Exactly, hujasema hazitakosa kuwepo ,Lakini umesema watu waache kujadili "kisicho cha kawaida" kilichotokea lakini wajadili kutatua "tatizo la ajali za barabarani" .......nikosoe kama nimekosea
Ndipo mimi nikakuambia, ajali zipo na zitaendelea kuwepo kwa sbb zinahusiana moja kwa moja na udhaifu wa kibinadamu....!!
Ralph Nader, Mmarekani mwanaharakati aliyepata kugombea urais wa Marekani, miaka ya nyuma sana, alichunguza jinsi watu wanavyokufa kwa ajali za magari.
Akagundua kwamba, vifo vingi sana vinavyotokana na ajali za barabarani vingeweza kuzuiwa kama magari yangekuwa na mikanda ambayo watu wanafunga wakipanda (enzi hizo magari yalikuwa hayana mikanda).
Ralph Nader akafanya kampeni kubwa sana Marekani kuonyesha jinsi gari likiwa na mkanda na mtu akafunga mkanda, hata kukitokea ajali, nafasi ya mtu kufa au kuumia vibaya inapunguzwa sana na kufunga mkanda.
Makampuni ya magari yakampiga vita.
Hakukubali. Akakusanya watu na kufanya movement kubwa sana. Akaandikakitabu "Unsafe At Any Speed".
Mpaka ikapitishwa sheria kwamba magari yote yaliyotengenezwa kuanzia mwaka fulani ni lazima yawe na mikanda ya kufunga watu ili ikitokea ajali watu wasifariki kwa sana.
Leo hii gari kuwa na mkanda ni kitu standard.
Huyu bwana hakusema "ajali hazitakosa kuwepo" akaridhika. Alichunguza ajali zinatokeaje, akajua kwamba, licha ya ukweli kwamba ajali hazitakosa kuwepo, inawezekana kabisa kupunguza vifo vinavyotokana na ajali. Inawezekana kabisa kupunguza idadi ya ajali.
Nilichosema mimi si kwamba tufute ajali zisitokee kabisa, hilo litahitaji ujuzi ambao hatujaufikia bado.
Nilichosemani kwamba, mbona hata hatujiulizi chanzo cha ajalini nini na tunawezaje kudhibiti hizi ajali?
Ukishakubali "ajali zitakuwepo tu" umekubali kushindwa hata kuuliza maswali ya msingi tu kaunagalia jinsi gani ya kupunguza ajali na vifo.
Kwa habari zaidi kuhusu Ralph Nader na kampeni yake iliyopelekea magari kuwa na mikanda soma kitabu kinaitwa "Unsafe At Any Speed"
Here is the Wiki.
Unsafe at Any Speed - Wikipedia