Redio clouds leo imedhirisha kwamba hipo kimzaamzaa kwa kuendekeza mambo ya kitoto yasiyokuwa na msingi wowote ususani ktk kumuendeleza mtanzania kifikra na kadhalika kiuchumi:
Tangu asubuhi wanajadiri kufungwa kwa Manchester united na Barcelona juzi kana kwamba hakuna mtu aliyeshuudia mechi hiyo. Yapo mambo mengi ya msingi ambayo yangeweza kujadiliwa na kuweza kuleta mabadiliko ktk jamii mfano:- Usafi wa jiji, mbinu mpya za ujasiliamalii, ajari za barabarani n.k,
Hao akina Mhando na wenzie hayo mambo hawayaoni, wanabaki studio kuchekacheka na kubana pua kama machangudoa utafikiri kuna aliyewaahidi kuwapa Bia za bure kwa kushangilia Barcelona kwenye Studio.
Kwakweli sijafurahia mambo wanayoyafanya kupitia hii Redio, hakuna amabaye hakuna kwa jinsi Manchester ilivyofungwa na wala Clouds wakichonga sana Barcelona hawawezi kuwatambua bali nikukosa ubunifu wa kutumia Vyombo vya habari.
.
Si clouds tu bali WaTZ ndivyo tumekuwa siku hizi! Unakuta mtu anawafahamu mpaka 'mahouse girls' na walinzi wa Ferguson au Lionel Messi lakini hafahamu hata ni nani anasababisha matatizo yanamkabili! Time has already told us but we do not want to hear even!!!
We, vipi? Najua umekereka kufungwa na hizo kashfa za clouds fm zinakuuma, cha kushangaza TANGU ASUBUHI unawasikiliza!:dance: acha watu wafurahi, maana Man U, wangeshinda na NYIE mngefurahi! Kutesa kwa zamu!
kwanza mtoa mada nadhani anachuki binafsi na kituo hicho, kama angeona inamkera angebadili stesheni sababu ziko nyingi sana siku hizi za FM na si kuleta mambo yake binafsi hapa, pia aelewe kuwa kike kituo ni kituo cha burudani hivyo wana haki ya kufanya maamuzi gani leo watumie kuendana na tukio lililopo kwa muda huu, binafsi nadhani leo kama angepata muda angepitia sehemu mbalimbvali za kazi bila shaka angekereka sana sababu leo kila mtu ambao tangu juzi ijumaa wameachana kazini kwenda mapumzikoni leo wanakumbushia mechi hiyo au hata ile ya simba wa wacomoro, je nao arasema wana mambo ya kitoto?
Bora na mie nifanye hivyo, Clouds ni kichefuchefu