Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Timu bado haina muunganiko hii, ni wanakimbiakimbia tu.
Kuanzia mabeki mpaka viungo wanaviwango vya kawaida tu..yaan kama hawatosajiri vizuri basi msimu ujao mateso yako palepale.
 
Courtois amekiri kuwa hawakufata mpango wa Alonso, ni aibu sana.

Ngoja tuone mabadiriko ambayo Alonso amesema, bila shaka huenda kuna wachezaji wakakalia mbao ndefu sana wasipokuwa makini.
 
Jana bekinza madrid zilikula urojo kabla ya game, maana makosa ya kitoto kabisa. Na yule ascensio anachomesha kweli kweli
 
Vipigo vinatunyemelea kwa msimu wa pili mfululizo
Mechi ya jana nauhakika itakuwa imemuonyesha Alonso namna gani afanye ili kikosi kiwe imara.

Niwe mkweli tu sikuwa na tumaini lolote la ushindi siku ya jana, PSG imetengenezwa vizuri sana.
 
Maana halisi ya kucheza kitimu ndio hawa Chelsea sasa hakuna abiria uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…