RC Makonda ashtakiwa kwa kudhalilisha wanawake na kukosa maadili

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,940
NGOME YA WANAWAKE - ACT WAZALENDO
TAARIFA KWA UMMA​

Ngome ya Wanawake ya Chama cha ACT Wazalendo imeshtushwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma zinazoendelea kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Jana, katika mkutano anaouita wa kutatua kero, Bwana Makonda ameendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Watanzania.

Kitendo cha Mkuu wa Mkoa Makonda akiwa katika eneo la Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam kumtolea lugha ya udhalilishaji Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka kwa kumtamkia kuwa; "Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa". kimetusikitisha Sana na tunakilaani kwa nguvu zetu zote.

Kauli kama hii sio tu haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa katika ngazi ya Mkoa lakini pia ni kauli mbaya ambayo ililenga kumdhalilisha na kumvunjia heshima yake mbele ya umma Bi Rehema Mwinuka.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo, Leo tarehe 29.11.2016 imepeleka mashtaka rasmi dhidi ya Mkuu wa Mkoa huyo mbele ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma na utawala bora kuwataka wamuwajibishe kwa kitendo chake hicho cha utovu wa maadili.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inamtaka pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atambue kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, kanuni ya 65(1) inamtaka mtumishi wa umma;

_"kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu"._
Alichofanya Mkuu wa Mkoa ni kumuaibisha na kumtolea lugha ya udhalilishaji Bi Rehema Mwinuka kinyume cha Sheria na Kanuni za Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inaitaka Tume ya Maadili na Utawala Bora ifanye uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yalikiuka sheria ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inayataka pia Mashirika na Asasi mbalimbali zinazosimamia Haki za Binaadamu, Haki za Jinsia na Utawala Bora kupaza sauti dhidi ya kauli isiyo ya kiuongozi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa dhidi ya Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka.

Kadhalika, Ngome na Chama kwa ujumla tutaendelea kuwasemea wanyonge wote popote walipo kwa kadri ya uwezo wetu.

Imetolewa na:
Esther Kyamba,
Katibu,
Ngome ya Wanawake
ACT Wazalendo

Maneno ya makonda alipokuwa akijibizana na afisa ardhi wa Kinondoni
 
Nadhani kama ni kukurupuka itakuwa wewe kuliko wao ambao wamequote na vifungu vinavyowapa nguvu ya kufanya walichoamua kufanya.
Hebu tupe kifungu ambacho kinasupport argument yako tulinganishe

Kifungu gani ?? Mi sina vifungu unavyo vitaka weka wewe ivyo vifungu ambavyo Mimi sijaviweka


Acheni kukurupuka na ningekuwa Mimi mkuu wa mkoa ningemchapa huyo mtumishi wa uma makofi mawili ya motoooo , linchi la wajinga kabisa ilo kila kitu kipo shaghalabaghala arghhhhhh mnakera sana


Endeleeeni kucheza taarabu
 
Watanzania tuache unafiki, kisa kadhalilishwa mama ndio tunasema, n wanaume wangap wamedhalilishwa? Yafaa kupinga vitu viovu ktk s kwa vnavotokea kwa upande mmoja tu bal ata upande mwngn... mm sipingi hatua yenu ya kumshtak ispokua napinga et kwa kua tu katukanwa mwanamama... fikiria anaeambiwa hivo n ndugu yako utajskiaje.
 
Tatzo s ubogas, mbona mtu akshndwa kukz vgezo au kupaform kuna hatua za kuchukua s kumdhihak na kumdhalilisha... fikiria uyu mama n mkwe wako au mama mzaz halafu anaambiwa hivo mbele ya watu kua n kchaa anaetafutwa utajskiaje?

Acha kuleta undugu katika kazi we have to change

Utendaji ukiwa wakueleweka nani atakubugudhi???


Unauliza swali mtu badala ya kujibu anatoa maelezo ukiambiwa utoe maelezo sijui utaleta nini

Hata awe nani wangu kama alikosea ni sawa tuu

NINGEKUWA REGIONAL COMMISSIONER MIMI MBONA MNGELIA SANA ningekinukisha kila siku
 
Acha kuleta undugu katika kazi we have to change

Utendaji ukiwa wakueleweka nani atakubugudhi???


Unauliza swali mtu badala ya kujibu anatoa maelezo ukiambiwa utoe maelezo sijui utaleta nini

Hata awe nani wangu kama alikosea ni sawa tuu

NINGEKUWA REGIONAL COMMISSIONER MIMI MBONA MNGELIA SANA ningekinukisha kila siku
Ndio maana kuna sheria na taratbu nyngn, kama angekua ameshndwa angepeleka mamlaka huska wakamuwajbsha au wqkamfukuza kaz, ila s kumdhalilisha hvo, hiyo haikubalik, n matumiz mabaya ya ofisi, kuna muda anawagombeza watu waliomzd umri, je huku s kutafuta laana kwl? Kwanini asisubr afike ofisin halafu amfukuze kaz haf amgombeshe mbele ya watu?
 
Kichaa ni sifa wala siyo tusi" na ndiyo maana ule utafiti ulisema katika watanzania 4 mmoja ni kichaa....watu acheni kutetea watendaji wabovu ...viongozi wasipokuwa wakali mtaumia nyie wananchi
 
Tatzo s ubogas, mbona mtu akshndwa kukz vgezo au kupaform kuna hatua za kuchukua s kumdhihak na kumdhalilisha... fikiria uyu mama n mkwe wako au mama mzaz halafu anaambiwa hivo mbele ya watu kua n kchaa anaetafutwa utajskiaje?
Ulichoandika ni cha maana sana, ila Siku nyingine ukumbuke kuwa humu kuna bibi na babu zako usituandikie kama Facebook.
 
Kama mtu ni mzembe, ni mzembe tu. Wazungu wanamsemo wao; let's call a spade a spade. Kama mimi ningekuwa mkuu wa mkoa, kwenye hiyo mikutano ningekwenda na "fimbo". Watumishi kama hao ni wa kucharaza viboko tu mbele ya hadhara.
Aaaargh! Inakera sana, uzembe umezidi sana kwenye nchi hii. It's too much!
 
Back
Top Bottom