Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Jana ilikuwa full shwangwe kuanzia mtanange wa kirumba na Paris pia.

Kikubwa kinachofurahisha kwa Madrid wakifikaga robo final tu wanabadirikaga hatari. Mechi ya jana ilikuwa wazi kwetu. Kwanza timu tulizopita nazo ukianzia na PSG,CHELSEA ndio ikaenda mpaka extra time,Man city zote vigogo. Ongezea na bahati jana ilikuwa lazima Liver waangamie. Hiyo ndio REAL MADRID hasa.
 
Wameanza sub zao za bila macho kumtoa Luis Diaz ni janga jingine kwao
Luiz jana ilikuwa ni lazima atolewe. Cavajal jana alimkaba kila kona. Ni bahati mbaya hata Keita alipoingia akawa butu kuliko Luiz. Pongezi kubwa kwa strategy ya Real Madrid hasa kwenye ukabaji. Ulinzi ulikuwa shirikishi. Kila mchezaji jana alikuwa ni beki hata Benzema na ndio maana Real Madrid haikuwa na shots nyingi kule mbele
Mfano VJ alikuwa na attemp 1, on target 1, goli 1
RM shots
Total 4
On target 2
Goal 1

Liver
Total 24
On target 9
Goal 0

Kipa MOTM
Militao supurb
Carvajal moto
Mendy on fire
Casemiro alidhobiti vizuri katikati
 
Ile battle ya Carvajal na Luis Diaz ilikuwa kubwa sana, halafu kuweka mambo kuwa magumu zaidi Valverde na yeye akawa anashuka kumsaidia Carvajal, wakipanda wanapanda wote, huku nyuma Militao anafanya follow up., huo upande kulikuwa na battle haswa, tofauti na watu walivyo kuwa wanafikria kuwa upande wa Arnold na Vini Jr ndio ungekuwa wa moto.

Tulikuwa na shots ndogo kwenye lango la Liverpool kwa kuwa Valverde alikuwa anachelewa kupanda kusaidia mashambulizi., pia Toni na Casemiro hata Modrić muda mwingi walikuwa wanachelewa kupanda, ninaona kama walikuwa wanavuta muda ili kipindi cha pili waanze kushambulia Liverpool wakiwa wamejisahau na kuchoka., na ndio kitu kilichotokea., kuona kama hawa hawatakuja, kushangaa watu wanashangilia., hapo ndio experience inaonekana.

Muda mwingi nilikuwa na wasi wasi na aerial threats kutoka kwa Liverpool kwenye set pieces, ila Militao alifanya hiyo kazi kwa umakini sana.,
 
Na plan ya Ancelloti ilikuwa kuwaingiza Rodrygo na Camavinga ili sasa tuende kushambulia, ila alipoona tumepata goli basi akambakiza Casemiro na Kroos uwanjani ili wakamilishe kazi waliyoianza., kwasababu jana Casemiro licha ya kuwa mzito, ila jana alikuwa anafanya marking kwa umakini sana, Alaba alikuwa anapanda anatibua kisha anamwachia Casemiro kazi ya kuweka mambo Sawa.
Thiago ni aina ya wachezaji kama akina Ozil, huwa hawaangalii matokeo, mfungwe ama mshinde yeye ataendelea kucheza vile vile., Sasa wale wetu huwa wana badilika kutokana na hali ya game.,
Nimeona Robertson akihojiwa, anasema kuwa Real Madrid wanajua namna ya kumaliza mpira endapo wamepata matokeo., na hapo experience ndio huwa hutokea.
Nikiangalia game za PSG, Chelsea na City, ingekuwa ni sisi tulikuwa tumepata yale matokeo awali basi mambo yangeishia pale pale.,
 
Halllaaaa,
 
Hivi yule Diaz ana umri gani? Yule jamaa ni mzuri sana, kama umri bado basi atakuja kuisaidia Liverpool huko mbeleni.
 
Kwani jana Liver kamiliki mpira ilikuwa almost 50/50
Tofauti jana liver walicheza staili yao ya kawaida kwa kujiamni. Wao walijua watafunga magoli mengi na kweli bila umahiri wa Courtois goli jana zingeingia 4 hdi 6 wavuni mwa RM
 
Swali haliji kutoka point of view hiyo, Pasi ya Mpira uliokwenda kwa Benzema ilitoka kwa mchezaji wa Liverpool, Kwa maana hapakua na offside pale, Refa alivurunda.
Naona VAR na refa walichukulia ule mpira ulimgonga mchezaji wa liver ndio ukaenda kwa Benzema, kama ni hivyo ile ilikuwa offside halali
Naona kwenye sheria za mpira kuucheza mpira ni hadi kuwepo na intent/kusudio la kuucheza kitu ambacho jana beki ambaye mpira ulimgonga hakuwa na harakati yeyote ya kuucheza ule mpira badala yake ulimgonga ukadivert kwa Benzema ambaye alikuwa offiside
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…