Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,279
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam imesema ipo tayari kutoa usafiri kwa ombaomba wanaotaka kurudi kwao kwa hiari ifikapo mwezi wa sita mwaka huu. Huku akiwataka Wakuu wa wilaya kuratibu zoezi hilo ikiwamo pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria mawakala wanao waleta kutoka mikoani.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala amewataka ombaomba wote walipo Dar Es Salaam kujiandikisha kwa hiari majina yao pamoja vijiji wanavyo toka ili ofisi yake iweze kuwarudisha nyumbani na kuwaepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo mwezi wa sita mwaka huu ofisi yake iweze kuwapa usafiri wa kuwafikisha makwao suala ambalo ameleza limewapa usumbufu wakuu wa mikoa waliopita akiwemo Mzee Yusufu Makamba.
Aidha Mhe. Makala ameongezea kuwa suala la ombaomba limekuwa mradi kwa mawakala ambao uwasaidia ombaomba hao kuwasafirisha kutoka makwao na kuwapagishia vyumba pamoja na kuwapa chakula na kuwataka walelete pesa wanazoomba kila siku.
Katika hatua nyingene Mkuu wamkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye madhimisho ya siku ya kujenga uwelewa juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi.
ITV