RC Iringa: Kuna maafisa wanafokea wananchi, kama huna majibu ya maswali aliyokuuliza mwananchi usimfokee

RC Iringa: Kuna maafisa wanafokea wananchi, kama huna majibu ya maswali aliyokuuliza mwananchi usimfokee

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ameonya na kukemea tabia ya Watumishi na maafisa wa Serikali kuwafokea na kuwatokea kauli mbaya Wananchi pindi wanapohitaji huduma, huku akisema kuwa kufanya hivyo ni utovu wa Nidhamu na kwenda kinyume cha Misingi, taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

"Kama hauna majibu ya maswali aliyokuuliza mwananchi, usimfokee.

Tuna maafisa wanafokea Wananchi, Ulimi katika Utumishi ni Kitu muhimu sana, unaweza ukawa Daktari Mzuri, Mwalimu Mzuri, Afisa Mzuri lakini Ulimi mbaya, watu wanahitaji huduma Yako lakini Ulimi wako unawajeruhi kabla ya huduma"

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, wakati akizungumza na Watumishi wa Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Julai 15, 2025.

 
Na Bado si wamegundua kua watanganyika hawana mtu w kuwatetea masikini.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mimi naomba kuuliza, hivi kuna sheria nchini inayowawajibisha viongozi na ahadi za uchaguzi wakishindwa kuzitekeleza, yan sheria inayowabana viongozi kwamba unapoahidi jambo wakati wa kampeni basi kisheria unatakiwa kuitimiza na ukishindwa kuna adhabu inakufuata, sheria hii au kifungu cha sheria cha namna hii kipo kweli?
Naomba maoni yenu tafadhari wadau
 
Ni kama wafanyakaz wa NIDA mtwara, hata salamu haitikii, wamekunja uso kama vinyago vya kimakonde...,kazi ambayo hata mwanafunz wa kidato cha kwanza ukimuelekeza ndan ya wik moja anaifanya kwa ufanisi, ila wao wanajiona special... Wa****sana.
 
Back
Top Bottom