Re:Najaribu Kumsahau lakini Nashindwa

Re:Najaribu Kumsahau lakini Nashindwa

Kila chenye mwanzo kina mwisho,vumilia na ukimkumbuka tu nenda kijiweni kwa masela kapige stori.
Ushauri gani huo!! mizigo mbona ya kumwaga tu!?

1013726_10201377222340881_1799758292_n.jpg
 
mke mwema hutoka kwa bwana muombe sana mungu akusaidie utasahau tu. pole sana
 
[QUOTE=msd;
Wake up brother and reason like a grown Man, huyo hakupendi na apenda attention yako tu, unavyomsumbukia n.k Pia hajakomaa na hana mipango na wewe ndio maana hatulii. Kifupi kinachokusumbua ni hangover ya uhusiano. Tafuta hobby mpya, marafiki wapya wenye mtazamo wa kimaendeleo, badili uvaaji wako(jipende zaidi), fungua biashara, acha kuangalia picha zake wala movies mlizoona nae, badili perfume, safiri, date mtu mzuri hata kama ni temporary na si lazima iwepo sex n.k Acha kujiendekeza, wake up kuna wanawake mamilioni wewe unapiga kelele sababu ya mmoja asiekupenda?
 
Mimi ni Kijana wa Kiume,Nimebahatika kuwa na uhusiano na msichana mmoja since amemaliza form six mpaka karibu anakaribia kumaliza chuo ndo mambo yakaanza kwenda out of my expectation,kwa kweli tulikuwa tunapendana sana na tukawa tumetambulishana kwa baadhi ya ndugu zetu,before nilitaka tufunge ndoa akiwa mwaka wa pili kwa sababu nilikuwa na plan yakwenda kufanya Masters,but akawa amepropose mpaka amalize chuo basi tukawa tumekubaliaba,kwa kweli nilikuwa nampa everthing ili asipate vishawishi chuo.
Kuanzia mwezi wa pili mwaka huu akaanza kuwa hapokei/kujibu simu nikimpigia ama niki-sms na hanitafuti mpaka tena nimtafute mimi tofauti na awali alikuwa yupo sharp kunijibu,nikajaribu kumuuliza why anafanya hivyo akawa anajibu masomo yapo tait ndo maana.
Nikaanza kufanya utafiti nikaaja gundua kwamba ameanza kudate na wanaume wengine nikajaribu kumuuliza akasema hana uhusiano wowote ni normal friendship,baada ya hapo akawa amerudi kawaida..
Lakini ilivyo fika mwezi wanne nikawa nje ya Dar es salaam mwezi mzima kikazi,siku nasafiri ndo balaa likaanza kila nikimpigia,nikimtumia sms hajibu mpaka nimpigie rafiki yake nimuombe niongee naye ndo tutaongea,Basi imeenda same situation,kwa kama miezi miwili ikabidi niwache kumtafuta kwa sababu nilikuwa over stressed,Nikashindwa kufanya kazi kwa almost three days,nikawa kama naumwa ndo rafiki yangu mmoja tunaefanya naye kazi aka notice kuna kitu kinanisumbua akaniomba nimuambie basi nikamuambia everthing,akanishauri nijaribu kuacha kuwasiliana naye kwa muda tuone response yake,basi baada ya kama mwezi mmoja akawa amenipigia,nikamuuliza why anafanya hivyo akanijibu steel ananipenda but ameamua tu aishi hivyo,mwezi wa tano nikawa nimerudi Dar nimejaribu kumtafuta ili tuongee lakini ananipiga chenga,Nikawa nimeamua nimuache na maamuzi yake,kwa sababu niliona mm ndo naumia zaidi.
Tumekaa kama week kaanza tena kuni sms,na kuni call,lakini kila akinitafuta anasababisha nianze kumfikiria kwa nini amefanya hivyo na hajawahi kuniambia reason,Lakini trend ikaenda kama week tena akakata tena mawasiliano.
Hebu nisaidieni ili niweze kumtoa kichwani mwangu kwani kila siku namfikiria yeye ukweli bado nampenda.
Lakini vile vile nimeanza kuchukia kupenda katika maisha yangu na sitaki uhusiano wowote kwa muda huu.
naelewa maumivu unayoyapitia kwa kipindi hichi mkuu,mahusiano ni matamu sana km mnapenda kwa dhati ila ni ugonjwa wa moyo ikiwa ni vise versa, jaribu kujisomea au kuingia jf wakati upo free au unaweza kuanza program ya kufanya mazoezi wakati wa jioni ili kujichosha hivyo kupata usingizi usiku,jaribu kukumbuka vile alivyokuumiza ukifanya hivyo nina imani utamchukia, nadhani unamkumbuka na unaumia pale anapokupigia, unaweza kuiweka namba yake ktk call reject ili asikupate kama simu yako inauwezo huo,nafikiri ukifanya hivyo utamsahau mkuu, watu wanafiwa na wazazi wao ambao waliwapenda na kuwathamini lakini wanawasahau sembuse mtu umekutana nae ukiwa mtu mzima? time will heal all the pain mkubwa.
 
