RC Makonda ashtakiwa kwa kudhalilisha wanawake na kukosa maadili

Sasa kaongeza maadui wengi wakiwa ni maafisa Aridhi,watendaji kata wenyeviti wa serikali za mitaa na wateja waliopora viwanja na wale waliopora viwanja vya wazi.
 
Anaempa masifa anamsifia ndio anamzidisha upumbavu! Matusi yale kwa watu wazima na watumishi sio sawa kabisa! Kazi zenyewe hizo za kuteuliwa bila hata proffesional unatukana watu namna hiyo! Hapana
 
Mimi mama yangu mjane!namuunga mkono makonda..wajane wananyanyashwa sana.nimeshuudia Mara nyingi.
 
Nilisikiliza ile audio.

Wafanyakazi waliokuwa wanapaswa kutoa majipu walikuwa wanalengo kupindisha ukweli. Hawakuwa wazi majibu wanatoa yani ujanja unjanja mtupu.

Huyo Makonda ameona awatolee uvivu palepale. Kuhusu kauli aliyotumia amekosea kiasi kwasababu ukichunguza kauli yake utagundua imejaa jazba. Kwenye uongozi ukifanya maamuzi kwa jazba unatumbukia shimoni.
 
Hivi maisha yake mwisho 2020 au 2025? Baada hapo ataishije?? Kuna maisha baada Magu kuondoka
 
Kwa heshima yote,naomba kukueleza mh.Makonda kama unatusoma humu,hapo Mabwepande ulikosea sana.Hivi huyo mama angekuwa mama mkwe wako au shangazi yako ungemsema na maneno hayo?Taratibu za kuwajibisha watumishi wa umma zinasemaje?ni kuandaa mikutano,kupokea tuhuma na kudhalilisha watumishi hadharani?!Mh.Makonda manung'uniko ya moyoni ya watu wazima hawa yanaweza kukutesa sana baadae.Ulimi ni kiungo kidogo sana,lakini kikitumika vibaya kina uwezo wa kuanzisha vita dunia nzima!
Mimi naomba wazee wenye busara ndani ya CCM muwaite hawa vijana wenu mliowakabidhi serikali na kujaribu kuwafunda kidogo.This is too much!Tena mods muelewe mpaka hapa nimejitahidi sana kudhibiti hisia zangu niandike kwa ustaarabu ili kutoa somo kwa hawa vijana wetu wa leo.
 
Huka makonda huku Ali hapi,, katikati anasimama magu endeleeni kuisoma algebra tu wakuu
 
Viongozi wa uma wakiwa kimya mnalalamika mnawaita dhaifu wakiwa aggressive mnasema madictator

Nyie Bavicha badilikeni
Yote hayo uliyotaja sio indicator ya uongozi bora na imara.Kutukana ndio tulichowatuma?unashabikia upumbav
 
Hahahahah ilibidi wabebe mafaili yote,ili kila kinachoulizwa wajibu kwa uhakika kadiri ya docs zinavyojieleza. kweli sio sahihi alichofanya RC,walihitaji kufanya reference ama wangeambiwa hiyo ishu waje na majibu hadharani. Sijui kama alifanikisha kutatua hilo tatizo hapo mkutanoni bila maelekezo mengine kufanyika ofisini.
 
Kawazalilishaje , mbona mnakurupuka ??

Shida hamtaki kuambiwa ukweli maana asilimia kubwa ya watumishi wa uma ni mabogas sana

Tena alipaswa amchape vibao huyo mtumishi wa uma maana wamezidisha ubwege pambaf kabisa

Watanzania wavivu wa kufikiri na kutenda jinga kabisa

Hivi vyeo vingekuwa vya kitaaluma mi ningeshangaa sana kusikia kilichosemwa! Ila kwa kuwa unapewa kama peremende, acha waendelee na hiyo style. Kwa majibizano haya, na ulichoandika hapa, wote nawaweka kwenye kapu moja, kuwa wote ni vichaa! Kichaa anamtambua kichaa mwenzake bana
 
Nikweli waingereza wanasema kila mtu all ni kichaa isipokuwa kitajulikana aina ya kichaa pindi akipimwa. Mfaransa anasema kila mmoja ni kichaa. Sasa hapo yawezekana Bwana makonda labda katumia franchise principles
muite mtukufu hivyo halafu utajua kama ni tusi ama la.
 
Kichaa ni sifa wala siyo tusi" na ndiyo maana ule utafiti ulisema katika watanzania 4 mmoja ni kichaa....watu acheni kutetea watendaji wabovu ...viongozi wasipokuwa wakali mtaumia nyie wananchi

ulichoandika nacho kimefanana na mawazo ya kichaa. Ukali sio suluhu la ufanisi, wala hakuna chuo kinachofundisha principles za ukali ili eti watu watende kazi. Acha ukichaa wako wewe
 
Mtajuana...si mlizoea kutuzingua tukija kutaka huduma na tumewaajiri kwa kodi zetu, kuna watu wamezoea kufanya mambo kwa mazoea sasa mlichokuwa mnataka ndio hicho! Fanyeni kazi kwa weledi muone kama mtadhalilishwa kama mnavyodai.
kwahiyo matusi ndio tiba kero?
 
Alitoa yasiyofaa kwa watu wazima mfano wa Lowassa, akaamua kutunishia msuli wa zaidi ya baba yake bw. Warioba, sasa katengeneza mfumo wa kuwavunja moyo watumishi wetu. Akimaliza atatukana na Watanzania wote na kujiita "Mungu Kijana"
 
Back
Top Bottom