Redio ya Upendo, nimewashangaa kwa hili

Redio ya Upendo, nimewashangaa kwa hili

Usoka.one

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2013
Posts
770
Reaction score
374
Leo nikiwa kwenye chombo cha usafiri nimesikia mtu anahubiri hasomi neno anaongea tu suala la msamaha jambo ambalo ni jema lakini kilichonishangaza ni huyu mtu kuwa mgumu sana kutaja jina la yesu.

Na mafundisho yake yameonesha kumtaja Mungu mfalme wa wafalme lakini Yesu na roho mtakatifu naona limekuwa gumu mno!!na akitaja anataja kiaina hebu mwenye ufahamu atujuze na sie tusio na dini tuelewe.

Ni kipindi cha saa sita hadi saa saba leo Jumatatu.

Naomba tuelimishane sina nia mbaya.
 
Unamlazimisha mtu aamini unachoamini wewe ? Ndio maana kuna uhuru wa kuabudu
 
Toka mwanzo Injili ilishatiwa maji,toka vitabu 12 mpaka vinne,kwa hiyo ile dhambi ya mauzauza bado ina endelea.
 
Ukiona hivyo huyo anayehubiriwa siyo Mungu Yehova, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Hata mimi huwa nashangaa sana mahubiri ya namna hiyo. Siku fulani niliabudu kanisa fulani, mchungaji aliyehubiri hakutaja jina Yesu Kristo hata mara moja kwa muda wote (almost 2 hours) aliosimama madhabahuni kuhubiri. Hakukemea dhambi wala kutaja neno dhambi. Hakika wana wa Mungu tumevamiwa, tuwe macho hizi ni nyakati za mwisho!
 
Umeona nimelazimisha rafiki?au umekurupuka tu!!tena huyo mtu mtangazaji anamuita mwalimu.Jamani anayeelewa naomba anisaidie ninahisi lile jambo lililosisitizwa kuna majasusi kanisani laweza kuwa kweli.
 
Toka mwanzo Injili ilishatiwa maji,toka vitabu 12 mpaka vinne,kwa hiyo ile dhambi ya mauzauza bado ina endelea.

Unamaanisha Apocripha Gospels...?Mkuu kwanza siyo injili 12 bali ni 24...injili zilikuwa 24 ila zilizpchaguliwa katika Mtaguso wa effeso zilikuwa ni 4...Sababu za kuchaguliwa kwa injili hizo zipo wazi na kwann zingine ziachwe zipo wazi..

Na pia sio injili tuu bali kuna vitabu kedekede vilipigwa teke na Kanisa....Vitabu vya Ufunuo vilikuwa vingi tuu ila vyote vilipigwa teke na Ufunuo wa Yohana ukapata nafasi...Pia kunasababuzake za kitheologia na kihistoria..
pia kulikuwa na barua ya Tatu ta Mt Paulo kwa Wakorinto...Pia ilipigwa teke na kuwekwa kapuni...Ila vyote hivo vitabu vipo maktab ya Vatican..

sababu ya moja kwa moja ilikuwa vitabu hivyo vilijaa uzushi mwingi na vilikosa Theological connection na maisha ya kristo
 
Sasa ninyi mnachanganya mada. Je huyo mhubiri alikuwa ana-cite maandiko yoyote? Au alikuwa akirejelea usuri wa anachofundisha? Huwezi fundisha msamaha bila kumtaja Yesu. Vingine ni ushenzi mtupu!
 
Leo nikiwa kwenye chombo cha usafiri nimesikia mtu anahubiri hasomi neno anaongea tu suala la msamaha jambo ambalo ni jema lakini kilichonishangaza ni huyu mtu kuwa mgumu sana kutaja jina la yesu.

Na mafundisho yake yameonesha kumtaja Mungu mfalme wa wafalme lakini Yesu na roho mtakatifu naona limekuwa gumu mno!!na akitaja anataja kiaina hebu mwenye ufahamu atujuze na sie tusio na dini tuelewe.

Ni kipindi cha saa sita hadi saa saba leo Jumatatu.

Naomba tuelimishane sina nia mbaya.

katika IMANI kuna kitu kinaitwa HIGHER POWER je unakifahamu?
 
Ndugu yangu mambo hayo yapo sana siku hizi, kama hiyo radio ni ya kikristo ((nadhni ni ya KKKT) BASI VIONGOZI WAKE WALIANGALIE HILO, SI UNAKUMBUKA HATA HAO WANAOWEKA MABANGO YA PICHA ZAO BADALA YA KUHUBIRI INJIILI?
 
Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, ... {RUM 1:16}
Ujumbe wa Msalaba una nguvu ya Mungu
{1KOR 1:18
 
Yasiyokuhusu yaache.
Na wewe mzee wa kanisa badala utuletee hekima zako unasema hayatuhusu wakati redio inarusha mahubiri yenye shaka nusu saa nzima?hebu fafanua jambo ipasavyo,mie sijaja kuponda nataka msaada wenu au mniambie majasusi wa upande wa pili wamewazidi akili hadi mmeamua kulevel kila kitu.
 
Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, ... {RUM 1:16}
Ujumbe wa Msalaba una nguvu ya Mungu
{1KOR 1:18
Asante sana huu ni ujumbe hata kwa wale wasiotaka kuelewa na hii ndo sababu ya kuwepo redio za injili
 
Ndugu yangu mambo hayo yapo sana siku hizi, kama hiyo radio ni ya kikristo ((nadhni ni ya KKKT) BASI VIONGOZI WAKE WALIANGALIE HILO, SI UNAKUMBUKA HATA HAO WANAOWEKA MABANGO YA PICHA ZAO BADALA YA KUHUBIRI INJIILI?

Asante sana. Unayo yasema ni kweli kabisa.Niliiona video ya askofu anavyovunja amri ya sita, inasikitisha sana. Nilikuwa sijawahi kumwona kwa macho askofu huyo wa KKKT bali kwenye video hiyo chafu tu. Na siku nilipo muona kwa macho nikamtambua bila ya introduction.

Video niliyoiona ni ya ukweli na sio ya kutengeneza. Nia ya aliye inasa anasema ni kwa ajili ya kufichua uchafu wake na kujiuliza kuwa ni wangapi wameangukia mikononi mwao.

Askofu huyo akiubiri utadhani ni wa kweli, kumbe mageresha tu.
 
Ukiona hivyo huyo anayehubiriwa siyo Mungu Yehova, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Hata mimi huwa nashangaa sana mahubiri ya namna hiyo. Siku fulani niliabudu kanisa fulani, mchungaji aliyehubiri hakutaja jina Yesu Kristo hata mara moja kwa muda wote (almost 2 hours) aliosimama madhabahuni kuhubiri. Hakukemea dhambi wala kutaja neno dhambi. Hakika wana wa Mungu tumevamiwa, tuwe macho hizi ni nyakati za mwisho!

Kumbe kuna wengine kama wewe mnaabudu makanisa, kweli sasa dini zinaingiliwa hizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom