Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 710
- 1,365
*RC MAKONDA AREJESHA TABASAMU KWA PASCAL CASSIAN ALIEKUWA AMEPOTEZA MATUMAINI YA KUISHI, WALIOSEMA HAWEZI KUPONA HAWAAMINI KILICHOTOKEA*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo ametembelewa ofisini kwake na *Pascal Cassian* ambae amefika kwa lengo la *kutoa shukrani na kumthibitishia kuwa Amepona* tatizo la Mfumo wa *Figo na Kibafu cha mkojo* lililokuwa likimsumbua kwa *muda mrefu* na kumfanya *familia yake kupoteza matumaini.*
Itakumbukwa *RC Makonda* aliona taarifa ya *tabu na Mateso* aliyokuwa akiyapata *Pascal Cassian* kupitia mitandao ya kijamii na kuagiza *atolewe nyumbani* apelekwe *Hospital ya Muhimbili* ambapo alitoa *ahadi ya kugharamia matibabu* yake ndani na nje ya nchi na hivi karibuni alimpatia *kitita cha fedha kwaajili ya Matibabu nchini India, Tiket ya Ndege* kwa watu watatu waliomsindikiza pamoja na *fedha ya malazi kwa siku zote* walizokuwa wakipata matibabu Nchini India.
*RC Makonda amemshukuru Mungu kwa kutenda miujiza kwa Pascal ambae aliondoka nchini akiwa amebebwa huku akiwa na mifuko ya kuhifadhi haja ndogo na leo Pascal anamtembelea RC Makonda ofisini akiwa anatembea kwa miguu na akiwa anajisaidia haja ndogo kama alivyokuwa zamani*.
Aidha *RC Makonda amemshukuru Mungu kwa kumponya mtu ambae baadhi ya watu walisema hawezi kupona* na wengine kusema hadharani kuwa pesa alizotoa *RC Makonda* kwaajili ya matibabu ni *sawa na kutupa pesa kwenye shimo la choo.*
*RC Makonda* amewashukuru watu *wote waliomuunga mkono kwa kumuombea Pascal* hadi ameweza kupona huku akiwataka *watanzania kuwa na moyo wa upendo na kusaidiana.*
Kwa upande wake *Pascal Cassian* amemshukuru *RC Makonda* na kumuhakikishia kuwa *amepona* na sasa anaweza kuendelea na *shughuli zake za kutafuta kipato* kama alivyokuwa awali.
Nae *Mke wa Pascal Cassian na watoto* wake wamesema kuwa awali hao na familia pia *walikata tamaa kwa hali aliyokuwanayo Pascal* lakini *walipata tumaini jipya* pale walipohakikishiwa na *RC Makonda* atasimama *bega kwa bega na familia hadi kuhakikisha anapona.*