RC Paul Makonda na matendo yake

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
597
2,225
Mkuu wa mkoa ulitangaza hadharani kuwa unashughulika na wakosoaji wa serikali unataka kutuaminisha mpango wako ulisimama baada ya kauli hiyo? Maana baada ya kusema maneno haya mambo yalianza kubadilika kweli kweli.

Mkuu wa mkoa, najua HON. John pombe Magufuli hawezi kukunyang'anya wadhifa wako kwa haraka hivyo licha kwamba hakuna ukichowafanyia wakazi wa Dar es Salaam cha maana vyote ni 0.

Kuanzia mipango ya kumuunganishia mambo ya siri sana siyo mpaka taifa litambue vyote vinabuma ila nataka kukushauri jambo moja. Kichwani mwako una vitu vingi vizuri ila shida huna mipango sahihi; kila kitu kwako ni kukurupuka ndiyo maana hakuna kitu ulichokifanikisha zaidi ya kuwa kama upepo wa vuli bila kukamilika mambo.

Mkuu wa Mkoa, usione watu wanaogopa kukukosoa, sema wameshakujua wewe ni nani nyuma ya pazia ndiyo maana wamenyamaza, ila unajulikana sana wewe ndiyo mratibu mzima wa njama mbaya na chafu kwa taifa hili.

Yule Mungu unayemlilia huwa sijui ni wa mbingu ya ngapi, maana mikono yako imejaa ufisadi na damu za roho za watu.

Mkuu wa Mkoa unakumbuka sakata lako la madawa ya kulevya ulivyopiga hela nyingi? Hata ile gari si ulipewa kama hongo kipindi cha sakata la madawa ya kulevya? Hakika wachungaji waliokuwekea mkono kukuombea walikuwa mazimwi maana ule ilikuwa ni mpango uliokufaidisha wewe binafsi.

Mkuu wa Mkoa, kwani nani asiyejua Tanzania ina miiko yake na hatukubali vitendo vya ushonga tangu Nyerere hadi Mkapa ila kimataifa bado mtu akiua siyo kwamba naye auliwe.

Hata wewe Mkuu wa Mkoa ulipochukuwa vyeti na jina ambalo siyo yako hakuna mtu aliyevunja sheria juu yako; ndiyo maana hata Marekani imejithibitisha na kukuitwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda badala ya kukuvunjia heshima ya kukuita muuaji au katili wa haki za binadamu, hivyo haki ya kibinadamu ni msingi ndiyo maana zikawepo sheria za haki za binadamu.

Mkuu wa Mkoa, jambo la mwisho leo umewekewa wewe zuio la kuingia huku Marekani ila kumbuka kupitia wewe unachafua taswira ya nchi.

Ndio mara ya kwanza kwa Mtanzania kuwekewa vikwazo. Hiyo siyo sifa ya Mtanzania maana kikao kinachofuata ni namna gani kuiwekea vikwanzo serikali ya Tanzania.

Ningekuwa wewe ndio mimi ningejing'atua madarakani kwani utafanya Rais Mafuguli kuendesha nchi kwa shida sana.
 
Sijui kama hata nguvu ya kushika Simu na kuingia JF anayo bwana Dab, huko alipo anakufa kwa kihoro saizi.
 
Hili lijamaa la dar limeleta nuksi kwa taifa zima, tulikatae pamoja na aliyemweka kwenye wadhifa huo wote lao moja.
 
Back
Top Bottom