RC Makonda kwa hili hapana..

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
767
677
RC Makonda wew ni kijana wa mfano kwa sasa, umeonyesha kufanya mengi mazuri.

Kwa hili la bodaboda ebu tafakali kwanza na jaribu kupata mawazo ya wadau hasa Polisi na raia kwa ujumla. hata sisi tunafurahi kuwepo kwa bodaboda maana ni ajira pia zinalahisisha usafiri, bodaboda ni ajira kwa vijana wengi lakini lazima tuangalie changamoto za ajira hii kwa umakini zaidi..

Boda boda kwa makusudi wameuwa watu kwa umoja wao, wanashiriki katika matukio ya uhalifu, wanajeshi lao na wanajiona kuwa wako juu ya sheri, hawataki kufuata sheria. Kwa hiyo kutafuta namna ya kuwaongeza jijini ni kuhatalisha maisha ya wakazi wa Dar.

Kutaka kuongeza bodaboda jiji la Dar esalaam ni kuongeza matatizo kwa raia na pia ni kuwaita vijana walioko vijijini na miji mingine midogo kuja dar. Hii hali itaongeza population dar na baadhi ya matendo mabaya kuongezeka.

Ni vyema sasa ujitahidi kuziondoa pikipiki jiji la dar na sio kuziongeza, tafuta namna ya kuwasaidia vijana kwa njia nyingine na siyo hii ya bodaboda.

Aziondoe jiji la Dar halafu akazibwage wapi?hata huku mikoani tumezichoka boda boda.Malizaneni nao tu!
RC Makonda wew ni kijana wa mfano kwa sasa, umeonyesha kufanya mengi mazuri.

Kwa hili la bodaboda ebu tafakali kwanza na jaribu kupata mawazo ya wadau hasa Polisi na raia kwa ujumla. hata sisi tunafurahi kuwepo kwa bodaboda maana ni ajira pia zinalahisisha usafiri, bodaboda ni ajira kwa vijana wengi lakini lazima tuangalie changamoto za ajira hii kwa umakini zaidi..

Boda boda kwa makusudi wameuwa watu kwa umoja wao, wanashiriki katika matukio ya uhalifu, wanajeshi lao na wanajiona kuwa wako juu ya sheri, hawataki kufuata sheria. Kwa hiyo kutafuta namna ya kuwaongeza jijini ni kuhatalisha maisha ya wakazi wa Dar.

Kutaka kuongeza bodaboda jiji la Dar esalaam ni kuongeza matatizo kwa raia na pia ni kuwaita vijana walioko vijijini na miji mingine midogo kuja dar. Hii hali itaongeza population dar na baadhi ya matendo mabaya kuongezeka.

Ni vyema sasa ujitahidi kuziondoa pikipiki jiji la dar na sio kuziongeza, tafuta namna ya kuwasaidia vijana kwa njia nyingine na siyo hii ya bodaboda.
 
Ifahamike boda boda sio ajira ila ni kazi ya kuwawahisha watu kwenye ajira zao! Kazi hii inatakiwa kufanywa na chombo kimoja cha usafiri! (Maana yake kuboresha usafiri wa umma) hivyo hawa vijana Walitakiwa wawe na kazi za kufanya! Hivyo kiuchumi boda boda na kucheza pool table hakuna tofauti ila wanasiasa wamejitoa uelewa
 
anasema atawapa mikopo ya bodaboda kwa marejesho ya tsh 2500 kwa wiki... kwa maana hiyo kila kijana anayetaka kupata bodaboda atapata..kitakachofuata sijui..
Kina watu wanawehuka bado vijana....ngoja tuone
 
Ifahamike boda boda sio ajira ila ni kazi ya kuwawahisha watu kwenye ajira zao! Kazi hii inatakiwa kufanywa na chombo kimoja cha usafiri! (Maana yake kuboresha usafiri wa umma) hivyo hawa vijana Walitakiwa wawe na kazi za kufanya! Hivyo kiuchumi boda boda na kucheza pool table hakuna tofauti ila wanasiasa wamejitoa uelewa

Exactly!! Mbaya zaidi bodaboda ni kamari inayo kamaria uhai wa mtu, mwendeshaji na mpandaji! Ukifika salama mkeka umetema, likitokea janga mkeka umechanika. Huu ndio ukweli mtupu kuwa BODABODA si kazi.
 
