RC Mtwara amtupa selo Afisa kiwanda cha Dangote

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amemwagiza kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya kumuweka ndani ofisa kazi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Nadhiru Omary kwa madai ya kushindwa kutatua malalamiko ya wafanyakazi ambayo yanaelekezwa katika ofisi yake.

Byakanwa ametoa maagizo hayo leo Jumatano, Jana Machi 7, alipofika kiwandani hapo baada ya baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kugoma kuendelea na kazi kwa muda usiojulikana kwa madai mbalimbali.

Wafanyakazi hao wanadai kunyanyaswa, kutolipwa mishahara yao kwa wakati na kufukuzwa kazi bila kuzingatia sheria.

“Tangu nimefika hapa wewe bwana umelaumiwa na umetuhumiwa kwa mambo mengi,hata vikao vyote tulivyokaa hujabadilika, kwa sababu kama ungebadilika taarifa hizi tungezijua mapema,” alisema na kuongeza kuwa:

“Sisi kama Serikali tungekaa na watumishi hawa kabla hawajaanza kuandamana, RPC huyu akapumzike kwanza, kamata huyu mtu tuondoke naye hatuwezi kuendelea na watu ambao badala ya kusikiliza malalamiko ya watu.”

“Kama unakaa sehemu ya kazi halafu chama cha wafanyakazi hakipo na ofisa kazi hauchukui hatua zozote unapoteza sifa zote, inaonekana ni tatizo la kudumu na ni tatizo sana.”

Mhasibu idara ya usafirishaji kiwandani hapo, Justie Fumbuka ameiomba Serikali kuchunguza utaratibu wa utoaji vibali vya kufanya kazi na kuishi nchini kwa kuwa umegubikwa na rushwa inayotolewa kwa watendaji wa idara ya kazi na Uhamiaji wasiokuwa waadilifu.

“Mchakato uchunguzwe kwani vibali vimekuwa vikitolewa kwa wasio na sifa na ni wanyanyasaji wa wafanyakazi na tunaiomba Serikali iwaondoe nchini mara moja,” ameeleza Fumba mbele ya mkuu wa mkoa.

Machi 3 mwaka huu, waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alitembelea kiwandani hapo na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho na baadaye alikutana na baadhi ya wafanyakazi wakiwamo madereva.

Wafanyakazi hao walimpa malalamiko yao ambapo aliahidi yatafanyiwa kazi baada ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji Machi 15.

Mwananchi
 
Wakuu wa mikoa wamekuwa kimbilio la wananchi

Kigwangalla: Mtahama
Wananchi wamelialia kwa Mnyeti
Mnyeti: Msihame subirini wataalamu wa ardhi wapime

Mwijage: Matatizo yenu yatashughulikiwa kiwanda kikifunguliwa Machi 15
Wafanyakazi wamelialia kwa Byakanwa
Byakanwa: Kamata huyo HR...
 
MAAJABU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO......UKISHAMUWEKA NDANI NDIO MADAI YATALIPWA.........Kwanini usimburuze mahakamani???
 
Aisee,,yaani RC ana mamlaka ya kumuweka ndani mfanyakazi wa kampuni binafsi kisa changamoto za ndani za hio kampuni!??

Nna uhakika mwaka huu mpaka uishe lazima Tanzania tuingize maajabu si chini ya tano ktk top ten ndani ya kitabu cha Guiness!!!
 
Maisha ni kama gwalide. Ukiambiwa nyuma geuka, wa kwanza anakuwa wa mwisho.
 
Tatizo la kiwanda cha Dangote limeanzia mbali, na tatizo lililopo pale ni uzembe uleule wa mamlaka kwa maana ya wizara ya kazi, Osha nk kushindwa kufanya kazi yao... Kumuweka huyo ndani ni kama kumfanya mbuzi wa kafara tu, wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo, wageni wahindi wapo kiwandani kiholela kifupi wengi ni vilaza aka kamlete kutoka india, Usalama wa wafanyakazi kazini mdogo, hakuna standard ya kazi kifupi hakuna kigeni watu wetu wanaweza kujifunza hapo..

