Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Kwa anae kataa kuwa ile sio Penalty, atuwekee maoni yake kuhusu lile tukio...!!

Lakini wachambuzi wamekili kuwa ile penati ni halali.
 
Hakuna mchambuzi yeyote wa soka duniani akaichambua foul ya Leo tuliyopata penalty nikamuelewa..kikubwa tumebebwa hakuna ubishi na kwenye soka mambo kama haya yapo. This was a big game and referee should be very keen in decision.. Michael Oliver kafeli kwenye kuweka ile penalty, nauhakika tungepita kwa goli zuri tu kama tungeenda 120.
 
Mkuu nina mashaka na knowledge yako ya soka, sheria ni sheria haingalii muda, game au nani katenda.

Itakua ata goli la Sane jana lililokataliwa unaamini ni goli.

Hii pk ya leo ni pk halali kabisa, hata ingekua katikati ya uwanja bado ingeitwa faulo. Tatizo leo imetokea kwenye game kubwa, ndani ya box na muda mbaya ila Ile Ni faulo na unajua faulo ndani ya box maana yake Nini

Kama jana goli la Sane lilikataliwa sababu alimuingilia Milner nyuma, leo Vasquez kasukumwa kabisa toka nyuma, ni vp isiwe foul


Otherwise unataka baadhi ya sheria zisiwe zinatumika kwenye baadhi ya matches.
 
Braza why stressing yourself!?
Haikuwa mechi nzuri ila mwishoni tumepata penalty na tumepita.

Wacha tufurahi tuwaze next mechi hapa
 
Mzee Jecha jana kapiga mkwanja wa nguvu huko Roma. Sasa Nasikia Juventusi wanamtafuta Mzee Jecha kakimbia
na pesa zao...
 
Anyway,
Hebu nijipe muda kidogo nikaiangalie kwa umakini mkuu.

Ila kwa mtizamo wa haraka haraka,

Sikuona Kama kuna contact yoyote ilotokea nyuma ya Vazquez.

Nlichokiona ni kwamba, Vazquez alipoteza balance alipo upokea mpira kifuani

Na pale ndipo beki wa juve, alipouwahi akafanya clearence kifuani kwake kabla ya Vazquez hajafanya maamuzi

Kitu ambacho nakiona ni jambo LA kawaida sana kwny mpira kwa mabeki wengi kufanya clearence za namna ile.

ANYWAY,
Mkuu, NTAITIZAMA TENA KWA UMAKINI ZAIDI MKUU ILI NIJIRIDHISHE.
 
Na laiti yule beki kama ule mpira angeugusa basi isingekuwa penalty
 
Beki wa juve haku ugusa mpira na ndio maana ilikiwa penalty.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…