RC Tabora aagiza kuwe na benki za matofali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza Halmashauri zote kuwa na Benki ya Tofali kwa kila Kijiji.

Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa pindi muda wa wanafunzi wanapotakiwa kijiunga na Darasa la Kwanza ama Kidato cha Kwanza.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui.

Alisema kutokana na maoteo ya watoto wanatakiwa kiujiunga na Darasa la Kwanza kila Mwaka ni vema kuwepo na mipango endelevu la kukabiliana na ongezeko la watoto wanaingia Kidato cha kwanza kila Mwaka.

“Hatakiwa kuwa na mipango ya zima moto ya kusubiri watoto wachaguliwe ndio tuanze kufukuzana na ujenzi wa madarasa, tuweke mipango mizuri ya kutowafanya watoto wawe wanachelewa kujiunga na masomo eti kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarsa” alisisitiza

Aliongeza kuwa sanjari na uwekaji wa mipango ya kuweka na benki ya tofali lazima kuwepo na utaratibu wa kutengeneza madawati ya kutosha ili kutowafanya wanafunzi kukaa chini.

Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa Tabora inayo mistu ya kutoshahakuna sababu ya wanafunzi kukaa chini.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wazazi kuweka mazingira yatakayowavutia ili walimu wapende kufanyakazi mkoani Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akizindua Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui leo

Michuzi Blog
 
Nimekumbuka mkoa wa Ruvuma mwaka 2016/2017,tofari hazikua na ubora na ziliishia kuharibika tu.
 
Bank za matofali zikoje hizo? Serikali bwana, rahisisheni msemo ili wananchi waelewe mnachokusudia. Eti Heading inasema "bank ya matofali" taarifa inazungumzia kingine.😆😆😆 hii nchi shida tupu

Halafu mutuambie matofali yapi ayo? Block or yakuchoma?
 
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza Halmashauri zote kuwa na Benki ya Tofali kwa kila Kijiji.

Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa pindi muda wa wanafunzi wanapotakiwa kijiunga na Darasa la Kwanza ama Kidato cha Kwanza.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui.

Alisema kutokana na maoteo ya watoto wanatakiwa kiujiunga na Darasa la Kwanza kila Mwaka ni vema kuwepo na mipango endelevu la kukabiliana na ongezeko la watoto wanaingia Kidato cha kwanza kila Mwaka.

“Hatakiwa kuwa na mipango ya zima moto ya kusubiri watoto wachaguliwe ndio tuanze kufukuzana na ujenzi wa madarasa, tuweke mipango mizuri ya kutowafanya watoto wawe wanachelewa kujiunga na masomo eti kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarsa” alisisitiza

Aliongeza kuwa sanjari na uwekaji wa mipango ya kuweka na benki ya tofali lazima kuwepo na utaratibu wa kutengeneza madawati ya kutosha ili kutowafanya wanafunzi kukaa chini.

Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa Tabora inayo mistu ya kutoshahakuna sababu ya wanafunzi kukaa chini.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wazazi kuweka mazingira yatakayowavutia ili walimu wapende kufanyakazi mkoani Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akizindua Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui leo

Michuzi Blog
Akili za Ma Rc wetu ni za kawaida hazina tofauti na za watu wanao ongozwa
 
Pamoja na idea yake mwakani bado atazima moto kujenga vyumba vya madadasa muda ukiwa umeisha. Kwa sababu hata yeye pia haamini hiyo idea.

Kama yuko serious ajenge sasa
 
Wazo zuri sana likisimamiwa ipasawvyo na hii ingekuwa Kila shule kupitia pesa za elimu bure inatenga fungu tatizo watu Wana njaa na shida za kijinga wataishia zila pesa au kuuza tofari
 
Ni hela na wema tu ndio akiba isiyooza,
Vingine vyote ni ngonjera,
Hela zitakaa benki, kwa gharama ndogo, ila tofali ni gharama kuzihifadhi
 
Kwani mkoani hakuna planning officers...au wapo lakini majukumu Yao wanafanya wanasiasa?
 
Back
Top Bottom