Regia Mtema 'anaishi' Morogoro,Pwani bado yetu

Regia Mtema 'anaishi' Morogoro,Pwani bado yetu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Regia Mtema bado anaishi kifikra katika siasa za Morogoro. Pamoja na ulemavu aliokuwa nao, Regia anatajwa Morogoro nzima kama mpambanaji, mjenzi wa hoja na demokrasia na mpinzani wa kweli. Regia Mtema ni kinara wa mabadiliko ya kidemokrasia Morogoro.

Ameacha mizizi. Kuanzia Kilosa hadi Ulanga zote; Morogoro Mjini na majimbo mengineyo,Regia ameacha mbegu za upinzani. Ana wafuasi sasa watunyimao usingizi Morogoro.

Kuhusu Pwani, yatosha kusema bado yetu. Pwani wanatupenda,nasi twawapenda. Hakuna matata Pwani.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
R.I.P kamanda mpambanaji Regia Mtema

Wanakufa Wapamvanaji duniani wanabaki wasaliti kama kina nyepesi na kundi lake, Ingekuwa ni amri ya umma wangetamgulia kwanza hao na maccm yote yasiyojitambua

BACK TANGANYIKA
 
Asante kwa kutushtua sasa tunaenda kuweka kambi Pwani,japo nina shaka na hawa watu hawaelimiki sawa na mkubwa wao
 
Mzee Tupatupa naomba maoni na tathimini yako kuhusu sakata la ESCROW, Vipi ile kauli ya kuwadhibiti wanaojitangazia kugombea kiti kikuu cha Magogoni kimeishia wapi? Eti ni kweli jana meli ziliwausha wasikilizaji kwenda Kisiwani kuongeza idadi ya watu kwenye mkutano wa Kibandamaiti?

Tathimini zako na ripoti zako za mikoani nazikubali tungekuwa na watu kama mzee Tupatupa hakika nchi ingekwenda mbele,

Chikaka wa Sumuni
 
Pwani inahitaji mabadiliko ya kifikra na maono,bila kuitikisa serikali ya CCM kwa kuinyima kura tutabaki kuonekana shamba la bibi la CCM,na hivyo kutofanya lolote la msingii kimaendeleo.Mtwara na Lindi washajikomboa kutoka katika fikra mgando ni wakati wetu nasi wanapwani tujiondoe huko ili angalau serikali na ituthamin hasa hii pwani ya Rufiji ndo hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom