RC Singida: Nilimuweka DMO rumande ili apate akili

Mkuu hapo kwenye dots nimeshindwa kuconnect, ulitaka kuandika nini?
 
Kati ya RC na Waziri nani ana nguvu dhidi ya mwenzake ilhali wote wameteuliwa na mtu mmoja?
Waziri ataendelea kulalama jukwaani ila hana power yeyote dhidi ya RC. Kwani Gambo si alimvimbia prof.Maghembe na hakuna kilichofanyika? Au Bashite vs Nape!
Ni sawa na ukoo wa kambale
 
Huyu mama nilikuwa namuona wa maana tangu amuweke ndani Daktari nimemshusha thamani halafu hiyo hapo juu ina maana anamjibu Waziri wa afya? Mbona anazidi kujidhalilisha, angenyamaza tu
 
Alikuwaje daktari bila kuwa na akili?Huko rumande alikwenda kuzaliwa upya akawa na akili mpya?

Alitaka atangaze mlipuko atumbuliwe kama aliyetangaza uwepo wa Zika?
 
Alikuwa ana ogopa kutumbuliwa kama wao wanavyoogopa kutumbuliwa na Magufuli kama watatangaza janga la njaa ambayo inawakabili wananchi ndio maana DMO hakutangaza janga la kipindupindu.
 
Issue sio mamlaka ya sheria kwa uzembe uliofanyika. La hasha anadhani ilibidi amtie adabu mbona tungepelekana mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka clearly that is a violation of ones right. Eti unampeleka rumande apate akili na hawa human rights kauli kama hizo awaoni kasoro zake.
 
Mpaka uwe daktari inachukua miaka mitano chuo ukisoma, mpaka kuwa mkuu wa mkoa inakuchukua miaka mingapi chuo? Ukipata jibu utajua nani hana akili
Kuwa Daktari huchukua miaka mitano ya shule pamoja na mwaka mmoja wa internship hapo ndo unakuwa daktari wa kawaida but ukitaka kuwa na heshima ya udaktri, ongenza miaka mitatu ya residency jumla inakuwa miaka tisa na kwa ma DMO walio wengi wamesoma miaka 9 na wengine wapo hapa tunasoma nao. Kwa kifupi inaudhi na inatia hasira nisome miaka tisa halafu mwanasiasa tu hata shule hana anakuja kukuweka ndani kwa umaarufu wa kisiasa na kutafuta sifa za kijinga! Eti nilitaka apate akili! Kati ya yeye na Dr nani mwenye akili? Naunga mkono uamuzi wa Dr kujiuzulu.
 
Daktari hana akili??hivi huwa haugui huyu mkuu?madaktari mmekaa kimya tuu!!nyie wakuu acheni kuchezea taaluma za wenzenu.
Nchi za wenzetu wanasema/wanadai baada ya Mungu ni Daktari huku kwetu ati RC anamweka ndani Daktari iliniuma sana ni udhalilishaji wa hali ya juu,
 
Rehema Nchimbi amehamia Singida miezi kama mitatu kutokea Njombe.. is it fair to judge kwamba ameshidwa kufanya kazi yake kwa muda huu mfupi?
Kwa hiyo una mtetea? Kamwambie ameshindwa kazi, kama Daktari kamuweka ndani, bwana afya kamfanya nini? Au mimi ndio sielewi? Naomba ufafanuzi
 
Majibu ya mlevi wa madaraka! Pamoja na mkwara wa Waziri kuwa Ma-RC/DC wasiwaweke ndani watumishi wa afya, haitasaidia lolote kwa sababu sheria inayowaruhusu kuweka ndani watu kwa muda wa masaa 48 bado ipo na itaendelea kutumiwa vibaya!
 
Ndio maana hatuwezi kukubali Bashite aachwe hivihivi, yaani mtu kafeli hadi darasa la 4 halafu anajiona Mungu mtu, hii ni dharau. Kuna umuhimu wa kuangalia elimu pia kwenye teuzi za u-dc na u-rc
 
madaktari mmesikia huyu mtu akiumwa akaja kwenu nadhani mnajua mumsaidiaje...ingekuwa mi daktari hahahaa Kama anaumwa akaja kwangu nampa nusu kaputi alafu "namtibu tartiiibu"
Mchome maji au aondoke zake ukikaa naye Muda mrefu utamuhurumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…