Kwa hakika kuna mambo yanaudhi sana. Ukifika jioni pale Ubungo makutano na ukauona ule umati wa wadau wakifanya biashara chini ya nyaya za umeme, kando ya mitambo ya gesi, juu ya madaraja, kando ya barabara zenye magari mengi, siku zijazo kutakuwa na magari ya speed kali unabaki unajiuliza, serikali na NEMC wako wapi?
Hivi likitokea lolote baya tutasema ni kazi ya Mungu kweli? Nakuomba Mheshimiwa Makonda kwa kutumia taasisi zako, angalia usalama wa eneo lile. Mapendekezo yangu, ni vema eneo lile libaki kuwa eneo la kupita tu na sio eneo la biashara kama ilivyo sasa saa za jioni.