waliopendekeza Serikali tatu ni wazee wanaosubiri kufa.

View attachment 104489
---------------------------
Habari Kamili
---------------------------


NAPE: Waliopendekeza Serikali tatu ni Wazee wanaosubiri kufa​

MZIMU wa serikali tatu bado unaendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo jana, Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipinga tena uwepo wa serikali tatu na kudai kuwa waliotoa maoni hayo ni wazee wanaosubiri kufa. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili mchakato wa Katiba Mpya, katika ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye alisema nia ya serikali tatu ni kuleta matabaka ambayo yatasababisha migogoro.

“Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja Muungano enzi za ujana wao? Wamenufaika na Muungano kwa kipindi cha miaka 50, sisi vijana wanataka kutuachia mgogoro!”alisema Nnauye.

Nape alisema kuvunjwa kwa Muungano kutasababisha mgogoro mkubwa wa rasimu kutokana na muda ambao Muungano huo umedumu.

Alisema kuundwa kwa serikali tatu si sera ya CCM kama wanavyodai wapinzani, bali ni maoni ya watu waliyoyawasilisha katika ukusanywaji wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya.

“Sera ya CCM ni kuongoza serikali mbili na si tatu, na hii sera tutaendelea kuitetea na kuilinda mpaka mwisho wa dunia, tunachoamini katika chama chetu hatuogopi kutetea sera ambazo tumezitoa wenyewe,” alisema Nnauye.

Alisema ni vyema zikamalizwa kasoro zilipo katika mfumo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na si kuongeza madaraka yasiyo na tija.

Nape alisema kitendo cha Tume ya Jaji Joseph Warioba kusema imetumia sheria ya mwaka 1964 kuwa kigezo cha kuundwa kwa serikali tatu si sahihi, kutokana na makubaliano ya mwaka huo kwamba ni serikali mbili.

Kiongozi huyo wa CCM pia alishangazwa na kitendo cha Rasimu ya Katiba mpya kutamka wazi idadi ya mikoa pamoja na wilaya ambazo zitatumika katika uchaguzi na kwamba mwenye jukumu hilo ni Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

“Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa serikali tatu itaelea katika madaraka, kwani serikali ya Tanganyika itakuwa haiwezi kuwatetea wananchi, hali itakayosababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa urasimu ambao ni adui wa maendeleo,” alisema Nnauye.

Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa Muungano kutasababisha kuiburuza Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani asilimia 95 ya uchumi wa visiwani unategemea Tanzania Bara.

Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa kiongozi ni kuwatetea wananchi na si kuwazidishia mizigo.

Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Nnauye alisema CCM hakiogopi mgombea binafsi, kwani hata akigombea chama hakitapata hasara yoyote.

Nape alisema sera ya CCM ni kukataa wagombea binafsi wanaouza unga na si kukataa mgombea binafsi kama ambavyo vyama vingine vya siasa vinavyodai katika vyombo vya habari.

Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9 inazungumzia umri wa Mbunge kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa CCM suala hilo si sahihi, kwani wabunge wenye miaka 21 wanawajibika vizuri kuliko wazee.

Source: Mwananchi
Weka video yake hapa vinginevyo tupis
 
Back
Top Bottom