RC Makalla aishangaa Serikali kuu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
14,197
Points
2,000

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
14,197 2,000
AMOS Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ameshangazwa na hatua ya serikali kuu kupeleka fedha Sh. 9.6 bilioni kwa uongozi wa Chuo cha Ualimu cha Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe bila kutoa taarifa kwa uongozi wa mkoa.

Serikali imetoa Sh. 9.6 bilioni kwa uongozi wa chuo cha Mpuguso kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya chuo hicho kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, kilichoanzishwa mwaka 1975 huku miundombinu yake ikiwa chakavu na isiyokidhi mahitaji.

Fedha hizo zitatumika kujenga nyumba 13 za watumishi, madarasa 6, mabweni mawili, ukumbi wa mikutano , ukumbi wa mihadhara, maabara za sayansi mbili, maktaba pamoja na vyoo.

“Uongozi wa chuo hiki muhakikishe mnatumia fedha vizuri na majengo yanayojengwa yawe yenye ubora kulingana na fedha iliyotolewa na serikali,” amesema Makalla.

Aidha Makalla amesema hatua ya Serikali kuu kupeleka fedha hizo mkoani Mbeya bila ya kuutarifu uongozi wa mkoa si mzuri kwani fedha hizo ni nyingi na zinahitaji usimamizi mkali.

“Pamoja na nia nzuri ya serikali ya kuleta fedha hizo ambazo ni nyingi lakini mkoa na wilaya haukupewa taarifa ya serikali kuu kuleta fedha hizo. Mkoa na wilaya lazima zisimamie vyema matumizi ya fedha hizo kama viongozi wakuu na wasimamizi wa shughuli zote.

Ni vizuri Serikali kuu iwe inatoa taarifa kwa mkoa na wilaya pale zinapoletwa fedha kwani fedha hizo ni nyingi na mradi ni mkubwa hivyo kunahitajika uangalizi mkubwa,” amesema.

Doroth Mhaiki, Mkuu wa chuo hicho amesema ukarabati na ujenzi mpya chuoni hapo utaboresha makazi ya wakufunzi na kuongeza morali ya utendaji kazi kwa wakufunzi.

“Katika mradi huu mkubwa unaoendelea, zaidi ya wananchi 100 waliopo wilayani hapa wameweza kunufaika na ajira za muda mfupi kutoka kwa makampuni yanayojenga majengo ya chuo chetu,” amesema Mhaiki.
 
Dundo_Boy

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
2,472
Points
2,000

Dundo_Boy

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
2,472 2,000
Safi sana, watakuja wengine ambao hawajapewa watamuonyesha kazi. Sasa unajiuliza amepataje taarifa....atueleze anaongeleaje kitu ambacho anadai hana taarifa. Akaulize serikali kuu, sio anapayuka tu!. Ngoja atumbuliwe
 
tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,314
Points
2,000

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,314 2,000
Alitaka zipitie kwake azifanyie kama alivyozifanyia Mkuu wa Mkoa wa Arusha??
Acha utoto hujui viongozi wa taasisi za Serikali wanavyohujumu Mali za umma.

Wewe unawaza rambirambi na kebehi kwa viongozi halafu ndiyo unategemewa upewe nchi.
 
lukindo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2010
Messages
8,469
Points
2,000

lukindo

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2010
8,469 2,000
An alert kwa waliopitisha bajeti kwa mbwembwe, wataishia kuona utekelezaji wa 30% huku vilivyofanyika sivyo walivyoviona kwenye vitabu!
 
Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Messages
17,835
Points
2,000

Quinine

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2010
17,835 2,000
Safi kabisa rais hawaamini wakuu wake wa mikoa, mtu kama Gambo kaaminiwa kukusanya rambirambi kazilamba zote, kwa hili nampongeza Magufuli.
 
Kiherehere

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,809
Points
1,500

Kiherehere

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,809 1,500
mil 500 inajenga jengo la ghorofa nne Dar Es Salaam.....hapo hapo, 9.6Bilion, inenda kujenga nyumba za watumishi 13, mabweni 6, madarasa mawili na vyoo???? Hii nchi imejaa utapeli asieee!!!! Hizi kiki....zinawafanya msahau ya jana
 
Tetty

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
26,390
Points
2,000

Tetty

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2012
26,390 2,000
AMOS Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ameshangazwa na hatua ya serikali kuu kupeleka fedha Sh. 9.6 bilioni kwa uongozi wa Chuo cha Ualimu cha Mpuguso kilichopo wilayani Rungwe bila kutoa taarifa kwa uongozi wa mkoa.

Serikali imetoa Sh. 9.6 bilioni kwa uongozi wa chuo cha Mpuguso kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya chuo hicho kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, kilichoanzishwa mwaka 1975 huku miundombinu yake ikiwa chakavu na isiyokidhi mahitaji.

Fedha hizo zitatumika kujenga nyumba 13 za watumishi, madarasa 6, mabweni mawili, ukumbi wa mikutano , ukumbi wa mihadhara, maabara za sayansi mbili, maktaba pamoja na vyoo.

“Uongozi wa chuo hiki muhakikishe mnatumia fedha vizuri na majengo yanayojengwa yawe yenye ubora kulingana na fedha iliyotolewa na serikali,” amesema Makalla.

Aidha Makalla amesema hatua ya Serikali kuu kupeleka fedha hizo mkoani Mbeya bila ya kuutarifu uongozi wa mkoa si mzuri kwani fedha hizo ni nyingi na zinahitaji usimamizi mkali.

“Pamoja na nia nzuri ya serikali ya kuleta fedha hizo ambazo ni nyingi lakini mkoa na wilaya haukupewa taarifa ya serikali kuu kuleta fedha hizo. Mkoa na wilaya lazima zisimamie vyema matumizi ya fedha hizo kama viongozi wakuu na wasimamizi wa shughuli zote.

Ni vizuri Serikali kuu iwe inatoa taarifa kwa mkoa na wilaya pale zinapoletwa fedha kwani fedha hizo ni nyingi na mradi ni mkubwa hivyo kunahitajika uangalizi mkubwa,” amesema.

Doroth Mhaiki, Mkuu wa chuo hicho amesema ukarabati na ujenzi mpya chuoni hapo utaboresha makazi ya wakufunzi na kuongeza morali ya utendaji kazi kwa wakufunzi.

“Katika mradi huu mkubwa unaoendelea, zaidi ya wananchi 100 waliopo wilayani hapa wameweza kunufaika na ajira za muda mfupi kutoka kwa makampuni yanayojenga majengo ya chuo chetu,” amesema Mhaiki.
Nadhani Mkuu wa Mkoa amepitiliza hajui majuakumu yake kama Mkuu wa mkoa na taasisi za Serikali.Hajui kwamba taasisi za serikali ahzireport kwake.

Madaraka bila kuwa na JD ni shida kabisa
 
Forum statistics

Threads 1,390,490
Members 528,186
Posts 34,052,419
Top