Mapenzi yanatesa sana! Miye nahsi nshamsahau! Ila kikubwa mshukuru mungu kwanza kwani hata hiyo kupropose kufunga ndoa baada ya yeye kumaliza ni mpango wa mungu! So usimlaumu,hakupendi alikuwa anakutumia tu ili amalize shule yake that y kaanza vi2ko mwishoni! Chamsingi mpotezee mazima usipende kukaa peke yako,usipokee sim yake wala kujibu text zake utaumia mwache na uhuru wake ! Japo ni ngumu ila jiridhishe! Ipo siku yataisha na utaona kawaida saana! Kila la kheri na pole!
Shukrani sana,,nitajaribu kufuata ushauri wako
 
Uyo mwanadada akikutana na wenzie wanajazanaga ujinga vyuoni na kusahau kuna maisha baada ya hapo,ulipotoka nae alishapasau sasa anaishi kwa ndoto,wanarahisisha maisha ndio maana hata wanaume vyuoni walio wengi huwezi kuta anademu wa kudumu,mim nakushauri maisha ni marahisi sana ukijitambua,huo ni mwanzo wa suluba kama utaishi nae kwa kulazimisha,fanya maamuzi ambayo baadae utayafurahia,achana nae hakufai tena kwa kukudhibitishia hafai wewe muache uone akimaliza chuo na hayo mapenzi ya kusadikika vyuoni uone kama haji kwa magoti,KAKA JITAMBUE ACHANA NA HAO WADUDU UTAUGUA PRESHA AU KUFA KABLA YA WAKATI WAKO WAKATI ULIEKUUMBA ANAKUHITAJI ULIMWENGUNI ZAIDI.POLE SANA
 
Mimi ni Kijana wa Kiume,Nimebahatika kuwa na uhusiano na msichana mmoja since amemaliza form six mpaka karibu anakaribia kumaliza chuo ndo mambo yakaanza kwenda out of my expectation,kwa kweli tulikuwa tunapendana sana na tukawa tumetambulishana kwa baadhi ya ndugu zetu,before nilitaka tufunge ndoa akiwa mwaka wa pili kwa sababu nilikuwa na plan yakwenda kufanya Masters,but akawa amepropose mpaka amalize chuo basi tukawa tumekubaliaba,kwa kweli nilikuwa nampa everthing ili asipate vishawishi chuo.
Kuanzia mwezi wa pili mwaka huu akaanza kuwa hapokei/kujibu simu nikimpigia ama niki-sms na hanitafuti mpaka tena nimtafute mimi tofauti na awali alikuwa yupo sharp kunijibu,nikajaribu kumuuliza why anafanya hivyo akawa anajibu masomo yapo tait ndo maana.
Nikaanza kufanya utafiti nikaaja gundua kwamba ameanza kudate na wanaume wengine nikajaribu kumuuliza akasema hana uhusiano wowote ni normal friendship,baada ya hapo akawa amerudi kawaida..
Lakini ilivyo fika mwezi wanne nikawa nje ya Dar es salaam mwezi mzima kikazi,siku nasafiri ndo balaa likaanza kila nikimpigia,nikimtumia sms hajibu mpaka nimpigie rafiki yake nimuombe niongee naye ndo tutaongea,Basi imeenda same situation,kwa kama miezi miwili ikabidi niwache kumtafuta kwa sababu nilikuwa over stressed,Nikashindwa kufanya kazi kwa almost three days,nikawa kama naumwa ndo rafiki yangu mmoja tunaefanya naye kazi aka notice kuna kitu kinanisumbua akaniomba nimuambie basi nikamuambia everthing,akanishauri nijaribu kuacha kuwasiliana naye kwa muda tuone response yake,basi baada ya kama mwezi mmoja akawa amenipigia,nikamuuliza why anafanya hivyo akanijibu steel ananipenda but ameamua tu aishi hivyo,mwezi wa tano nikawa nimerudi Dar nimejaribu kumtafuta ili tuongee lakini ananipiga chenga,Nikawa nimeamua nimuache na maamuzi yake,kwa sababu niliona mm ndo naumia zaidi.
Tumekaa kama week kaanza tena kuni sms,na kuni call,lakini kila akinitafuta anasababisha nianze kumfikiria kwa nini amefanya hivyo na hajawahi kuniambia reason,Lakini trend ikaenda kama week tena akakata tena mawasiliano.
Hebu nisaidieni ili niweze kumtoa kichwani mwangu kwani kila siku namfikiria yeye ukweli bado nampenda.
Lakini vile vile nimeanza kuchukia kupenda katika maisha yangu na sitaki uhusiano wowote kwa muda huu.

