Regina wa kinondoni moroko

Regina wa kinondoni moroko

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,977
Reaction score
37,879
Mwaka 1993, bendi ya muziki wa Dansi ya VIJANA ORCHESTRA wana SAGA RHUMBA ikiongozwa na MUHINA PANDUKA a.k.a TOTO TUNDU, walitoa albamu yao ( sikumbuki jina la albamu), ila moja kati ya nyimbo kali zilizokuwemo ndani ya albamu hiyo ni pamoja na huu " UZURI WA REGINA " .

Baadhi ya mashairi ya wimbo huo ni :

Hapa ulimwenguni kila binadamu, Mungu kamuumba na sifa zakee, yoyo yoyo yooo x 2.

Lakini uzuri wa Regina unaweza kukufuru Mungu, kwa kusema kapendelewa, kapendelewa eeeh x 2.

Msichana huyu ni mkazi wa jiji la Darisalamu, ukitaka kumuona nenda Kinondoni Morocco Road x 2.

Wakaazi wa mtaa huu, bila kujali jinsia, wakamwita top queen!

A top queen of Moroko Road x 2.

Ntambuika wee imebaki kwetu wavulana, wenyewe kwa wenyewe tumebaki tunaulizana tunagombana x2.

Wengine wameenda na magari ya kukodi, na suruali za kuazima, lakini regina anawakataa

Lakini kijana mmoja msukuma mikokoteni wa Ilala, amefunga ndoa na regina, tumebaki tunaulizana, tunashangaa !

Nilikuwa darasa la pili wakati wimbo huu unatoka, but i was oolder enough to know who is beautiful woman and who is not. Nilikuwa natamani sana kwenda Kinondoni Moroko kumuona huyo Regina kwa sababu nilikuwa naamini nikifika tu Moroko ntamkuta Regina hapo( akili za kitoto ), but sikuweza coz by that time tulikuwa tunaishi Tabata....

Mpaka leo hii, bado sijajua kama kisa cha Regina kilikuwa ni cha ukweli ama kilikuwa cha kubuni tu, kama ni cha ukweli basi kumbe wakati mwingine pesa haiwezi kuwa jawabu la kumpata mwanamke.

Kama kuna yoyote nafahamu kuhusu wimbo huu na kisa chake, anaweza kushare nasi hapa. Jumapili njema wakuu.
 
Umenikunbusha gelofurendi wangu wa jeshini alikuwa anaitwa Regina, kimahabati nilikuwa namwite Reggy.
 
utunzi wa Marehemu Jerry Nashon 'Dudumizi" , mtaalamu wa nyimbo za Mapenzi ukiwemo VIP
 
Hebu funguka kaka, kisa cha Regina kilikuwa halisi au fiction?
 
Kama kuna mwenye hilo song tunaomba upload hapa tujikumbushe tunzi za ukweli za wakati huo. Nahisi ilikuwa ni kisa cha kubuni tu.
 
Naye gelufrendi wako alikuwa mjeda, binti wa mjeda au beki 3 wa mjeda?

Back
Top Bottom