Ni vyema pia serikali ikavipitia viwanda vyote wa wahindi na wachina Tanzania hasa dar ili ijionee watanzania walivyo watumwa ndani ya Tanzania na sio hizi blah blah za kisiasa... UWEKEZAJI WA MCHINA, MHINDI NA MUARABU KWA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA NI HASARA TU NA HAKUNA FAIDA YEYOTE.. bado tunamhitaji sana mzungu aje kuwekeza kwa ustawi wa watu wetu kwa maana ya kujua teknolojia na kazi,kwa maana ya usalama kazini, na malipo yanayoridhisha, social interuption ya mzungu huwezi kufananisha na hao jingaz kwa maana ya kujichanganya na jamii kwenye starehe na hata kuchanganya damu..
 
Hii awamu hi tamu sana aiseee
Nasikia na huko shinyanga kuna diwani kampa kichapo nesi hospitalini mbele ya wagonjwa.

Kazi mnayo mwaka huu,.
 
Ni vizuri RC angekaa na management yoote ya kiwanda hapo na sio HR, maana huenda HR anapeleka malalamiko kwenye management juu ya ongezeko la mishahara lakini management ya juu ndio haiji na positive results, Tatizo la kiwanda cha Dangote ni uwepo wa wahindi kwenye management na suluhu ni serikali kuingilia kati na kuweka mazingira magumu ya ufanyaji kazi wa waasia Tanzania hasa wahindi, wachina na waarabu maana hii jamii haina faida kwa watanzania zaidi ya kuongeza kiwango cha umasikini..
 
weka ndani bila kufunguliwa mashitaka kwanza,na siajabu RPC katekeleza amri hii sasa huyu aliyewekwa ndani akikufia hapo mahabusu nani atawajibika wakati hakuna docket hapo?why why nchi yangu karne hii bado tunaendesha nchi kienyeji bila kufuata wajibu wa kisheria?
 
Msimlaumu huyo ofisa au hao wanyanyasaji. Laumuni wazazi wenu waliowaleta Duniani ihali wakijua Dunia siyo sehemu nzuri ya binadamu wa hadhi ya chini kuishi.
 
“Sisi kama Serikali tungekaa na watumishi hawa kabla hawajaanza kuandamana..”

If only..
 
Tatizo la kiwanda cha Dangote limeanzia mbali, na tatizo lililopo pale ni uzembe uleule wa mamlaka kwa maana ya wizara ya kazi, Osha nk kushindwa kufanya kazi yao... Kumuweka huyo ndani ni kama kumfanya mbuzi wa kafara tu, wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo, wageni wahindi wapo kiwandani kiholela kifupi wengi ni vilaza aka kamlete kutoka india, Usalama wa wafanyakazi kazini mdogo, hakuna standard ya kazi kifupi hakuna kigeni watu wetu wanaweza kujifunza hapo..

Ni vyema pia serikali ikavipitia viwanda vyote wa wahindi na wachina Tanzania hasa dar ili ijionee watanzania walivyo watumwa ndani ya Tanzania na sio hizi blah blah za kisiasa... UWEKEZAJI WA MCHINA, MHINDI NA MUARABU KWA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA NI HASARA TU NA HAKUNA FAIDA YEYOTE.. bado tunamhitaji sana mzungu aje kuwekeza kwa ustawi wa watu wetu kwa maana ya kujua teknolojia na kazi,kwa maana ya usalama kazini, na malipo yanayoridhisha, social interuption ya mzungu huwezi kufananisha na hao jingaz kwa maana ya kujichanganya na jamii kwenye starehe na hata kuchanganya damu..
Sasa wewe taja kampuni moja ya mtanzania inalipa vizuri sana ndio uje kuwataja watu kwa asili zao. Dangote ni mnigeria jiulize kwanini anafanya anayofanya. wafanyakazi si wana vibali au? wewe ajiri wa bongo halafu utaona habari yake tukubali ukweli mchungu tunaiba sana na mbaya tunaiba bila kutumia akili hata hao wahindi wanaiba lakini smart.
 
Back
Top Bottom