RC Makalla awashangaza Machinga

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
CPA AMOS MAKALLA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM NI MFANO WA KUIGWA JUU YA MACHINGA DAR ES SALAAM.

Shirikisho la Machinga Taifa (SHIUMA) likiongozwa na Mwenyekiti wake, Ernest Matondo Masanja lapongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam kwa mchango wake kwa Machinga.


Nikweli wakuu wa Mikoa kwa uwingi wao wanafanya kazi kubwa sana dhidi ya Machinga ili kulisaidia kundi hili.

Lakini tukubali tukatae Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam anaupigwa mwingi sana. Haijazoeleka kabisa kwa Viongozi wa Serikali kwa mamlaka zao kuwaza namna bora zaidi ya kuwafanya Machinga wawe sehemu ya Dunia hii.

Machinga wapo Duniani kote na wanafanya vizuri na wamewekewa utaratibu mzuri sana kwenye Majiji makubwa na Nchi mbalimbali huko Duniani ikiwemo China, Dubai, Uingereza na hata Marekani. Kwa ufupi sana naweza kusema Machinga wapo Dunia zima na Mhe CPA Amos Mkalla Mkuu wa Dar es salaam ameamua asiifanye Dar es salaam ipo Nje ya Dunia hii.

Hivi karibuni Mhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam aliaidi kuwasafirisha viongozi wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Boda Boda kwenda Nchini Rwanda jiji la Kigali ili kujifunza namna viongozi na Machinga pamoja na Boda Boda wanavyofanya kazi huko.

Hili Nijambo kubwa na lakuigwa na kupongezwa na kila mwenye mapenzi mema na shughuli za Machinga hapa Nchini. Mhe CPA Amos Mkalla ameona mbali sana na hakika anaweza kutufanya Machinga tuone mwanga zaidi katikati ya Giza Nene.

Ikumbukwe Machinga Nchini wanaona kama wanaonewa wanapoambiwa kupangwa kama maelekezo ya Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yalivyopendekezwa na ili kutambulika rasimi.

Sasa kupeleka viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Machinga na Boda Boda, inapunguza malalamiko kwa viongozi wenyewe, dhidi ya maelekezo ya serikali pamoja na Machinga wenyewe kuambiwa yaliyomo kwenye miji ya wezetu huko Nje ya Nchi yetu na hata hivyo kuuona kwa karibu umuhimu wa maelekezo ya Mhe Rais wetu.

CPA Amos Mkalla atakumbukwa sana kwa kazi zake nyingi Mkoa wa Dar es salaam na kwetu sisi Machinga tunaendelea kumuombea sana mbele za Mungu kwa kazi yake zuri kwetu na ameweka Alama (legacy)kubwa sana katikati ya mioyo yetu kote Nchini.

Of course, (bila shaka) kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia na tunaoongozwa ni kusonga sawa sawa na Dira ya kiongozi wetu. Kwa Mikoa yetu yote wakuu wa Mikoa ndio Dira yetu na Kwa Nchi yetu ni Mhe Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Hakika CPA Amos Mkalla ameacha Alama (legacy).

Tarehe 6/02/2023 Viongozi hao watasafiri kwenda Kigali Nchini Rwanda na tarehe 10/02/2023 watarejea kwaajili ya mwendelezo wa kazi kwa ujumla wake.

Sisi Viongozi wa Shirikisho la Machinga Taifa (SHIUMA)Tukiongozwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa ERNEST MATINDO MASANJA, Tunapongeza juhudi za (CPA Amos Mkalla Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam* ambazo ni kubwa sana na zenye tija kwa Taifa letu.

USSR
 
Sasa unasema eti sio enzi za chadema halafu unampongeza makala ambaye ni RC kwani chadema iliwahi kuweka RC DSM?

Kama makala kaweza kama RC basi ina maana RC waliopita ambao pia ni wateule wa CCM ndio walioshindwa
 
Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa unakaribia, ukimuita CPA au vinginevyo haiongezi kitu kwenye utendaji wake, huyo jamaa yako hana ubunifu wowote zaidi ya kuvaa miwani ya jua tu.

Kuwapeleka Machinga Rwanda au popote pale wakati mazingira ni yaleyale na wanunuzi ni wale wale ni ujinga uliojificha kwenye kichaka cha kujifunza.

Makala hana ubunifu wowote ule zaid kinachombeba ni UCCM wake tu na kutumika kama daraja la watawala.
Unapojinadi kuwapeleka Machinga kwenda nje kujifunza umeyaandaa mazingira?

Ni sawa na kutumia fedha za walipa kodi kuwapeleka Walimu kujifunza technology halafu wakirudi wanaendelea kufundisha shule zile zile ambazo hazina hata computer la chogo zaid wanakomaa na machaki yao katika mazingira ambayo hata network hayana.

Kila kiongozi wa CCM ni kichaa sema ukichaa wao umetofautiana kidogo.
 
Hao wahuni wa "Sakalla" wanaojiita viongozi wa machinga hakuna machinga anayewatambua zaidi ya Sakalla mwenyewe. Mwambieni aendeleee na propaganda zake huku akiendelea kuchoma kodi za waTz.
 
Back
Top Bottom