Eti ndo anasema UKAWA hawana chao Dar. Yeye ndo Rais wa jiji na mkoa wa Dar. Hawawezi kuamua chochote bila yeye kukipitisha. Hivi halmashauri zinaongozwa kwa matakwa ya huyu Makonda au kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa? Na je, kila kitakachojadiliwa na kupitishwa na baraza la madiwani lazima kipitishwe na Makonda?
 
Ifahamike boda boda sio ajira ila ni kazi ya kuwawahisha watu kwenye ajira zao! Kazi hii inatakiwa kufanywa na chombo kimoja cha usafiri! (Maana yake kuboresha usafiri wa umma) hivyo hawa vijana Walitakiwa wawe na kazi za kufanya! Hivyo kiuchumi boda boda na kucheza pool table hakuna tofauti ila wanasiasa wamejitoa uelewa
Kumbe hadi wacheza pooltable wanapeleka hesabu jioni kwa bosi wao
 
Kick za ubunge hizi kwa kaasii analivutia jimbo

mbunge? Mbunge my foot! Bungeni ataingiaga kwa njia nyingine na misifa kibao za wafungwa viatu na vyeo vya kupewa kwa kujipendekeza ila sio kama mbunge.
Nirahisi ajipendekeze kwa viongozi wababe wamuelewe na kumpa vyeo ila sio kwa kura za wananchi.

Kama kweli ana hamu ya ubunge ni kweli kabisa kuwa kuchaguliwa na mtu mmoja sio sifa kuliko kuchaguliwa na watu wengi.

Kazi kubwa ya kujipendekeza anayo. Maana kuja kukomboa majimbo ya ukawa kwa kuongeza boda2 kazi anayo. Jitutumue dogo tuone mwisho wa mchezo kama ana ndoto hiyo.
 
Eti ndo anasema UKAWA hawana chao Dar. Yeye ndo Rais wa jiji na mkoa wa Dar. Hawawezi kuamua chochote bila yeye kukipitisha. Hivi halmashauri zinaongozwa kwa matakwa ya huyu Makonda au kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa? Na je, kila kitakachojadiliwa na kupitishwa na baraza la madiwani lazima kipitishwe na Makonda?
Mwache ajidanganye! Hivi hajasikia Ma-DC wanavyotimuliwa kwenye mabaraza ya madiwani maana wao siyo wajumbe! Hata yeye siyo mjumbe hivyo hakika atakuwa anasikia tu kwamba leo meya wa jiji anagawa hela ya mikopo bila yeye kujua! Hii ndo shida ya vijana wakipewa madaraka makubwa! Ukuu wa mkoa wapewe watu ambao ni wakomavu kiakili na kimwili!
 
Kama lengo ni kujipatia sifa yeye mwenyewe ni wazo zuri sana, lakini kama lengo halisi ni kuwasaidia vijana huu mpango sio sahihi, Mimi ningemshauri ahamasishe vijana wajiunge katika vikundi harafu wapewe mafunzo ya kilimo na ufugaji kisha watafutiwe aridhi tena ikibidi nje ya DSM wapewe mikopo yenye masharti nafuu wafanye kazi za uzalishaji huko ,siyo kila mtu awe bodaboda, machinga nk, hizi zilizopo ni zaidi ya mahitaji kwa sasa
 
Wenzake nigeria wamepiga marufuku okada au bodaboda mijini zibaki kijijini na mashambani zirahisishe usafiri.

Wanachafua sana mazingira angalia vituo wanapokesha lazima utakuta taka ni nyingi mabanda ya sigara mengi,mama lishe wengi, wauza samaki wengi na mikojo na mifuko iliyojaa haja kubwa. Ni wachafuzi wakubwa wa mazingira na stendi yai lazima kuwe na pusha muuza bangi na sigara kali.

Hawa watu waondolewe kabisa dsm hatuwataki
 
Back
Top Bottom