RC Gambo ameikosea Mamlaka, aondolewe haraka

Ndani ya Sheikh Amri Abeid Arusha. Kuaga miili ya waliofariki kwenye ajali ya basi dogo. Watu 35 wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 wa Shule ya Lucky Vicent.

Nilikuwa Jukwaa kuu. Karibu na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Muda wa salamu za rambirambi ukafika. Wakuu wa kiserikali na kisiasa wakawa wanakaribishwa. Mkaribishaji ni RC Mrisho Gambo wa Arusha. Mwenyeji

Wasaidizi wa Mama Samia wakapata ujumbe mfupi kutoka kwa Mbowe. Wakamletea Mama Samia. Mama Samia akamuagiza mmojawapo amuite RC Gambo ili amuagize jambo. Jambo muhimu la kisiasa na kiserikali. Amri

Mama Samia,Gambo alipokuja, akamuagiza Gambo awaongeze Mbunge Lema na Meya Lazaro kwa watoa salamu za rambirambi. Wakati huo,mzungumzaji alikuwa Ndugu Simbachawene. RC Gambo akatikisa kichwa kumkatalia Mama Samia. Akina Lema hawakuongezwa

Amri ikakataliwa. Mamlaka ikakosewa. Kinachotakiwa sasa ni kumuondoa Gambo kwakuwa Makamu wa Rais,kama taasisi ya pili ya juu nchini,lazima alindiwe heshima yake. Who is RC!?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Mzee Tupatupa wa Lumumba,
Umenena vema! Tatizo la Mkuu wa nchi hamweshimu hata huyo mama Samia! Mnakumbuka kuna kipindi fulani kulikuwa na uvumi kuwa M/Rais alitaka kujiuzulu kwa kufokewa na Magufuli!
Hivo tusishangae kuona alichofanya mGambo ni maelekezo toka juu!!!!
Siyo siri Magufuli ana chuki na Mhe.Lema na upinzani wote kwa ujumla!
Kifupi ni kwamba Magufuli anaendeleza sera za kibaguzi kiasi cha kupelekea kupoteza kabisa kile tulichoachiwa na Mwasisi wa Taifa hili Mwl. Nyerere(RIP).
 
Ndani ya Sheikh Amri Abeid Arusha. Kuaga miili ya waliofariki kwenye ajali ya basi dogo. Watu 35 wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 wa Shule ya Lucky Vicent.

Nilikuwa Jukwaa kuu. Karibu na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Muda wa salamu za rambirambi ukafika. Wakuu wa kiserikali na kisiasa wakawa wanakaribishwa. Mkaribishaji ni RC Mrisho Gambo wa Arusha. Mwenyeji

Wasaidizi wa Mama Samia wakapata ujumbe mfupi kutoka kwa Mbowe. Wakamletea Mama Samia. Mama Samia akamuagiza mmojawapo amuite RC Gambo ili amuagize jambo. Jambo muhimu la kisiasa na kiserikali. Amri

Mama Samia,Gambo alipokuja, akamuagiza Gambo awaongeze Mbunge Lema na Meya Lazaro kwa watoa salamu za rambirambi. Wakati huo,mzungumzaji alikuwa Ndugu Simbachawene. RC Gambo akatikisa kichwa kumkatalia Mama Samia. Akina Lema hawakuongezwa

Amri ikakataliwa. Mamlaka ikakosewa. Kinachotakiwa sasa ni kumuondoa Gambo kwakuwa Makamu wa Rais,kama taasisi ya pili ya juu nchini,lazima alindiwe heshima yake. Who is RC!?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Ha ha ha
RC wa Arusha,
RC wa Dar
 
Ramli chonganishi hii
Bavicha bana,wewe ulimsikia wakati anamuelekeza Mrisho amuingize Lema?Je kama ndio alikuwa anaelekeza Lema asiongee?
Halafu sio lazima Lema aongee,Mbowe bosi wake ameshaongea inatosha kabisa.
Chadema acheni kutafuta kiki kupitia misiba
Lema kwenye misiba/sherehe za CCM ni kama Mzamiaji. Hawampendi hata kumuona. Pole Mbunge Lema unatengwa walipo kama mwenye Ebola.
 
Mkuu tatizo ni kuwa kama amri ya makamu wa raisi iligonga mwamba jiulize huyo Gambo anatoa wapi hiyo jeuri ya ku-punch agizo la mama Samia. Jibu lipo wazi kwa mwenye uelewa.

