PreGE2025 RC Mtanda asisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu

PreGE2025 RC Mtanda asisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ametoa wito kwa wafanyakazi nchini kuhakikisha wanadumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu, akisema amani ni nguzo muhimu ya upatikanaji wa haki na ustawi wa jamii.

Mtanda ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kwimba jana Mei Mosi, 2025.

“Asiyeshukuru kwa kidogo hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru, amani ndio jamvi la upatikanaji wa haki, huwezi kuzungumzia haki kama nchi haina amani, Serikali inawezaje kupeleka maji au shule sehemu ambayo wananchi wanapigana vita?...Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia itaendeleza falsafa ya Baba wa Taifa ya kuhakikisha Jamhuri ya muungano wa Tanzania inakuwa huru, yenye amani, usalama na utulivu". amesema RC Mtanda

Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Mkuu wa Programu kutoka Shirika la WoteSawa, Demitila Faustine ameiomba Serikali iridhie mkataba wa Kimataifa namba 189 unaolenga kulinda haki za wafanyakazi wa nyumbani ili kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira salama, ya heshima na yenye staha kama walivyo wafanyakazi wengine.
 
Wachafuzi wa wamani mnatumia polisi na watekaji alafu mnataka amani.
Yani unizabe vibao alafu uniambie pole.
 
Back
Top Bottom