RC Makonda anatumia msafara wa magari zaidi ya 35

Ziara yake ni anatatua hizo kero at the spot au anatoa maelekezo papo hapo, huoni utofauti wake? Kwa lugha nyingine kile wabunge na madiwani wanachofanya yeye amekuja kukitatua mojakwa moja na kutoa maelekezo. Kwenye mtaa wetu tulikuwa na kero ya mda mrefu ya mfereji wa kiwanda cha bia kuwa na miondombinu mibovu iliyochokaa inayoshindwa kucontrol maji hayo machafu toka kiwandani na kusababisha kero kwa wakazi, diwani tulikuwa naye Ila hukupeleka kero hiyo sehem husika kwa sababu tu alikuwa akipokea rushwa.
sasa nyie mmechagua diwani wa ccm mkitegemea nini?
 
Kama upuuzi wa kiwango cha kusikitisha ni wa Makonda jioni ya leo akiwa kwenye kitu kinachoitwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi.

Nikiwa niko Jof pub njia ya Ubungo Maziwa nilishuhudia msafara wa magari yasiyopungua 35 yakiwemo ya jeshi la polisi trafiki na FFU yote yakiwa full loaded.

Gari nyingine zote hazikupungua watu wane! Hakukuwa na gari ndogo hata moja VX V8 zilikuwa tano! Shangilieni huu upuuzi lakini mjue hiki kiama ni chetu sote....

- Mkuu wa Mkoa wa Dar anasafiri kwenda kutembelea Wananchi na Mkoa mzima kujua kero za Wananchi, Wahusika wote wa Mkoa Serikalini ni wajibu wao kuwepo kwenye Ziara hizo kwa sababu wao ndio wanaotakiwa kujibu kero za Wananchi hapo hapo,

- Imagine kutoka hoja za list of shame mpaka kwenye Kufikia hoja za kuhesabu magari ya Msafara wa Mkuu wa Mkoa hahahahahaha kweli mmefika mbali sana, poleni sana huko!!

le Mutuz
 
Aisee! Leme reserve my comment at least for now...!
 
Watu kwa uwezo na nafasi zao wanavyowadhulumu wanyonge, wazee,wajane wawatu wamekuwa wakidhulumiwa haki zao, ambao sasa wamepata matumaini baada ya ziara ya makonda kwa kuwa sasa wamepata msaada. Wewe hilo kwako huoni kuwa ni LA maana zaidi kushinda huo msafara wa magari? Ifikie muda tujifunze Ku appreciate kwa mambo mazuri.Tuache chuki zisizo na faida yoyote. Laiti wewe ungekuwa mmoja wa MTU aliyedhurumiwa haki au usiyependa kuona MTU anadhurumiwa kwa sababu tu ya unyonge wake hilo LA msafara wa magari katu lisingekuwa jmbo LA maana kwako.

Una takwiu za watu waliokuwa wamedbulumiwa haki zao kabla na baada ya msafara wa mhe mkuu wa mkoa wa Dar kutatua kero zao?

Watu wanashindwa kuelewa na kukubali ukweli ulio wazi kabisa. Si mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, wala rais wa JMT, JPM, anaweza kutatua kero za wananchi kwa kuzisikiliza tu! Kutatua kero za Watanzania ni mchakato wa kudumu unaohitaji mikakati kamambe na rasilimali. Akijitokeza mtu akadai kuzimaliza ujue anafanya usanii unaolenga "kumjenga".

Vyanzo vya kero vibainishwe, yawekwe malengo ya kutatua kero, ibuniwe mikakati ya kutimiza malengo yaliyowekwa, nk. Kifupi ni zaidi ya suala la maendeleo ya wananchi na utawala bora.

Mambo matatu aliyotaja Baba wa Taifa kwenye miaka 1960 kuwa ni maadui wa taifa hili bado yangalipo: ujinga, maradhi na umaskini. Akataja ardhi, siasa safi na uongozi safi (utawala bora) kama vitu muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Leo hii hakuna Sera na miongozo ya kitaifa. Tanzania ina zaidi ya mikoa 20 na wilaya karibia 130. Kila mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya anatekeleza yanayomjia kichwani mwake. Kazi kwelikweli.

Katika hali hiyo Waziri Mkuu na waziri wa TAMISEMI wanakosa udhibiti ya yanayotendeka mikoani. Ushaidi ndiyo hayo ya akina Makonda.
 
Kama upuuzi wa kiwango cha kusikitisha ni wa Makonda jioni ya leo akiwa kwenye kitu kinachoitwa ziara ya kusikiliza kero za wananchi.

Nikiwa niko Jof pub njia ya Ubungo Maziwa nilishuhudia msafara wa magari yasiyopungua 35 yakiwemo ya jeshi la polisi trafiki na FFU yote yakiwa full loaded.

Gari nyingine zote hazikupungua watu wane! Hakukuwa na gari ndogo hata moja VX V8 zilikuwa tano! Shangilieni huu upuuzi lakini mjue hiki kiama ni chetu sote....
Hajalibiwi
 
Back
Top Bottom