RC Makonda atengua uamuzi wa DC wa Ilala

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,590
223,179
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema amepiga marufuku shughuli zote za ibada ambazo zinafanyika katikati ya juma. Hivyo shughuli za ibada zitakuwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayesali katikati ya wiki.

Hata hivyo
RC Paul Makonda ametengua agizo la DC wa Ilala, Sofia Mjema aliyepiga marufuku ibada kufanyika katikati ya wiki, akisema ibada ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. RC amesema wananchi waendelee na ibada bila kuvunja sheria, huku akiwasihi viongozi kuwa makini kwenye masuala ya dini.

Tena kwa kuwa mimi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ibada nazitaka sana kuliko sehemu yeyote ile, kwa sababu huko ndiyo uzima ulipo.
 
Mleta mada ,mada yako ingepata wachangiaji wengi ungeweka heading nzuri mfano Mkuu wa mkoa atengua kauli ya mkuu wa wilaya kuhusu siku za kuabudu.Au omba moderators wabadilishe au post upya .Kichwa ulichoweka hakina mvuto kwa wachangiaji
 
Naunga mkono!
 
Halafu hakuna pahali kwenye biblia pameandikwa siku ya kusali ni ipi mimi siku yangu ikifika kama ni j3 naenda kusali so sioni tatizo.

Makonda yupo sahihi kwa ili uhuru wa kuabudu uzingatiwe.

Naona sasa ivi akili zimeanza kumkaa vizuri hakuna haja ya kuwekeana vizuizi vya kufanya tutakacho.
 
Mleta mada ,mada yako ingepata wachangiaji wengi ungeweka heading nzuri mfano Mkuu wa mkoa atengua kauli ya mkuu wa wilaya kuhusu siku za kuabudu.Au omba moderators wabadilishe au post upya .Kichwa ulichoweka hakina mvuto kwa wachangiaji
Ni moderator ndio karekebisha , nifuatilie vizuri , nyuzi zangu zinalenga kutoa taarifa na kuweka kumbukumbu tu , silengi kuvutia yeyote yule , ukichangia sawa usipochangia pia hewala , kipengere ninachokizingatia ni ile idadi ya walioupitia uzi husika
 
Ni moderator ndio karekebisha , nifuatilie vizuri , nyuzi zangu zinalenga kutoa taarifa na kuweka kumbukumbu tu , silengi kuvutia yeyote yule , ukichangia sawa usipochangia pia hewala .
Kichwa chako Cha habari hakikuwa na habari kilikuwa kichwa kitupu tunashukuru moderator
 
Kuna watu wanajua kuwatia watu ubaya, si dhani Kama Bi Mjema aliishia hapo au alisema hivyo from no where.

Hivi karibuni makanisa yakilokole yameanzisha tabia ya kufanya ibada zao katikati ya wiki mpaka saa sita usiku wakifungulia mziki mkubwa na ukichunguza ndani utakuta wapo waumini wawili au watatu.

Mfano mzuri wale wakazi wa Salasala A Kuna Nabii mmoja anajiita Flora.

Hebu mleta uzi tupe taarifa kamili kabla hatujamchamba mtu kwa uonevu
 
Ni moderator ndio karekebisha , nifuatilie vizuri , nyuzi zangu zinalenga kutoa taarifa na kuweka kumbukumbu tu , silengi kuvutia yeyote yule , ukichangia sawa usipochangia pia hewala , kipengere ninachokizingatia ni ile idadi ya walioupitia uzi husika
Ulichemka bwashee....... Tumshukuru Yehodava kwa kuokoa jahazi!
 
Freeedom of Worship. ......... Hivi hawa watu wanasomaga Katiba kweli? Kiongozi siku zote lazima uongozwe na katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hata kama ni bylaws zinaanzishwa hazistahili kwenda kinyume na katiba.

Mfano hakuna sehemu katiba ya Tanzania inaongelea mambo ya kunywa pombe mchana, Lakini halmashauri zinaweza kutunga bylaw zinazotoa katazo la kunywa pombe mchana ambapo ni sahihi kwasababu sio kinyume na katiba.

Lakini katiba ya Tanzania imetoa uhuru wa kuabudu kwahiyo ni utashi wa anayeabudu kujua tu kwamba you are only free if your freedom does not affect other people.

Kwahiyo saa saba mchana nikapiga magoti pale kwenye ufukwe wa coco beach nikaongea na Muumba wangu bila kumbugudhi mtu nitakua sijatenda kosa lolote

Mungu wajalie hawa viongozi wetu utashi wa uongozi. Wanapokosea mara nyingi sisi wanao ndio tunateseka, Ninajua Baba hutatuaacha katika hali ya majonzi. ni hayo machache tunaomba na Kuamini AMEN.
 
Back
Top Bottom