kazi rahisi sana.
Fanya hivi......toa fikra za kumuona yeye ni mzuri kuliko wengine..kwa kufanya hivyo utaupa ubongo nafasi ya kuchagua alie mzuri zaidi yake then akili itakuonyesha huyo mrembo (mzuri zaidi yake).........fanya mbinu zako mtongoze then utamsahau huyo aliyekutosa na utaona alikuwa anakupotezea mda.

Pole kwa yaliyokupata. Jipe moyo ni stage ktk maisha meeeeeeeeeeeeeeeeeeen
 
Another broken heart........ pole ndugu, najua hasa unavyojisikia, you have two options 1. to forget her completely which is the best. ukishindwa opt number 2. Jibembeleze tu, mtafute mfuate umuombe muendelee kuwa wote, fight for your love, kuwa chini utumikie moyo wako. Ila ujiandae kuwa responsible kwa concequences iwapo umechagua option 2.
 
Uyo mwanadada akikutana na wenzie wanajazanaga ujinga vyuoni na kusahau kuna maisha baada ya hapo,ulipotoka nae alishapasau sasa anaishi kwa ndoto,wanarahisisha maisha ndio maana hata wanaume vyuoni walio wengi huwezi kuta anademu wa kudumu,mim nakushauri maisha ni marahisi sana ukijitambua,huo ni mwanzo wa suluba kama utaishi nae kwa kulazimisha,fanya maamuzi ambayo baadae utayafurahia,achana nae hakufai tena kwa kukudhibitishia hafai wewe muache uone akimaliza chuo na hayo mapenzi ya kusadikika vyuoni uone kama haji kwa magoti,KAKA JITAMBUE ACHANA NA HAO WADUDU UTAUGUA PRESHA AU KUFA KABLA YA WAKATI WAKO WAKATI ULIEKUUMBA ANAKUHITAJI ULIMWENGUNI ZAIDI.POLE SANA
Shukrani sana mkuu kwa kunipatia matumaini mapya.
 
Kuna game kwenye iPhone inaitwa Cindy Crakers-very addictive jaribu hiyo kila kumbukmbu ikija
 
I know how it feels bro...time heals...only time
 
Mapenzi yanatesa sana! Miye nahsi nshamsahau! Ila kikubwa mshukuru mungu kwanza kwani hata hiyo kupropose kufunga ndoa baada ya yeye kumaliza ni mpango wa mungu! So usimlaumu,hakupendi alikuwa anakutumia tu ili amalize shule yake that y kaanza vi2ko mwishoni! Chamsingi mpotezee mazima usipende kukaa peke yako,usipokee sim yake wala kujibu text zake utaumia mwache na uhuru wake ! Japo ni ngumu ila jiridhishe! Ipo siku yataisha na utaona kawaida saana! Kila la kheri na pole!

Nakumbuka wangu alifanya nikawa napiga push ups usiku ili nichoke nilale. Nilivotulia na yeye kule yalipochacha akaja, nilimfukuza kama simjui hadi akanishangaa kuwa 'hivi na wewe unaweza nifanyia hivyo mimi?' nikamwambia I am not the one you left, so find the guy you left not me. Hakuamini.
 
Dah! Mkuu wacha na mimi nipige push ups...teh teh teh umenifuraisha aisee
 
pole sana mkuu na zidi kumuomba mungu ili uweze kuwa sawa tena.. usikate tamaa kwani haya ni majarib ya dunia tu na nimapito pia..
 
Mapenzi hayalazimishwi kama mtu hataki kupokea simu, sms kwa nini huangaike nae ukimlazimisha sana baadae atakusumbua. Jaribu kutokukumbuka mazuri yake na pia usipende kukakaa peke yako, penda kwenda kwenye sehemu za mjumuiko ili usipate msongo wa mawazo.
 
pole sana mkuu, huyo lazma atakuwa amepata mwanaume mwengine. we fanya shughuli zako usiwe unamuwaza waza sana.
 
Back
Top Bottom