RC Makonda kwa hili hapana..

RC Makonda kwa hili hapana..

Matatizo ya nchi/jiji hayawezi kutatuliwa na Mwanasiasa mfano wa PAUL MAKONDA, ISIPOKUWA wataalamu tu!!
Huyu kijna ana mihemko ya Kupenda sifa na kujifanya anafahamu kila kitu!!

Tunawaomba MIPANGO MIJI +SUMATRA+ POLISI +JWTZ+TISS waachiwe suala la bodaboda.
Paul Makonda should be considered as mkurupukaji and knows nothing about modernity.
 
Exactly!! Mbaya zaidi bodaboda ni kamari inayo kamaria uhai wa mtu, mwendeshaji na mpandaji! Ukifika salama mkeka umetema, likitokea janga mkeka umechanika. Huu ndio ukweli mtupu kuwa BODABODA si kazi.

Huyu RC anawaongezea wachina soko la pikipiki kama walivyopewa mradi wa bandari ya Bagamoyo. Ukimkabidhi rungu nanihii..........
 
-ila si vyema kudharau kazi ya mtu kuna uwezekano kazi unayofanya sasa hivi unaifanya tu kwa sababu huwezi kupata ile kazi ya ndoto yako.
- unaposema bodaboda si kazi, ni wezi, wachafu, wanatuharibia mji, sijui ni mtaji wa kisiasa wapigwe marufuku na blah blah kibao then husemi serikali ifanye iwapeleke wapi baada ya kuwafukuza mjini hapa naona si matumizi sahihi ya akili.
- mimi ni bodaboda na huu uzi nina usoma nikiwa na uchungu kuona kazi yangu ikidhalilika lakini nikikwambia nilichokipata toka nimeanza hii kazi kuna uwezekano watoto wa mama waliochangia huu uzi wataanza kufikiria kununua au kuanza kuendesha...
-P. Makonda kwa maelezo ya humu humu JF niliyosoma anasema lengo ni kutusaidia kuachana na kupeleka hesabu kwa bosi ambayo ni kama 7000-10000 kwa siku inategemea na makubaliano tukopeshwe hizo boda kwa rejesho dogo ili maisha yaendelee....kwa serikali inawezekana maana hizi boda kwa bei ya kibiashara tuseme ni 1.8 but serikali wanaweza wakaagiza kwa bei ya chini na mambo yakaenda..(Tshs 7000/= kwa siku ni nyingi najua hapa JF kila mtu wakisure lakini ukweli mnaujua maana MB zilishushwa humu watu walipiga kelele na tunaona watu wanavyofunga safari kwenda kujiunga vifurushi vya chuo ila yote maisha)
- kazi ni kazi aisee tufanye kazi tufuate utaratibu tusidharauliane kwa kazi tunazozifanya... mimi sio mshabiki wa ujambazi na si kweli kila ajali ya gari na bodaboda basi mwenye boda ndio kakosea....ila waswaili tunaongea saaana ila hatujui kutafuta hela hivi kazi ukawa na malengo hasi uka save 20000/= kwa siku ni ndogo kwa humu JF ingawa kwa wajasiriamali watanielewa hivi kuna haja gani ya kwenda kuajiriwa kwenye viwanda ukalipwa 5000/= kwa kutwa tujiongeze.
- Serikali ituelekeze hasa jeshi la polisi nini cha kufanya yapo tunayaona usiku tunavyokesha mabaya hasa ila kwa figisu tulizokuwa nazo na jeshi letu inabidi ukae kimya na hili linaeleweka na hakuna kinachoshindikana....

n.b
kwa mtakaotaka usafiri wa michepuko yenu mni PM niko hewani muda wote na nitawapeleka sehemu mkapumzike ambako nikiwafikisha hamtajutia na mi ntalamba kamisheni yangu freeesh kwa wenye lodge zao huku na peruzi JF na naingiza hela wakati kuna watoto wakiume huku kila siku utawasikia kuna mshikaji wangu ana mawe ana mawe maae zenu ndio mnatuongezea mapenzi ya jinsia moja mjini humu.......
 
Back
Top Bottom