Kisha tafuta uzi upo humu kauanzisha Mh. Lema mwenyewe upate kujua ukweli kwamba hao sio kwamba walitakiwa waongezwe bali walikuwepo katika protokali na wakatolewa kwa amri ya Gambo.
Na kuonyesha hilo limemkera Mh Makamu wa rais ikabidi awatambue wakati anajiandaa kutoa pole. Sasa asiye jaribiwa au kupangiwa atafanya jambo??
 
.Kiki hadi misibani
Mtu mwenye huzuni halilii kuongea msibani kamwe
hawa tunako elekea watakuja kuombea misiba mikubwa itokee kwao
wapate kiki
Hawa watu ni wabaya sana katika kutafuta kiki kwa misiba.
Waliwahi kuuburuza mwili wa Mawazo toka katoro mpaka Mwanza,eti kuuaga,walipoambiwa huyo kwao ni Geita, rudini Geita wakaisusa maiti kwanza kama wiki hivi halafu wakaiburuta tena hadi geita yote hii wapate kiki
 
Watu kutojiuliza haya maswali, imenifanya nianze kuogopa sana kama taifa tunaelekea wapi au labda tumefika wapi. Kutwa mijadala yetu ni mambo ya kitoto tu.

Nimambo yakitoto kwasababu 90% Mijadala huletwa na watoto,
Huwezi kulilia kuongea msibani
kwamba ndio itawasaidia nini wafiwa!!
Au usipo ongea msibani lema hatajulikana?
Aongee mbowe bado hawa tosheki!!
Hawa watu wana shida sio bure
 
Hawa watu ni wabaya sana katika kutafuta kiki kwa misiba.
Waliwahi kuuburuza mwili wa Mawazo toka katoro mpaka Mwanza,eti kuuaga,walipoambiwa huyo kwao ni Geita, rudini Geita wakaisusa maiti kwanza kama wiki hivi halafu wakaiburuta tena hadi geita yote hii wapate kiki

Ila ninacho kiona ni Watoto wenzie ndio wanashangiria upuuzi huu!!
Unaanzaje kulilia kuongea msibani!!?
Kila mmoja akililia kuongea itakuwaje!?
Tuseme wazazi na Lema nani mwenye uchungu wa msiba ule!!?
Kwanimi alilie kuongea lema na si Mzazi aliye fisha!!

Naona watu hawazeeki mwili bali Akili kwa sasa
 
Mmeona mmemshindwa makonda mmehamia kwa gambo. Anafuata sijui atakua nani?
 
Lema kwenye misiba/sherehe za CCM ni kama Mzamiaji. Hawampendi hata kumuona. Pole Mbunge Lema unatengwa walipo kama mwenye Ebola.
Lema na Mbowe na mkubwa kwa cheo?
Kiki hadi msibani?Na leo ole wake angejigalagaza kwenye mavumbi kama alivyofanya kwenye uzinduzi wa ujenzi wa hospitali
 
kijana Hana adabu kabisa. makufuli anawatia ujinga hawa jamaa wa mikoa
 
Ndani ya Sheikh Amri Abeid Arusha. Kuaga miili ya waliofariki kwenye ajali ya basi dogo. Watu 35 wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 wa Shule ya Lucky Vicent.

Nilikuwa Jukwaa kuu. Karibu na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Muda wa salamu za rambirambi ukafika. Wakuu wa kiserikali na kisiasa wakawa wanakaribishwa. Mkaribishaji ni RC Mrisho Gambo wa Arusha. Mwenyeji

Wasaidizi wa Mama Samia wakapata ujumbe mfupi kutoka kwa Mbowe. Wakamletea Mama Samia. Mama Samia akamuagiza mmojawapo amuite RC Gambo ili amuagize jambo. Jambo muhimu la kisiasa na kiserikali. Amri

Mama Samia,Gambo alipokuja, akamuagiza Gambo awaongeze Mbunge Lema na Meya Lazaro kwa watoa salamu za rambirambi. Wakati huo,mzungumzaji alikuwa Ndugu Simbachawene. RC Gambo akatikisa kichwa kumkatalia Mama Samia. Akina Lema hawakuongezwa

Amri ikakataliwa. Mamlaka ikakosewa. Kinachotakiwa sasa ni kumuondoa Gambo kwakuwa Makamu wa Rais,kama taasisi ya pili ya juu nchini,lazima alindiwe heshima yake. Who is RC!?

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
uongo mtupu
 
Back
Top Bottom