CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 6,087
- 5,352
Kuelekea Dira2050 jumla ya vijiji 12,201 kati ya vijiji vyote vya nchi hii 12,318 vyapewa hati miliki.
Katika kutekeleza mwelekeo wa DIRA2050 ya Maendeleo ya Taifa 2050 wa kujenga miji jumuishi, salama na yenye uchumi unaomlenga mtu mmoja mmoja, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha sekta ya ardhi kwa hatua madhubuti zinazolenga usalama wa umiliki na matumizi yenye tija ya rasilimali hii muhimu.
Chini ya Rais Samia mwaka 2024 pekee, Serikali iliandaa hatimiliki 111,450 za viwanja na mashamba kwa ajili ya usajili, huku ikitoa hatimiliki za kimila 87,110, ongezeko la asilimia 16.4 kutoka 74,830 mwaka 2023. Hii ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wananchi wengi zaidi, wakiwemo wale wa maeneo ya vijijini, wanapata stahiki zao za kisheria katika umiliki wa ardhi. Jumla ya nyaraka za kisheria za ardhi zilizosajiliwa ndani ya mwaka 2024 zilifikia 224,691, ongezeko la asilimia 12.2 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.
Katika kupanua usalama wa makazi, Serikali imerasimisha jumla ya makazi 297,550 yasiyopangwa, kutoka 196,146 mwaka 2023. Hili linaenda sambamba na ongezeko kubwa la michoro ya mipango miji iliyoidhinishwa 2,985 mwaka 2024 kutoka 492 mwaka 2023—ikionesha jitihada za wazi za kuimarisha upangaji wa makazi mijini na vijijini.
Aidha, Serikali iliidhinisha ramani za upimaji wa viwanja 194,209 na mashamba 7,170, pamoja na kutoa vyeti vya ardhi kwa vijiji 232, hivyo kufikisha jumla ya vijiji vilivyosajiliwa nchini hadi 12,201.
Katika kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa kwa haki na haraka, Serikali iliongeza idadi ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutoka 96 mwaka 2023 hadi 112 mwaka 2024. Katika kipindi hicho, mashauri 30,545 yalishughulikiwa, ambapo 16,969 yaliamuliwa na mengine 13,576 yaliendelea kusikilizwa.