Re: MMU

Re: MMU

watoto wa mujini wanawaumiza sana wakina kaka na dada ndo malalamiko yamekua ni mengi
 
Iv liz na ashadii wana id mupya???longtime.
kwel mmu changanyikeni mihogoni..ktk post sita mbili sifikishi au nachelewa ,mbili nimetendwa au natenda,mbili huyu demu au huy hawara...
Bora natalia,sijamckia nayeye kamuda kwel

Swts nipo kwa ID hii hii... Tajitahidi kujichanganya zaidi. Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:
watu wana majukumu.wengine walikuwa single,baadae wamepata wenza wanaona jf basi tena.wengine wana watoto wachanga,muda wa jf unakuwa haupo tena.wengine wanaona mambo ndio hayo kwa hayo,wanatafuta vijiwe vyengine.wengine wametendwa jf,wanaiona chungu hawarudi tena.
 
nina amini wengine wakitoka,hata hao wapya wakiingia,huwa wanachangamsha tu.ni mzunguko.namkumbuka michelle alikuwa mtu mwenye mawazo mazuri.or maybe wengine wanabadilisha id
 
Fanya hima AshaDii, jukwaa limekaliwa na Yona edson sasa hivi, mada zake ukiziona utachoka

Kama unaona thread haina mashiko si lazima kuchangia. Wengi wa wanajamvi wameyageuza baadhi ya majukwaa mathalani MMU kama vijiwe vya kupiga soga badala ya kutoa ushauri, maoni, mitazamo n.k.
Kwa mantiki hiyo basi sahau kuwaona wanabodi kama AshaDii, SnowBall, watu8, Kaunga na wengineo wengi wakija mara kwa mara pande hii kutoa nasaha zao.
 
Last edited by a moderator:
Sio lengo langu kuwatuhumu Moderators na JF owners, lkn nafikiri wanafaidika na idadi kubwa ya members na users kiasi kwamba kumonitor nini kinachangiwa sio priority kiviile.

Excuses zao wazitoazo pindi malamiko yakizidi huwa ni; 'vijana wanajiunga nao wana haki na niwajibu wetu kuwaongoza na pia wakipotoka basi tubonyeze kitufe cha report abuse'. MMU imekuwa chit chat, so tukiboreka tunakuja kupiga story badala ya kuomba au kutoa ushauri wa matatizo ya msingi.

So good, tuko wengi in terms of idadi lkn quality inapungua. Hata siasani watu wanalalamika. Jamii Intelligence pia hukuti vitu vya nguvu. I guess people have other better things to do.
Kama unaona thread haina mashiko si lazima kuchangia. Wengi wa wanajamvi wameyageuza baadhi ya majukwaa mathalani MMU kama vijiwe vya kupiga soga badala ya kutoa ushauri, maoni, mitazamo n.k.
Kwa mantiki hiyo basi sahau kuwaona wanabodi kama AshaDii, SnowBall, watu8, Kaunga na wengineo wengi wakija mara kwa mara pande hii kutoa nasaha zao.
 
Last edited by a moderator:
Shikamooni,

Ninajua mtabisha kama ilivyo kawaida yenu ila Niseme tu ukweli, hili jukwaa limefulia, kila nikifungua sioni la zaidi sana sana ni watu wanalia lia tu kwamba wametendwa, wengine watalipa kisasi na wengine kama akina yona edson kuja na mada zao zisizo na mguu wala mkono.

Tatizo ni nini? labda kupotea kwa akina lizzy, ashadii, yule mwenye ID yenye 1980 na wengineo ndio kumelichokesha? mie sijui, ila ukweli limefulia.

Laleni salama.

Kwa maoni yangu naona kuna ukweli fulani, lakini si limefulia kiasi hicho maana bado kuna post nyingine nyingi tu nje za hao wanaolialia kila siku. Na tukumbuke kuwa hili ni jukwaa linalozungumzia MMU na hivyo ni sehemu muafaka ya kuomba ushauri ingawa kwa sasa inaonekana topic zinajizojirudia rudia zimeongezeka kwa kasi kubwa.

Kwa mfano kuna watu kama ndugu yetu Mtambuzi ambaye amekuwa akijitahidi kutupa elimu za utambuzi na tafiti mbali mbali ambazo kwa sehemu zimekuwa zikitupa changamoto mbali mbali. Pia wapo wengineo wengi ambao wamejaribu kutupa hadithi na simulizi mbali mbali zenye lengo la kutuburudisha. Hao ni lile kundi la akina MziziMkavu! Wapo wengine ambao wamekuwa wakitupa furaha na jokes za kutufanya tuondoe stress kama akina lara 1 na Natalia yule mutoto ya tajiri! Tunao walimu kama akina gfsonwin na kundi lake nao wanatusaidia sana na hasa kwa wale wanaolia lia kupata japo ushauri wa bure.

