Madrid hatuwezi kudumu na striker 9 "kamili" wa kufunga magoli tu, kila striker akija wa kukaa mbele peke yake tutaishia kumtukana.
Kwasababu mfumo wa Real Madrid tunacheza kiteam zaidi siku hizi, tofauti na enzi za kina Raul Blanco, sasa hivi kuanzia midfield mpaka mabeki ni wafungaji sio striker peke yake. Halafu namba 9 wa madrid anatakiwa awaweke bussy mabeki wa timu pinzani ili wasitoke nyuma, kutengeneza nafasi ili ma winger wafunge na kuruhusu midfiled wetu waweze kuzunguka na kushambulia muda wote. Ndio maana moratta hakuweza kukaa, japo alikua anafunga ila hakuweza kuwachezesha kina Ronaldo na Bale na viungo, alikua anawaza kukaa mbele na ndio maana alikua rahisi kufichwa kwenye match.
Natamani hao vijana wetu wadogo wawe wasumbufu sana kama big benz, huyu jamaa ndio alikua anamchezesha Ronaldo, na Ronaldo alikua anampenda sana kucheza nae. Pia vijana wawe wanarudi mpaka nyuma kukaba na kupandisha timu mbele, ila wakitaka wacheze kwa kufunga tu magoli na kukaa mbele hawata dumu, au mfumo ubadilishwe kabisa wa timu.