Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Natumai kila mwana Madrid kafurahia ushindi. Tukutane second leg sisi tutaingia na nguvu ya kutafuta goli moja ili tujihakikishie nafasi

Kwangu ushindi wa mbili bila bado una changamoto kidogo
Nimefurahia ushindi ila mechi ya marudiano tucheze Kwa tahadhari kubwa nidhamu kubwa tusipate yellow card kwani itabidi baadhi wakose mechi hapo ndipo viraka akina NACHO wataingia na kuchomesha. Chelsea game ya marudiano ata shambulia kama nyuki
 
Sio kwa chelsea hii mbovu inayopigwa na wolves na nyukesto point 6
 
Mtaniii.

Nilisahau kuwapongeza kwa ushindi wa Camp Nou. Ilikua lazima mshinde, maana hata psychologically, mlikua more motivated to win kutuzidi. Tulikua tumewapiga mechi nyingi mfululizo, njaa yenu ilizidi njaa yetu.

Kwa Chelsea niliwatabiria kushinda siku nyingi tu. Chelsea hata akipewa Yanga, hapindui. Nadhani next round mnakutana na Man City. Sioni kama mko na quality ya kumpiga Pep Guardiola kwa sasa. Labda zitokee ngekewa!

Kuhusu copa del Rey, ngoja ile curse yenu iwashughulikie. Mtaikosa kimaajabu sana!

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…