Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Kiongozi gani wa juu Kituo cha Polisi Kirumba anazuia tuhuma hizi za ulawiti kwa mtoto huyu wa Nyakato - Mwanza?
RC Mtanda ameandika “Namshauri huyo aliyedhurumiwa haki yake kufika pia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Mkoa, kwa Mwanza kila Jumanne tunakutana na Wananchi wenye changamoto za namna hizo, anaweza kuwa hajasikilizwa na taasisi moja lakini Kiongozi wa Serikali katika Wilaya ya Nyamagana ni Mkuu wa Wilaya amuone, yawezekana hajui.
Ameongeza “Asiposikilizwa aje Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siku ya Jumanne kila wiki.”
Ikumbukwe Mdau alisema mtu huyo ambaye amemlawiti Mtoto wa Miaka minne eneo la Nyakato, alifikishwa Kituo cha Polisi akahojiwa, mtoto akatoa maelezo, vipimo vya Hospitali ya Sektoure vikaonesha kweli ameingiliwa lakini hakuna kinachoendelea, akidai kuna mazingira ya Mtuhumiwa kulindwa na Mtu kutoka ‘juu’
Pia soma ~ Sakata la Mtoto aliyelawitiwa Nyakato - Mwanza, RC Mtanda asema suala hilo limefikishwa Mahakamani