Kuna mengi sana naona yanafanyika hapa jukwaani ingawa ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya topic zinabore na zingine zinajirudia rudia sana, Labda elimu itolewe hasa kwa watumiaji wapya ambao mara kadhaa wamerusha topic ambazo kwa fikra zangu naona lengo lake ni kuanzisha gumzo tu. Zipo zile za kutafuta wachumba pia, ambazo huenda wamiliki wa jukwaa wangezitafutia Jukwaa maalum (kama halipo kwa sasa).

Copy: AshaDii, Kaunga, nyumba kubwa, snowhite, SnowBall, Eiyer, Nivea, [MENTION]Mr. Rocky[/MENTION], Kongosho, charminglady na wana MMU wote!!!
 
Last edited by a moderator:
jana kuna mahali nilikumbuka jamvi lilikotoka nikatolea aina ya nyuzi zilizokuwa zinawekwa hapa jamvini. as for me sion kwamba ni kutokuwepo kwa watu fulan ndi sababu bali naona akili za watu sasa hivi zimeshikwa sna na maisha ya kutokufikiri wala kutokuumiza akilli.

kwa mfano jana kauga aliweka uzi ambao ulikuwa unahitaj kuwaza sana hapa mmu ulikuwa ni uzi mzuri sana kwa vijana ambao bado ni singles ila cha ajabu zaid ya Kongosho na Kaunga , snowhite, Nicas Mtei FP labda na mm sikuona watu wengine wakijariu kuibua hoja ndani ya mada ile. nilikaa na kuwaza sana kwann hawa vijana wadogo hawataki kuumiza akili zao japo wawaze kidogo kuhusu maisha??

nafkiri kwa sasa hata mm nitajitahd niwe naleta mada ambazo zitatufanya kufikiri zaid zaid kuliko kuwa watu wa kutoa ushauri tu. pia MODS muwe makini mada sijui ya natafuta suga mammy, ama mm ni shoga na za kufanana na hizo msiziweke hapa jamani jamvi hili lina heshima yake.

mada kama hizo muusika apeleke RAHATUPU BLOG. GUMZO LA JIJI NA MARAFIKI.COM.

Otherwise wale ambao tunawamiss hapa jamvini jamani njooni,,,,,,,,,,,,,,,hasa AshaDii.
 
Last edited by a moderator:
Kwa muono wangu ni kuwa mada za Msingi zipo sana, ila nikiri na kukubali kuwa ni kwa uchache; kuna wadau hurusha threads za msingi mara nyingi sana ingawa siyo wengi huchangina hizo threads. Mfano kuna ladyfurahia na Nicas Mtei napenda threads zao, na mara nyingi ni za kujenga na huwezi kukosa kitu.

Threads nyingi sana zimekuwa za kutaka kusaidiwa kuliko zile ambazo zinatowa na kufunza moja kwa moja. Inapotokea Jukwaa zima lina threads zaidi ya 30 ambazo zote ni kuomba ushauri, kulalamika ama kutowa lawama inevitably Jukwaa lazima lionekane kama vile limefulia.

Hata hivyo kuna wadau ambao wanajitahidi kuleta mada mara kwa mara za kuelimisha kama ilivyo kwa Mtambuzi, gfsonwin na MziziMkavu , ila sasa sema idadi ya watoa mada za kuelimisha imepungua hivyo kwa wale ambao wapo interested sana katika kupata kitu kuliko kutoa ushauri kwa kiasi kikubwa huona kuwa kuna mapungufu makubwa sana.

Mie napenda sana masuala yanayohusiana na mahusiano... The complexity of it... Namna yasivyo na formulae na jinsi yasivyochosha kutaka kufahamu zaidi sababu ni kitu ambacho tunacho kila siku ya Mungu. Safari hii nitajitahidi pia kuwa mmoja wao wa watakaotuma mara kwa mara... Na tunaomba pia members kama Mbu, MwanajamiiOne, Lizzy, Asprin, na wengine wengi warudi na mada kuongeza idadi ya mada za kujenga na kuongeza mijadala na pia kwa wale ambao wapo na wana uwezo huo tuzidi kushirikiana.

Napenda nitoe much respect kwa wale ambao hujitahidi sana kutoa michango ya kujenga kwa mada mbali mbali ingawa si warusha thread mara kwa mara, michango yao ni mizito na ya kujenga pale wanapo amua kutoa hasa mawazo na misimamo yao. To mention but a few Kaunga, Kongosho, King'asti, HorsePower, SnowBall, snowhite, nyumba kubwa, Nyamayao, Dark City, Roulette, Mr Rocky na wengine wengi siyo rahisi kukumbuka wote. Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:
yale yote yaliyoletwa hapa wahusika hawayafanyii kazi ndio maana watu wamechoka kuleta mada wanaleta porojo tu
 
Back
Top Bottom