Mkoa wa Dar Una mpango gani na Machinga?

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Habari,

Serikali Ijithamini kuhusiana na suala la machinga.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabiashara wadogo "machinga" kutokana na sababu mbalimbali Ila sababu kubwa ni ukosefu wa ajira nchini.

Raisi Samia Hassan suluhu Mara ya mwisho alitoa tamko la serikali kwa upande wa mkoa kuwapa nafasi ya kufanya biashara kwa utulivu bila kuwafukuza.

Ila suala hilo nimeliona tofauti kwa machinga wanaopatikana maeneo ya kariakoo na ilala boma Leo hii nmeshuhudia wakibuguzwa na migambo na wakichukua vitu vyao.

Je, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla umeshindwa mbinu ya kuwasaidia hawa vijana?

Serikali Ina mpango gani na machinga?

Je, siku wakirudi katika kuiba kwa kupora na kunyanganya serikali Inachakujitetea?
 
Back
Top Bottom