Regency Hospital jirekebisheni tafadhali, mtatuua

Regency Hospital jirekebisheni tafadhali, mtatuua

BABA E's

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
354
Reaction score
136
Mnaeza mkawa mmezidiwa sana na idadi ya wagonjwa, lakini isiwe sababu ya kutokea kwa uzembe wa hatari ambao unaweza ukahatarisha maisha ya watu. Kumekuwa na mchezo wa siku nyingi kwenye maabara yenu wa kuchanganya majibu ya watu. Inaumiza na kuuzi sana kuambiwa hauumwi kisha kujiondokea zako kumbe ugonjwa upo na unaendelea kukutafuna zaidi mpaka hali inakuwa mbaya sana kisa umepewa majibu ambayo siyo ya kwako.

Natumaini kupitia mtandao huu ujumbe utafika.

Jirekebisheni Tafadhali.
 
Uzembe wa hali ya juu.

Msicheze na maisha/afya za watu.

Sie waTanzania kila kitu ni mzaha
 
Hapo unaweza kwenda kupima u.t.i halafu ukakuta kuna mwana mama kaenda kupima ujauzito kidume unapewa jibu lako una mimba na binti anaambiwa mkojo mchafu.
 
Regency ni wazembeeeeeeeee kinoumaaaaaaaa.............. Mimi nilienda kuchek mkojo.....wakachukua mkojo wakaniambia maabara yao ipo kinodoniiiiii.,.........so wakaniambia niendeee baada ya siku moja........na nahisi majibu waliyonipa hayakuwa ni sahihi maana tatizo nimekujaligundua tena...........wale waarabu wanapenda hela tuuu huduma mbovu mara mia
 
Wahindi bana
 
Hapa natatizika kidogo..! Regency ni hospitali au ni Maabara? Nijuavyo watu huenda hospitali kumwona Daktari akajieleza Dr akaamua apime nini? Inakuaje mtu anakwenda hospitali kupima mkojo? Hayo majibu yanapelelwa wapi?
 
Kazi ya maabara iko outsource kwa Lancet laboratory ?
 
wabaguzi kinoma,yan pale n waindi tuu ndo wanapata huduma nzuri .ukienda maabara ndo hovyoo masaa kibao unasubr majibu.
 
Mimi hao walinibambikiza haswa hiyo maabara yao ya Lancert. Mzee anatakiwa kufanyiwa operation 12 asubuhi mimi nikaja jana yake kutoa damu wakapima damu ,baadae wananiambia nipime damu kwa ajili ya ngoma tena kwa njia ya rhesus na inatakiwa damu ikae masaa 24 ndio ipimwe ngoma.Nikawaomba hao technicians wanisaidie damu blood bank maana mimi hiyo mpaka masaa 24 itapitiliza ratiba ya dokta aliyetupangia, aliyekuja kuelewana na mimi ni mkenya ile mitanzania hata haikunielewa japo na damu niliwaachia na elfu 80 juu kwa kipimo cha ngoma.
 
Hapo unaweza kwenda kupima u.t.i halafu ukakuta kuna mwana mama kaenda kupima ujauzito kidume unapewa jibu lako una mimba na binti anaambiwa mkojo mchafu.

na hapo kwenye vipimo vya mkojo ndio matatizo zaidi.
 
Hahahaha hatari....ila ts worse

Kuna wakati unaweza kuambiwa kabisa samahani tumepoteza sample yako tuletee nyingine, Sasa sijui huwa zinapotea vipi huko ndani. Kwa kweli inabidi wajirekebishe mapema kabla madhara makubwa kutokea sababu hatutawasamehe, huo utakuwa ni uzembe.
 
Back
Top Bottom