RC Makonda: Ni marufuku kuwasaidia Ombaomba barabarani jijini Dar

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini Dar Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la Dar wakijihusisha na kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, TAMISEMI pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

Chanzo: Channel ten

My take: Nchi yetu yenyewe omba omba maarufu duniani, halafu unapiga marufuku ombaomba??
 
Makonda, hawa ombaomba wa barabarani wapo karibia dunia nzima, hawa ombaomba wetu ni jukumu la serikali kuangalia jinsi gani ya kuwasaidia sidhani kama wakipata huduma bora wataendelea kuomba huko ni kukwepa majukumu yako.

Uwezi kumpangia mtu kutoa sadaka yake kila mtu anatoa pale anapoona ni sahihi kwake.

Masuala mingine ni ya kibinaadamu hayana uhusiano na siasa.
 
Nchi yenyewe ombaomba, aanze kwanza kuizuia serikali kuomba omba then ndio aje kwa wananchi.
 
Screen-Shot-2016-04-10-at-4.01.04-PM.png

Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dsm Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dsm wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

Source: Channel ten
Sasa alitakiwa atafute njia ya kutokuwepo hao ombaomba siyo kupiga marufuku watu kuwasaidia,hili ata-fail
 
Mnaotetea kuwapa fedha ombaomba barabarani sidhani kama mna nia thabiti ya kuwakwamua hao watu... sana sana mnawapa ziada ya fedha mlionayo ambayo haina uhakika wowote wa kumsaidia huyo ombaomba asiwepo tena katika hayo mazingira magumu...nadiriki kusema mnawaita waongezeke barabarani. mngekuwa mnatoa kwenye vituo vya kulelea watoto wenye mazingira magumu ningewaelewa na ndio hilo mkuu wa mkoa analolilenga hasa.. mwenye sadaka yake kiimani aipeleke pale sio unampa mtu barabarani mwisho wa siku anainywea pombe.
 
Screen-Shot-2016-04-10-at-4.01.04-PM.png

Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda amepiga marufuku wananchi wanaotoa Pesa kwa Omba omba kando ya barabara kwa kuwa wanachangia uwapo wa watu hao huku baadhi ya watu wakiwatumia watoto hao kujipatia kipato kinyume cha sheria.

Akizungumza jijini dsm Bw.Makonda amesema kumekuwa na Ongezeko kubwa la watoto katika barabara kadhaa za jiji la dsm wakijihusisha na Kuomba pesa huku wanaowatuma wakiwa wamekaa pembeni jambo ambalo ni kinyume na sheria lakini pia linahatarisha Usalama wa watoto hao.

Aidha amesema mkakati uliokuwapo kwa kushirikiana na Ustawi wa jamii, Tamisemi pamoja na manispaa kuhakikisha kuwa watoto hao wanakusanywa na kuwekwa katika vituo maalum huku wanaohusika na kuwatumia kufanya kazi hiyo wakichukuliwa hatua.

Source: Channel ten

My take: Nchi yetu yenyewe omba omba maarufu duniani, halafu unapiga marufuku ombaomba??
Mkuu
Huu upuuzi ungeupeleka kule Chit chat au Facebook,ndio stahiki yake
 
Sasa alitakiwa atafute njia ya kutokuwepo hao ombaomba siyo kupiga marufuku watu kuwasaidia,hili ata-fail
Njia mojawapo ni kutowapa hao ombaomba. Unajua ombaomba kwa siku anapata kias gan? Wangekua na nia ya kutoka kimaisha ombaomba kwa wiki anaweza kuwa na mtaji wa kuendesha kibiashara hata cha karanga xema ndo hivo wengi kuomba ndo life style yao
 
Back
Top Bottom