RC Gambo: Mazishi yoyote yatakayofanyika mkoani Arusha yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10 bila kujali ugonjwa uliomuuwa marehemu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Mkuu wa mkoa wa Arusha mh Mrisho Gambo amesema mazishi yoyote yatakayofanyika mkoani Arusha yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10 hata kama marehemu hajafa kwa ugonjwa wa Corona.

Gambo amesema mkoa umechukua hatua hiyo ili kudhibiti misongamano ya watu katika kipindi hiki cha janga hili la Corona.

Source ITV habari!
 
Ila bar bado ziko wazi, madukani na masokoni nyomi kama kawaida, mikusanyiko ya ibada kama kawaida, kwenye vifodi kama kawaida, restaurants kama kawaida ila kuzika tu ndo ishu.................
Kwenu wamekufa wangapi kwa maambukizi yaliyosababishwa na maombi ya rais Magufuli??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila bar bado ziko wazi, madukani na masokoni nyomi kama kawaida, mikusanyiko ya ibada kama kawaida, kwenye vifodi kama kawaida, restaurants kama kawaida ila kuzika tu ndo ishu.................
Maajsbu ya Dunia...sijui Ni mganga kaelekeza?!!
 
Wakili Msando ashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada kutoa taarifa kuna wagonjwa wengi wa Corona

Ila bar bado ziko wazi, madukani na masokoni nyomi kama kawaida, mikusanyiko ya ibada kama kawaida, kwenye vifodi kama kawaida, restaurants kama kawaida ila kuzika tu ndo ishu.................
Ndio unapogundua viongozi wa awamu hii akili hazipo kabisa kabisa.
Unazuia makaburini ambako kwanza kuko wazi kabisa lakini unaruhusu misikiti na makanisa ambayo yako locked?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha mh Mrisho Gambo amesema mazishi yoyote yatakayofanyika mkoani Arusha yatahudhuriwa na watu wasiozidi 10 hata kama marehemu hajafa kwa ugonjwa wa Corona.

Gambo amesema mkoa umechukua hatua hiyo ili kudhibiti misongamano ya watu katika kipindi hiki cha janga hili la Corona.

Source ITV habari!
Ombi : Wazikwe na serikali tu
 
Hii marufuku ingepigwa mpaka nyumbani ..nyumba yenye watu zaidi ya kumi wakimbiane

Nguvu kubwa inayotumika kupambana na corona kwenye media kama ingetumika kiuhalisia corona isingefikia hutua hii tuliyopo...tatizo viongozi wamekezana kupambana na corona kwenye vyombo vya habari

Kwa halii hii corona itaisha kwenye media ila mtaani itaendelea kuwepo
 
Mazishi tu ndio yanaleta maambukizi watu wasizidi 10 ila bar, kanisani,maikitini, sokoni huko kote mambo yaende kama kawaida hakuna maambukizi.

Hizi akili za viongozi wetu. Afrika kuendelea ni jambo ambalo ni sawa na jiwe kuzaa mbuzi.
 
Ila bar bado ziko wazi, madukani na masokoni nyomi kama kawaida, mikusanyiko ya ibada kama kawaida, kwenye vifodi kama kawaida, restaurants kama kawaida ila kuzika tu ndo ishu.................
Sijui niseme nini... ila dunia ndivyo ilivyo.
Hii yote katika harakati ya kuleta non sense formality, isijulikane hipi covid na hipi sio covid burial.
 
Back
Top Bottom