RC David Kafulila: Hii ndio hirizi ya CCM kuitawala Tanzania miaka mingi ijayo

Ni vigumu kutengeneza 'Mass' ya kutosha inayoipinga CCM na kuweza kuiondoa madarakani kwasababu, waliokuwa wakosoaji wa CCM awamu moja wanaweza kuwa mashabiki awamu nyingine na kinyume chake.
 
Baada kuogerea na kupinga selfie kipi wamepata?
Wameuangusha utawala wa Rajapaksa ambao uliigeuza nchi kama mali ya familia, na wamepeleka ujumbe duniani kuwa nguvu ya umma haijawahi kushindwa ikiamua jambo.
 
Hayo maneno anayosema Kafulila ni kwakuwa yuko kwenye asali. Ni kama vile mwanaume ukimchukua mwanamke yoyote hata chagudoa unamwambia unampenda sana kwakuwa yeye ni mzuri. Utashangaa huyo mwanamke anavimba kichwa hata kama ni maneno anayoambiwa na kila mwanaume hata waliyeachana.
Umenivunja mbavu! Halafu kiongozi msomi anapotamka mambo kama mahirizi nk. naona kama anajidhalilisha, anajieleza alivyokuzwa na imani potofu na anashindwa kuachana nazo hata baada ya kuelimika. Pfuuu inanuka!
 
Umenivunja mbavu! Halafu kiongozi msomi anapotamka mambo kama mahirizi nk. naona kama anajidhalilisha, anajieleza alivyokuzwa na imani potofu na anashindwa kuachana nazo hata baada ya kuelimika. Pfuuu inanuka!
Hiyo ni lugha ya picha
 
View attachment 2301176
===
Katika mahojiano yake na EFM redio mkuu wa mkoa Simiyu Mhe David Kafulila amefafanua juu ya maasi yanayoendelea nchi za wenzetu na hatma ya

ukuaji wa uchumi wa Tanzania katika mizozo hiyo,

Mhe Kafulia anachambua Machafuko na matokeo yake kwa nchi zingine na namna yanavyoathiri uchumi wetu, hii ni baadhi ya michango ya RC Kafulila,

Swali, Tanzania tuna somo gani la kujifunza kutokana na machafuko yanayoendelea nchi za wenzetu?....

"Kwanza tukubaliane huwezi kujenga uchumi wala kuleta maendeleo kukiwa na machafuko ndani.

Ndio maana kazi ya kwanza ya Rais yeyote duniani ni kuhakikisha utengamano( stability) kwanza kabla ya agenda yoyote.

Rais wa awamu ya sita, Mhe Samia Suluhu Hassan unaweza kumuona vizuri katika hili na namna alivyoituliza nchi kwa sasa,

Maono yake Mhe Samia Suluhu Hassan ni kujenga Taifa ambalo wote tunakuwa sehemu ya ujenzi bila kujali tofauti za vyama, rangi, kabila wala asili yoyote bali uwezo tu wa muhusika.

Wote tunajenga kwapamoja , "Upinzani na CCM" Kwa kujenga pamoja nchi yetu kwa Upendo na Amani,

Mzee Makamba anasema tunakula asali kwa pamoja kwa maana ya "Ustawi wa Taifa kuwanufaisha watu wote",

Na hii ndio nguvu asilia ya Chama cha Mapinduzi CCM.

CCM ni chama kikongwe lakini wakati wote kinaonekana ni "chama cha kisasa" ni kutokana na kujibadilisha badilisha ili kukidhi mahitaji ya wakati husika,

Kwamfano tu,Leo hii Wakosoaji wa CCM huwezi kuwakusanya kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya hii ya sita ukawaweka kapu moja.

Kwani wanabadilika awamu moja na nyingine, CCM inawa' swap'...

Tanzania,ndio maana ni ngumu kutengeneza 'Mass' inayoipinga CCM kutosha kuiondoa madarakani kwasababu , waliokuwa wakosoaji wa CCM awamu moja wanaweza kuwa mashabiki awamu nyingine na kinyume chake.

Hii ndio 'hirizi' ya CCM. Hakuna muujiza zaidi ya kujibadilisha kukidhi mahitaji ya wakati na hili linaifanya CCM itawale kwa miaka mingi zaidi ijayo,
Kazi nzuri Rais Samia
 
Kafulilaaaa 😂🤣🤣🤣 kamtekenya aliyembeba, watu wamemla kichwa! Chalamila aliyebaki kimya kaonekana ana busara zaidi.
 
Back
Top Bottom