Redio E-Fm wanapika data kujiongezea ubora, ukweli ni huu

Redio E-Fm wanapika data kujiongezea ubora, ukweli ni huu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Habri wanaJF,

Redio ya E-Fm imekuwa ikitoa taarifa ambazo sasa zimethibitika kuwa ni za kupikwa zinazoonyesha kuwa wao ndio wanawasikilizaji wengi kuliko vyombo vingine kwa jiji la Dar es Salaam.

Hatukatai watu wa E-Fm wanafanya sana kazi. Sasa wajuvi wa mambo wamezama ndani na kuibuka na ukweli wenyewe;

Na kwa wasiojua Geopoll ndo watoaji wakuu wa takwimu za Radio na Tv nchi nyingi Africa. Kwa Tanzania ndio watoaji pekee

Hii ni taarifa ya kupikwa ya E-Fm Redio,

sa.jpeg

Na hizi ndio data za kutoka kwenye source za ndani,
CvmvZknW8AA24bs.jpg

CvmvZkkXEAAmKsU.jpg

CvnnDqoWIAAJuuK.jpg

CvnEGanXYAApSG8.jpg

Taarifa hizi ni Kwa msaada wa Ukurasa wa Twitter wa Ndugu: @salim_alkhasas
 
Kama ilivyo ada, siasa zilianza kwenye siasa... zikaingia kwenye soka, zikashika nafasi, kisha zikaingia kwenye bongo flavor na hatimae kwa karibu mwaka sasa zimeingia kwenye radio stations. Kote huko kuna matimu! Wakati propaganda zamani zilikuwa kwenye siasa peke yake, siku hizi kwenye bogo flavor, wanapiga propaganda... kwenye radio stations nako propaganda! What next?
 
E FM kiukweli imefanya mapinduzi halisi katika suala la radio station,kutokana na ubunifu kiukweli Wanasepa na JIJI ni Kama Msanii mpya aje kuchukua utawala wa Ali Kiba au Diamond katika bongo fleva pia Efm inatufundisha kwamba inawezekana Ukafanikiwa iwapo utajituma,Binafsi Nasikiliza radio zote but kutokana na kipindi husika lakini sana E FM na Clouds FM.
 
Wewe mtoa Uzi utakuwa mtangazaji hapo clouds,No,I meant utakuwa one of the big fish hapo mawingu.
Na wewe ukiwa kama big fish ulitakiwa ku-impove ratings na siyo kuleta hoja muflisi hapa.
 
mamia ya wasikilizaji mh!
mimi ntachojua wamemshtaki PJ kwa kuvunja mkataba.. alipe fidia mamilioni
 
Thatha mleta mada, umetumia kigezo gani kusema ulizoleta za ukweli na za wenzako zilipikwa!
 
Habri wanaJF,

Redio ya E-Fm imekuwa ikitoa taarifa ambazo sasa zimethibitika kuwa ni za kupikwa zinazoonyesha kuwa wao ndio wanawasikilizaji wengi kuliko vyombo vingine kwa jiji la Dar es Salaam.

Hatukatai watu wa E-Fm wanafanya sana kazi. Sasa wajuvi wa mambo wamezama ndani na kuibuka na ukweli wenyewe;

Hii ni taarifa ya kupikwa ya E-Fm Redio,

Na hizi ndio data za kutoka kwenye source za ndani,

Umetumwa na Clouds!? Na hapo bado hawajaingia Mikoani na hawana hata miaka miwili. Qwi Qwi Qwi.... Efm wana ipelekea Clouds Moto wa hataree.
 
Thatha mleta mada, umetumia kigezo gani kusema ulizoleta za ukweli na za wenzako zilipikwa!
Mleta mada kaleta data nusu. E FM wametoa data ya wiki zima wakati mleta mada kaleta data ya siku mbili tu.
 
Back
Top Bottom