RC Hapi: Mimi ni mtu hatari, usiniudhi, usinichezee!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.

Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mapolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kusikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa
 
Watayatamka sasa lakini kuna siku yatatamkwa na wengine yakiwalenga wao lakini watataka kuomba msamaha lakini watakuwa wamechelewa kwani adhabu ya Mungu hapa hapa duniani itakuwa imetimia na watakuwa bado wanatafakari na kufikiria pale watakapokufa nini hasa kitatokea kwao kama Mungu amewahukumu hapa Duniani kwa adhabu kubwa hivi je Baada ya kufa itakuwaje?
 
Petro E mselewa

Bongo hakuna kitakachobadilisha kitu mpaka mtakapopata akili ya kujua haki na wajibu wenu hapo nchini na duniani mlikuja kufanya nini kama kutawaliwa kimabavu kuburuzwa au kuongozwa kwa mujibu wa sheria mlizokubaliana
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mspolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kudikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa
Irreparable damage
 
Ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,mdogo wangu na Mwanasheria mwenzangu Ally Hapi. Alikuwa akielekea kutoa amri ya kukamatwa,kuwekwa ndani,kuhojiwa na kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wa Viti Maalum huko Iringa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kadiri ya clip ya video niliyoitazama kwa MillardAyo,kuna Mzee mmoja alilalamika kwa RC Hapi kuwa amebomolewa nyumba yake kwa amri ya Mwenyekiti na Diwani huyo wa CHADEMA. Mlalamikaji akajitambulisha kama Mwenyekiti wa Tawi la CCM.Mwanamama mhusika alijitetea bila mafanikio. Akakamatwa na askari wa kike wa JWTZ baada ya kukosekana kwa askari wa kike wa Polisi.

Kimsingi,maneno ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida kwa Wakuu wa mikoa na wilaya nchini. Yana tija gani? Yaendelee?

Nimeiangalia hiyo clip nimeona aibu yule mama alivyokuwa akizomewa na mijana mike ambayo yawezekana kuwa anaizaa. Kila alipojaribu kujitetea, hakusikilizwa.
Swali mbona Mgambo waliotumwa kuvunja hawakufika kutoa ushahidi. Kwa nini hao viongozi wa CCm waliruhusiwa kuongea wakati mkutano haukuwa wa chama? Anyway mlalamikaji atapewa laki tano sijui zinatoka fungu lipi? Ipo siku. Wamuulize Kenneth Kaunda na marehemu Chiluba mchezo unavyoweza kugeuka. Hata Rais wa Misri alidhani atafia madarakani, ashukuru katolewa jela.
 
Haihitaji kwa mwanamke kusema mimi ni mwanamke. mtu hatari hajinasibu watu watajudge kuwa ni mtu hatari. mengine ni mikwara tu.
 
Tatizo la viongozi kuwa wao ndiyo mspolisi na mahakimu wakati huo huo. Hata rais huwa haagizi hivyo huwa anaagiza uchunguzi na hatua kuchukuliwa. Sasa una muweka mtu ndani baada ya kudikiliza malalamiko ya upande mmoja, je baadaye ikionekana uliye mweka ndani hana kosa utamfidiaje. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi wamekuwa madikteta hawafuati sheria na taratibu kabisa
Wanajaribu kujifananisha na aliyewateua
 
Nimeiangalia hiyo clip nimeona aibu yule mama alivyokuwa akizomewa na mijana mike ambayo yawezekana kuwa anaizaa. Kila alipojaribu kujitetea, hakusikilizwa.
Swali mbona Mgambo waliotumwa kuvunja hawakufika kutoa ushahidi. Kwa nini hao viongozi wa CCm waliruhusiwa kuongea wakati mkutano haukuwa wa chama? Anyway mlalamikaji atapewa laki tano sijui zinatoka fungu lipi? Ipo siku. Wamuulize Kenneth Kaunda na marehemu Chiluba mchezo unavyoweza kugeuka. Hata Rais wa Misri alidhani atafia madarakani, ashukuru katolewa jela.
Niah

Usilinganishe watu wa misri na watu wa bongo

Misri asilimia kubwa wanajitambua na kujielewa same as Zambia though uchumi wao unatofautiana sana

Bongo kuna wajinga na wapumbavu wengi sana

So hayo yakusema wangoje ya misri au Zambia ni ndoto kwa bongo utasubiri sana huko kuna ng'ombe nyingi sana
 
Is very unfortunate wazee wa aina ya Jaji Samata walio tayari kusema, kukemea na kushauri juu ya tabia na maneno kama haya bila woga ni kama kwa sasa hawapo, natamani viongozi wakumbuke unaokua kwenye nafasi hizo na mamlaka hayo hata ukiongea jambo la kijinga bado watu watacheka na kukupigia makofi kila mtu kwa sababu yake ila siku nafasi na mamlaka yakiondolewa ndio wataelewa somo vizuri.
 
Ninyi ni wajinga wala sio madaraka ya kulevya

Mnatawaliwa badala ya kuongozwa karne ya 21 bado mnaishi karne ya 17 ninyi

Nendeni shule mkajitambue zaidi

Mbona hivyo tena Mkuu? Wewe unaunga mkono kuvunjiwa nyumba? au unapinga alichosema RC? Au unapinga vyote?
 
Niah

Usilinganishe watu wa misri na watu wa bongo

Misri asilimia kubwa wanajitambua na kujielewa same as Zambia though uchumi wao unatofautiana sana

Bongo kuna wajinga na wapumbavu wengi sana

So hayo yakusema wangoje ya misri au Zambia ni ndoto kwa bongo utasubiri sana huko kuna ng'ombe nyingi sana
Kweli lakini wakati mwingine, ng'ombe hujirudisha toka malishoni.
 
Back
Top Bottom